Lowassa na Drunken Master Kungfuu style

Lowassa na Drunken Master Kungfuu style

Hayo pia ni maoni,kwanini mnapenda kulazimisha,sio lazima lowasa au chadema ipendwe na kila mtanzania.hio ndio maana ya vyama vingi.

Umesomeka na unachosema ni ukweli. Ila kwenye siasa mipasho kati ya watani wa jadi ni vizuri ili kupeana hamasa. Samahani kama nimekukwaza!!!
 
Kwa wale wapenzi wa picha za kichina hususani za Kunfuu mtakua mnaikumbuka ile Style ya Drunken Kunfuu.
Katika hii Style ya Drunken mtu anapigana na adui kwa style ya kilevi, ambapo adui huona anapigana na mtu alielewa sana na dhaifu hivyo huja kichwakichwa akiwa na uhikika wa kushinda kilaini kumbe sivyo kwani Drunken Style iko makini vibaya mno.

Yaani, kama mtu anaanguka vile kumbe ndio anasimama
kama anapepesuka vile kumbe ndio anabalance
kama hakuoni vile kumbe ndio upo kwenye target
kama ana kwepa vile kumbe ndio anashoot
Kama anarudi nyuma vile kumbe ndo anasonga mbele.
kama anajitega vile kumbe ndio anajitegua
kama anatekenya vile kumbe ndio anamenya
kama anahitaji adui mwingine kumbe ndio kafinish mchezo.

Kwa kifupi ni kastyle fulani hivi kanafulaisha sana kukaona ukipenda angalia Move ya Jack Chen "Drunken Master"

Sasa tukirudi kwa Mtaalamu Lowassa anatumia Style hii kwenye Siasa na hapa sasa ndo mtampenda.


Yaani, kama haendi vile kumbe ndio anaondoka.
kama hajibu vile kumbe ndio kaelezea.
kama CCM hawamuogopi vile kumbe ndio full kuufyata.
kama mjinga vile kumbe ndio full Genius.
kama hajuijui vile kumbe ndio full Brain.
kama hapendwipendwi hivi kumbe ndo full mahaba
kama anaanza kuongea vile kumbe ndio kamaliza.

kwa hikika Style ya Kampeni za Lowassa ni kama Drunken Master Kunfuu Style nimeipenda sana.
Tutaifanyia evaluation Novemba kuona impact yake.
 
Back
Top Bottom