Kampeni za Ubunge ZNZ zaibua mengi, Maalim 'amuumbua' Kinana, baba amkana mwana, Lowassa na mahaba

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
Nimefuatilia uzinduzi wa kampeni ktk Jimbo la Dimani kule Znz.Mkutano ulifanyika ktk uwanja wa skuli ya Fuoni.Katika machache "yaliyonivutia" ni hotuba ya Lowassa.Kwa kweli kwa hotuba tu,Mzee wangu hajambo!!Kwanza alianza na salamu...Lkn pili akamshukuru Maalim Seif kwa kumualika ktk "sherehe" hiyo hapo Dimani.2020 UKAWA andaeni hii nafasi...msirudie kosa.

Lowassa akataja idadi ya kula alizopata Znz na zile za JPM.Katika idadi yeye aliongoza,kwa hiyo akawauliza kama yeye alimshinda JPM huko Znz akiwa wa UKAWA,kwanini waseme Shein alimshinda Maalim Seif na huko ndio "ngome" ya CUF?Ukisikiliza "vigongo" vya hotuba hizi basi unaona kwanini Mzee kaamua hii mikutano isiwepo mpaka 2020.Kuna mengi sana yangetibuka.

Maalim Seif akazibua siri,kuwa kumbe hata yale mabadiliko ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya chama yalifanyika bila hata Kinana kuelewa lolote;yaani hata yeye kaja kuyasikia tu mkutanoni kama vile mjumbe kutoka Wilaya ya Kalambo alivyoyasikia mlemle ukumbini Ikulu.MaalimSeif anasema

"Kinana weee... hujui yanayoendelea ndani ya chama chako, utayajua ya nchi wewe? Ikiwa kumefanywa mabadiliko makubwa ya muundo wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu ya chama chako na pamoja na kuwa Katibu Mkuu hukuwa ukiyajua, umeyasikia vikaoni kama wajumbe wengine, utayajua ya nchi wewe?"

Hii inastua!!Kwamba kumbe hata Kamaradi Kinana yanayoendelea ndani ya chama hayajui??Hii inaweza kuhitaji aya mpya na bandiko jipya.

CCM waitazame Zanzibar kwa jicho la mashauriano na si kwa ubabe.Hata baba wa mgombea wa CCM jana alitoka hadharani na kusema yeye atamuunga mkono mgombea wa CUF,si kwa sababu hampendi mwanae,bali hapendi dhulma ya Chama ambacho mwanae anagombea.

Wakati wa Ukoloni kulikuwa na msemo unasema Hence the saying: 'If the Sultan's drums sounded in Zanzibar, residents of the Great Lakes would dance to their rhythm"

Yanapofukuta Zanzibar,bara na Maziwa makuu hutikisika...Tuyapoze ya Znz,ili tusicheze ngoma yao.
 
Seif anashangaa Kinana hakujua Mabadiliko ya Halmashauri ya CCM lakin yeye hajishangai kwa kutojua kuwa The Professor alikuwa anarudi kwny Uenykt wake Taifa CUF!

Lowassa anayatambua Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Muungano kutokea Zanzibar kwa kuwa tu kule aliongoza lakin akitajiwa Matokeo ya Maeneo aliyokataliwa anasema Tume si huru sasa sijui Yale ya Zanzibar yalisimamiwa na Tume huru?

Kama Seif alijua mpaka taarifa za ndani kutokea Ikulu kuwa Kinana hakushirikishwa kwny Mabadiliko ndani ya Chama kwanini hakujua kuwa Mwenyekiti wake anarudi kwny Himaya ya Uenykt?

Lowassa asipeleke Fitna Zanzibar, Kama kudai kuibiwa kura wote wanadai wameibiwa kwanini Lowassa yeye anamtambua Dr. Magufuli lakin anamchochea Mwenzie kutomtambua Shein?
 
Show Ndiyo kwa inaanza
"HAKI YA MTU HAILIKI NI, TUNGU AMBIZANENI MLOILA. "
Nenda tena shuleni ukasome ili uandike kitu kinachoeleweka.

Lkn pia usitumie kichwa cha mwenzio au akili ya mwenzio kuwaza. Jaribu kutumia akili yako hata kiasi kidogo. Je yeye seif alijuaje kama kinana hakushirikishwa ktk uteuzi wa wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa? Ukipata hilo jibu basi za kuambiawa changanya na zako.
 
Sawa ngoja niende shule
 
Seif anashangaa Kinana hakujua Mabadiliko ya Halmashauri ya CCM lakin yeye hajishangai kwa kutojua kuwa The Professor alikuwa anarudi kwny Uenykt wake Taifa CUF!

Lowassa anayatambua Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Muungano kutokea Zanzibar kwa kuwa tu kule aliongoza lakin akitajiwa Matokeo ya Maeneo aliyokataliwa anasema Tume si huru sasa sijui Yale ya Zanzibar yalisimamiwa na Tume huru?

Kama Seif alijua mpaka taarifa za ndani kutokea Ikulu kuwa Kinana hakushirikishwa kwny Mabadiliko ndani ya Chama kwanini hakujua kuwa Mwenyekiti wake anarudi kwny Himaya ya Uenykt?

Lowassa asipeleke Fitna Zanzibar, Kama kudai kuibiwa kura wote wanadai wameibiwa kwanini Lowassa yeye anamtambua Dr. Magufuli lakin anamchochea Mwenzie kutomtambua Shein?
Pole sana najua inakuuma sana, narudia tena kwa heshima na taadhima nakupa Pole
 
Nenda tena shuleni ukasome ili uandike kitu kinachoeleweka.

Lkn pia usitumie kichwa cha mwenzio au akili ya mwenzio kuwaza. Jaribu kutumia akili yako hata kiasi kidogo. Je yeye seif alijuaje kama kinana hakushirikishwa ktk uteuzi wa wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm taifa? Ukipata hilo jibu basi za kuambiawa changanya na zako.
Wewe naye rudi shule ujifunze jinsi ya kufikiri na kusoma vizuri. Unasema uteuzi wa wajumbe wa NEC badala ya utenguzi wa zaidi ya nusu ya wajumbe wa NEC.
 
Kumbe ndio maana Kinana anakomaliaa kupumzika! Fikra za one man show! Anakuja na majina mfukoni kama yeye alivyopatikana!!!
 
Back
Top Bottom