Kaka,
Napata shida moja. Unasema hawa watatu hawafai. Ninavyofahamu mimi kwanza hawa watatu hawajasema watagombea, wanahisiwa tu. Aidha huendi mbele kutaja basi nani anafaa hata huko nje ya CCM. Mie kwa maoni yangu, suala zima la kugombea urais ni premature halafu tumejifunga sana kwenye majina machache ndani na nje ya ccm. Inawezekana baadhi ya majina ya ccm yasifae, lakini majina yanayotajwa chadema yaani mbowe na slaa pia hawafai. Kwa maneno mepesi, kwa kufuata hoja yako tunaweza kusema kuwa hatuna wagombea 2015. Naamini kusema huyu anafaa na huyu hafai ni kujipofusha. Tunaweza tu kusema huyu anafaana huyu hafai pale tutakapowapambanisha na wengine. Hadi sasa hatujampambanisha yoyote kuhusu urais tunachoongelea ni hisia tu na mapenzi yetu binafsi juu ya historia zao na nafasi zao walizonazo sasa. Tutamjua mgombea anayefaa atakapopambanishwa na wengine ndani ya chama chake kwenye primaries ambako wote wanaojihisi wanafaa watachukua fomu kuomba kuchaguliwa.
Kwa uelewa wangu mfupi, hadi sasa hakuna chama chochote ambacho kimeshafanya mkutano mkuu, CCM ni mwaka huu na CHADEMA nadhani ni mwaka huu au mwakani. Mikutano hiyo na safu mpya za uongozi zitakazotokana na mikutano hiyo ndio itatupa viashiria vya aina ya wagimbea watakaojitokeza na wenye uwezekano wa kupitishwa na vyama. Mathalan, baada ya mkutano mkuu, taswira ya NEC na CC ya CCM ikabadilika na kuingia watu wa mlengo wa Lowassa au Membe au Sitta tunaweza kubashiri ni aina gani ya mgombea atasimamishwa na CCM, maana mgombea hajisimamishi mwenyewe bali anasimamishwa na vikao vya chama. Vivyo hivyo, Baraza Kuu na Kamati Kuu ya CHADEMA nayo ikabadilika wakaingia watu wa maeneo mengine wenye kupinga ukristo na ukaskazini tunaweza kubashiri ni aina gani ya wagombea wenye uwezekano wa kupitishwa na kushinda.
Kwa kumalizia tu, tunapaswa kujiuliza, kwani watanzania ni raia wenye kufaa hadi wapate mgombea urais anayefaa? Kiongozi wa Tanzania atatokana na sampling frame iliyopo, kama Mbowe, Slaa, Lowassa, Membe na Sitta ndio waliopo kutokana na sampling frame yetu basi ndio wanaofaa ukilinganisha na makapi mengine ambayo tunayo. Wananchi irresponsible hawawezi kupata kiongozi responsible kupitia ballot box labda kupitia undemocratic means!