Lowassa, Membe and Sitta: Unfit to Lead, Unprepared to Command

Mkuu chama

Maneno yako yanaonesha Wivu na Inda dhidi ya Mzee Mwanakijiji. Its just prove the inferiority complex whet it comes to mwanakijiji article. Kutoa kwako matusi na Kejeli wala hakuwazuii wengine kusoma Fikra za Mwanakijiji as most of us zimetu inspire and through them we have manage to change other people. Kama huna uwezo wa kwenda toe to toe na MMM acha wanaccm wenzako kama Mchambuzi wajibu hoja

Mwanakijiji atanishinda kwenye riwaya na si kwenye siasa, fikra za mtu pumba zitamuingia mwenye kichwa kisicho na bongo asiyeweza kuchanganyua mambo; mimi sio mtunga riwaya sina hata sababu moja ya kumuonea wivu; hapa naongelea ukweli na ndio sababu anagwaya.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hauna uwezo wa kunishauri kitu chochote. Mwanasiasa anayebebwabebwa na kutumia hila kujipenyeza penyeza hana nafasi katika fikra zangu. Ushauri wako unawafaa wana CCM zaidi siyo mimi. Kusoma upuuzi wako hapo juu kunathibitisha tu hoja yangu: kati ya wale wenye madaraka hakuna ndani ya CCM mtu mwenye uwezo wa kuliongoza taifa hili kwa sasa. Kwanza kwa sababu hawana uwezo wa kuinspire na pili hawana uwezo wa kujenga hoja zikasimama zaidi ya kushambulia watu na kujaribu kutafuta ujiko kwa kuwatetemesha wanaotetemeka mbele zao.

Mimi sikushauri nakueleza ukweli acha kuganga njaa kwa kutumia kalamu; mtu mzima ameumbwa na haya; yaani wewe na taaluma yako yote ya uandishi hili ndio jibu ulilokuja nalo baada ya masaa 24? Ndugu yangu kuushinda ukweli huwezi hizi njaa tafuteni namna nyingine ya kuziganga; hebu tueleze nani mwenye uwezo kuliongoza taifa hili; hata hao watatezi wako wanabwabwaja tu hawana cha maan wanchosema; mara eti ohh nakuonea wivu mimi sio mtunga riwaya; mimi nina taaluma yangu. Mimi napingana na wewe kwasababu umekuwa mwandishi asiyefuata miiko ya kazi yako; mnazonunuliwa kusema uongo kwa faida ya taifa au kwa faida ya hao wanaowanunua?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Very low. U can't even build & develop an argument. You've shown us your malicious intent towards the two personalities (MM & Mbowe). Your criticism lacks logical sequence and exclusivity.

Another mwanakijiji? Who was Chadema main supplier? Give the answer then we will start from there! Remember that there is thin line between truth and lies! Bring it on!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mwanakijiji atanishinda kwenye riwaya na si kwenye siasa, fikra za mtu pumba zitamuingia mwenye kichwa kisicho na bongo asiyeweza kuchanganyua mambo; mimi sio mtunga riwaya sina hata sababu moja ya kumuonea wivu; hapa naongelea ukweli na ndio sababu anagwaya.

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu #chama
Ukweli unauma ha ha ha
 
I know who you are now.

Gud day.
aritoine
You can`t fight truth that was simple and honest question; I was expecting best answer but as always with Chadema followers in JF they can`t defend their arguments. So the answer you have is you know who I am? Man be serious !!!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mkuu Albedo
Ukweli unauma na ndio ninaoupigania, hizi njaa tafuteni namna ya kuziganga!!

Chama
Gongo la mboto DSM

Yah sisi tuna njaa iliyosababishwa na ccm na hatuoni ndani ys ccm atayetuokia na njaa hii. CCM Must go and it will go
 
Pamoja na yoote yanayosemwa na kuandikwa, ukweli ni kuwa CCM must go! Tumefikishwa hapa kwa uongozi mbovu wa CCM! Hakuna jipya pale, ni uroho wa madaraka tu waliobaki nao hao wanaotaka kuwa Ma Rais wa nchi hii! Shame!
 
Yah sisi tuna njaa iliyosababishwa na ccm na hatuoni ndani ys ccm atayetuokia na njaa hii. CCM Must go and it will go

...Unless kuna Chama na Viongozi Mbadala walio bora zaidi ya CCM na Viongozi wake hao, otherwise CCM na Wateule wake bado wana nafasi kubwa sana ya kuendelea kutawala nji hii, atleast baada ya uchaguzi wa 2015...
 
attachment.php

Ikulu ya Dar-es-Salaam

Our nation is looking for a new breed of leadership. A leadership that can and will inspire Tanzanians - young and old, men and women, educated and uneducated; of all creeds, of all colors and of all political persuasions - to look within themselves and find greatness that remains unchallenged, untapped and unleashed.

At a time like this where global balance of power in international affairs is shifting; where backward countries - once tormented by civil wars and internal wranglings are finding their rightful place in the community of modern nations Tanzania needs leaders who can stand as beacons of a better and prosperous nations. Leaders unchained from a corrupt mentality of a generation past who are willing to challenge the failed policies of the current ruling corrupt elite.

I do not see anyone from within the same ruling party whose failed polices and ideology of corruption have proved to be a generational catastrophe would stand today promising 'change' or 'better leadership'.

The structural depth of the corrupt mentality of the generation past is so embedded with the ruling elite to the extent that without a total dismantling of the party, a precise prosecution and punishment of corrupt figures within the party there would be no hope for any meaningful change from the same party.

My friends for quite sometimes now prominent figures within CCM namely former Speaker Samwel Sitta, former Premier Edward Lowassa and current Foreign Affairs Minister Benard Membe have tried to position themselves as potential candidates from within the ruling party for the presidency in 2015. The trio have - in so many occasions - tried to show themselves in myriad of ways as 'presidential materials' to contest the presidency against key opposition figures in much awaited General Elections in about three years from now.


The failures of the three individuals to show that they fully understand the fundamental flaws of their party; their failures to appreciate and come to the defense of human and civil rights in the country and more importantly their failures to challenge and criticize the actions of their government - to the point of resignations - lead me to believe that not only Lowassa, Membe and Sitta are not ready to lead our nation and indeed they are unfit to command. Not only have I taken this position against the three individuals - lest I be accused of favouring others - I DO NOT SEE anybody within the ruling party right now who can inspire Tanzania to greatness.

As I said about seven years ago that if Kikwete were to fail to inspire the nation during his tenure at Magogoni then there would be no other CCM candidate who do so in the near future.

The failures of Kikwete's administration coupled with the failures of his party's policies have destroyed any chance for another candidate from within the ruling party to be trusted with power. Kikwete who came to power with such fanfare and an overwhelming mandate has shown that leadership is more than good smiles, handsome faces, or vain promises.

It is about inspiring people, it is about being trusted, it is about bold decisions, indeed it is about improving people's welfare and more. None within the ruling party right now can claim such qualities. I MEAN NONE. If there is one somewhere then he/she is not in the parliament or government position of any sort. But for the three let me be on record -they are unfit to read and unprepared to command.

By. M. M.

Mwanakijiji umeongea mengi, mimi nimesoma heading yako tu, ila ukweli ni kwamba tunahitaji angalau mmoja wao kati yao hao watatu kwenye uongozi wetu wa ngazi ya juu unaokuja, au hata wote ikiwezekana. Tukiwapata wote watatu itakuwa nzuri zaidi, let's hope watakuja kutengeneza kambi moja come 2014, yaani kabla ya 2015.
 
mkuu chama...CCM inaweza kua mbaya kwa watu fulani kwa sababu zao binafsi (wanaona watafaidi binafsi CDM ikiingia madarakani, wanatoka kaskazini, waliokata tamaa kabisa, au ni wale wasio na uwezo wa kuchambua mambo na upeo mdogo). Kwa mtu makini CDM siyo mbadala wa CCM angalau uchaguzi wa 2015 hata ule wa 2020. CCM inahitajika kuongoza kwa sababu sioni umakini wowote wa CDM na viongozi wake zaidi ya kua political opportunists.

Hatuwezi kulitupa taifa kwa mbwa kwa sababu Tanzania haiko katika life support ya utawala wala ya kiuchumi kiasi kwamba tumweke Dr Slaa au Mbowe kama Rais. Hawa siyo hao inspirational leaders MM anaowaongelea hata kidogo na kama hamna mbadala tufanye nini sasa?

Matatizo binafsi ya kiuongozi ya Jk na rafiki zake wachache yasifanywe kuihukumu CCM nzima, CCM bado kuna watu makini na wakipewa uongozi wa juu tutaona tamaduni mpya kabisa ya uongozi haswa katika mazingira haya ya siasa za ushindani.

mimi napenda mageuzi, lakini mageuzi makini siyo kukimbilia kuwapa wapinzani (ambao hawajiandaa) taifa lenye changamoto kubwa kama Tanzania yetu hii. Kila mtu anayetaka CDM ishinde sooner than later kama siyo hopeless youth, (who is filled with anarchy testosterone) basi ni msomi kama MM anayeangalia parochial interests tu.

CDM imejaa question mark nyingi sana kwa mtu makini kuwapa kura leo au kesho. wacha waevolve, wakue, wapate uzoefu kwani tanzania siyo nchi rahisi kuongoza kama wanavyofikiria.

Ningependa CDM waje na comprehensive policies zao kuhusu uchumi, siasa na za kijamii siyo hizi vague statements za M4C au opearation sangara zinazolenga ushabiki tu wa kisiasa kitu ambacho Tanzania haitaji tena kwa sasa.
 
I do support the ideas in your write-up.
Imagine one of them is planning to dream ..., how can you plan a dream. I'm just waiting for a day when he will come before the media early in the morning claiming of having dreamed last night, thus he should contest for presidency and thus he is God's choice.

Membe...... I will live to see it...
 
Mimi nakubaliana na MM kwa kiasi fulani. Sijui misimamo ya Lowassa, Membe na Sitta katika masuala mbalimbali yanayoikabili nchi yetu. Nataka kujua misimamo yao katika vita dhidi ya ujinga, umaskini na maradhi. Misimamo yao binafsi as I do not give a damn about CCM! Mjadala wa namna hii ndio utatupatia kiongozi bora. JK (wa sasa) alichaguliwa bila kuulizwa maswali magumu juu ya msimamo wake katika mambo ya msingi. Akachaguliwa kishabiki tu, kwa rushwa na ahadi za kupeana vyeo na ulaji. Waliotaka mdahalo wakaambulia patupu. Tujadili misimamo ya watu wanaotajwa kuutaka urais 2015, na ikiwezekana tuwaulize maswali wao wenyewe wajibu - wasijibiwe na wapambe!

Tuache sasa huu upuuzi wa kutaka kumhalalisha Lowassa, Membe au Sitta kwa sababu Mbowe, Slaa na Zitto hawafai. Tumkague kila mmoja peke yake, kwa sababu tunapochagua Rais tunachagua mtu na sio chama chake au genge lake. Akiwa wa hovyo, kwa sheria zetu, kila kitu kitakuwa hovyo. Tujifunze kwa JK (wa sasa).
 
Hiyo lugha ni nyepesi tu, majibu anayo ninachokataa ni double standards, mwanakijiji anajua ninachokisema, hawezi kunishika pabaya namueleza ukweli.

Chama Gongo la mboto DSM
Sasa kama wewe chama unaona umeandika in such stylistics and semantics to be contextuously understood by MM you had better cautioned JF members not to disturb themselves and read your comments.

The fact that you have put your remarks at the disposal of the members be so kind and fare enough to respond gently, proactively and strategically to their queries.

But does any vulgar language need be understood by only MM. One member has been shocked such an archaic language "stupid article".

You may not agree to someone's opinions, views and what have but agree to disagree with and that's a sign of maturity. Otherwise your views might be good but restricting other people from commenting to them is quite absurd.

Let us give constructive and informative views for the betterment of Tanzania and Tanzanians of today and many years to come.
 
Ukweli ni kuwa hawa wote ni mazao ya ufisadi, wanajaribu kujitenga na ufisadi lakini uroho wa madaraka na vyeo vimewafanya washindwe kuonyesha ujasiri wao wa kuthubutu na kutenda mambo.
 
Msije mkawa munawa-dis hawa lakini mawazo mwenu kuna kile kibabu kipadri! Huko ni kuruka maji na kukanyaga moto!

Nimekuwa nikisema kila mara na leo narudia tena kusema kwamba MM ni mtu ambaye humu JF anaonekana kama mfalme, kama siyo mungu mtu ambaye wale wanaoumuunga mkono wanafanya hivyo passionately kiasi cha kudhani kwamba kila neno analotamka basi ni gospel truth na hawaamini kwamba anaweza kukosea (na amekuwa akikosea na kupotosha mara nyingi sana). Wala hawajui kwamba ana phobia dhidi ya watu wengine na mania kwa wale aliowachagua in equal measure. Kwa msingi huo amekuwa na prejudices zake dhidi ya kile asichokiamini.

Kwa kukosa balancing na objectivity, ameshindwa kutuambia kwamba kwa vile hawa hawafai na hata chama chao hakifai, then ni nani anadhani anafaa na kwa sababu ipi. Huwezi kusema kwamba eti kwa vile kiongozi fulani hajawahi kukosoa, kujindoa au kutofautiana na chama chake basi huyo hafai au amefeli vigezi alivyoviweka Mfalme MM. Yeye mara zote amejidhihirisha kama mtu anayechukia CCM, tena bila hata sababu za maana. Ingeshangaza kama angewapenda viongozi wake. Ni hoja potofu kusema kwamba kama mfumo fulani au itikadi fulani imefeli, kwa maoni ya mtu mmoja basi hao walio kwenye mfumo huo wote hawafai. Kama ingelikuwa hivyo basi hawa akina Cameron, ambao chama chao kilishindwa au kudumuza uchumi wakati wa akina John Major wasingekuwepo. Na wala kujitoa hakumfanyi mtu kuwa shujaa au kiongozi bora (rejea kujitoa kwa Mrema).

MM ni kada maarufu wa Chadema na hilo siyo la siri na wala isingetarajiwa aipende CCM wala viongozi wake ambao ni mwiba kwa ndoto zake. MM ni aina ya wale watanzania walio nje ambao wamekimbia kulijenga taifa lao, wakiona fahari kuendesha maisha ya watu wengine na huku wakijifanya majasiri na wazalendo wa kukosoa tu serikali iliyoko madarakani bila kujua kwamba kuna mazuri vile vile ambayo yanapaswa kuangaziwa na kupongezwa.

On this MM has failed miserably and has demonstrated the highest degree of partisanship and stereotype that lingers in his otherwise sober mind. I take a serious exception to his line of thinking!
 
Binafsi nimefurahishwa na makala ya mwanakijiji na sishangai anapopata mashambulizi kwani anakabiliana na system iliyotawala kwa miaka zaidi ya 50 mfululizo ambayo imezaa wanayoiunga mkono out of mazoea, wengine maslahi, wengine ushabiki na wengi zaidi ujinga (illiteracy/ignorance). Mimi ni Mwana CCM lakini hiki sio chama ambacho kama ningekuwa nina ‘choice’, ningependa kiwe katika hali ya leo. Lazima tukubali ukweli kwamba CCM imekosa. The only excuse we can have ni kwamba chama “hakijakosa mwelekeo” BUT “kinakoseshwa mwelekeo”. Wana CCM, hivi ni mambo gani ambayo leo hii tunaweza kusimama majukwaani huko vijijini na kujenga hoja kwamba CCM ni chama chao? Zaidi ya kuja na ‘make up list’ ya hapa na pale, kwa kweli hatuna hoja. Tusipoteze muda mwingi kwenda kwa wananchi kuwasemea upinzani, tutumie muda mwingi zaidi kwenda kwa wananchi kurekebisha mapungufu yetu kwa vitendo, hoja na kwa siasa safi.

Makala ya Mwanakijiji inapata upinzani mkubwa kutokana na mtatizo mawili makubwa: Kwanza, wengi tumekuwa wazito kuelewa dhana ya uhuru wa kutoa mawazo. Mimi sioni tatizo kama Mwanakijiji ni mfuasi wa Chadema. Na isitoshe, hata katika siasa za nchi za wenzetu waliokomaa kidemokrasia kwa mfano Marekani, kuna media organizations ambazo zipo aligned na vyama vya siasa na kwa uwazi kabisa. Kwa mfano, makampuni kama FOX, hawa ni republicans, na makampuni kama MSNBC, hawa ni democrats. Lakini pamoja na tofauti zao hizi ambazo hubebwa na utofauti katika ideological following or beliefs, vyama vyote vinasimamia maslahi ya taifa, wanachotofautiana au pishana ni njia ya kufuata towards a better America. Huwa namsoma sana Mwanakijiji hapa JF na kwenye magazeti, na mara nyingi hoja zake huwa ni za maslahi ya taifa kwa kweli kwani zina cut across mtu yoyote mwenye nia njema na nchi yetu. Inawezekana kuna nyakati anaonekana anaegemea upande fulani, lakini kama nilivyokwisha sema, hata kwenye nchi za wenzetu waliokomaa kidemokrasia, hili ni jambo la kawaida.

Pili, wengi wetu humu tupo busy kujaribu ‘to make sense of his (mwanakijiji) language’ in the article instead of making sense of the issues that he is trying to address before us. Makala ya Mwanakijiji leaves us with an important question that is in dispute and must be settled. Binafsi ningependa kuiangalia makala ya Mwanakijiji kwa mapana zaidi, hasa kuhusu suala zima la jinsi ya kumpata rais wa Tanzania. Vigezo na utaratibu uliopo ni kama vile Rais wa Tanzania daima atatokea CCM, and to make matters worse, kuna dalili kubwa kwamba CCM na mashabiki wake wanajikita zaidi kuzalisha marais wengi (quantity) kuliko wingi unaoendana na ubora wa marais hao (quality).
Katiba ya sasa ya Tanzania (1977) ni Katiba ya CCM. Pamoja na kufanyiwa amendments za hapa na pale lakini bado ilitungwa ili kuhalalisha supremacy ya CCM. Ndio maana kwa miaka karibia kumi na tatu (1964 – 1977), tulikuwa tunaongozwa na katiba ya mpito na hatukujali hilo kwani Katiba ya TANU, hasa Azimio la Arusha, na uongozi makini wa Nyerere ulifanya wengi wetu tusijali sana hilo kwani Nyerere alikuwa ana deliver. Ilipofika mwaka 1977, Vyama vya TANU na ASP vikaungana na kulazimisha mabadiliko, na hapo ndipo katiba ya nchi ikazaliwa ili kuhalalisha utawala wa chama kimoja (TANU + ASP = CCM), na ndio maana sehemu kubwa ya mgogoro wa katiba yetu ni the “union question”. Vinginevyo, baada ya 1977, Katiba ya CCM ikawa Superior kwa Katiba ya Nchi. Ipo mifano mingi juu ya hili lakini kwa haraka haraka niseme tu kwamba - viongozi wengi wa CCM na Serikali kwa ujumla walikuwa mara kwa mara wanakikiuka katiba ya nchi lakini hakuna aliyekuwa anawakemea, lakini ilipotokea kiongozi anakiuka Katiba ya Chama, huyo alionekana muasi, mhaini na kila lililo baya. Muundo huu ukatengeneza mfumo mbovu wa kutuzalishia viongozi, na ni hapa ndipo naungana na mwanakijiji kwamba mfumo wetu wa kutupatia viongozi (CCM) leo hii una matatizo.

Kwahiyo, tafsiri yangu ya hoja ya Mwanakijiji ndio hiyo i.e. ‘kimfumo zaidi’ – hasa pale anaposema kwamba haoni jinsi gani CCM inaweza kupata Rais bora ajae ambae atatoka miongoni mwa wabunge (CCM) wa sasa. Tukituliza kidogo akili zetu na kutafakari hili, wengi tutakubaliana na mwanakijiji hata kama haitakuwa mia kwa mia.
Nitajaribu kuichambua hoja ya mwanakijiji kwa kutumia Katiba ya sasa ya Tanzania kwani hiyo ndio inatoa vigezo vya mtu kuwa rais bila ya kujali rais anatoka chama gani. Lakini cha kushangaza kidogo ni kwamba katika mijadala kuhusu mapungufu ya katiba yetu, nje ya suala la umri na mgombea binafsi, hatuangalii sana suala hili la sifa ya mtu kuwa rais kwa mujibu wa katiba ya Tanzania (1977).

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania (1977), sifa za mtu kuwa Rais wa Tanzania, awe:

(a) Ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia;
(b) Ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) Ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) Anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,
(e) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Nitajaribu kujadili vigezo hivi vitano kwa haraka haraka.


  1. Kwanza ni suala la uraia – Siasa za sasa ni zamu ya upande huu au upande ule unatoa mwanya wa kutuletea Ma-rais wabovu ambao wanateuliwa ili kufanikisha zaidi malengo ya kisiasa. Kwa mfano, siasa ya zamu ya bara bila vigezo vingine vya msingi inaweza kutuletea rais wa ovyo lakini pia vile vile siasa ya zamu ya visiwani. Ni muhimu katika kumpata Rais, tukasukumwa zaidi na mahitaji ya watanzania in all spheres (kisiasa, kiuchumi na kijamii) badala ya kusukumbwa zaidi na siasa za muungano.


  1. Pili ni suala la umri (miaka 40). Hili tumeshalijadili sana hivyo nitaliacha kwa sasa.


  1. Tatu ni kuhusu mgombea lazima atokane na chama cha siasa – hili pia tumeshalijadili sana, huku wengi wetu tukihimiza umuhimu wa kuruhusu wagombea binafsi. Lakini ningependa kulisemea kidogo. Kwenye mdahalo baina ya Nape, Mnyika, Naibu Katibu Mkuu CUF (jina limenotoka), Nape alijaribu kujenga hoja kwamba hatuna haja ya mgombea binafsi kwani hata nchi kubwa kama Marekani wagombea binafsi hawana nguvu, hivyo kusisitiza msimamo wake kwamba Tanzania hatuna haja ya wagombea binafsi ndani ya katiba mpya. Hili ni suala ambalo hata Nyerere leo hii angepingana na Nape kwani hata yeye hakuona sababu za msingi za kuendelea kulikataa hilo kikatiba. Lakini nikirudi kwenye hoja ya Nape, anasahau kwamba Rais wa kwanza wa marekani ‘George Washington’, hakutokana na chama chochote cha siasa, na ilichukua muda mrefu kwa marekani kujenga vyama vya maana. Pamoja na kuibuka kwa vyama viwili vya maana baadae, bado katiba ya marekani iliendelea kuwapa option wananchi kuchagua mgombea binafsi. Kinachofanya wananchi wengi waegemee wagombea wa vyama kuliko wagombea huru ni kwa sababu nchi imegawanyika karibia nusu kwa nusu kiitikadi. Hata hivyo, bado kuna majimbo ambayo wabuge wake wanapita kama wagombea huru. Lakini sisi CCM tunafanya maamuzi juu ya suala muhimu kama hili ina top-down fashion, na mbaya zaidi ni katika mazingira yanayotawaliwa na ombwe la kiitikadi (including CCM). Hivi sio kuwatendea haki watanzania.


  1. Nne ni kuhusu sifa Rais lazima awe na sifa za kuwa mbunge: Je ni sifa zipi hizi? Kwa mfano katiba ya Tanzania inasema ili mtu kuwa mbunge ni lazima awe:
· ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
· na miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
· ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
· katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Tayari tumeshaona migongano mingi hapo, na kuna sifa nyingine ambayo sijaiweka hapo ambayo, wakati sifa kielimu (mbunge) ni angala darasa la saba, sifa kielimu (rais) ni angalau shahada ya kwanza.
Wengi wetu katika mjadala huu inaonekana hatupo kumfikiria mtanzania ambae haan nafasi ya ubunge, kwamba bila ya hivyo, mtu huyo hana uwezo wa kuwa Rais na Amiri Jeshi mkuu. Na hawajali kama ubunge wa kipenzi chao ulipatikana kihalali au kwa hila, vitisho, rushwa na ujanja ujanja wa kila aina. Kwa wenzetu hawa, hilo kwa sio muhimu!!


  1. Na mwisho ni juu ya ‘kutiwa hatiani’ kuhusu masuala ya kodi. Kwa kweli hapa tunachezeana tu akili kwani tumezidi kushuhudia jinsi gani wanasiasa wengi wanajificha nyuma ya pazia la ‘innocent until proven guilty’, huku vyombo vyote vya kufanya kazi ya kutia watu hatiani vipo mifukoni mwao. Hivi kweli are we serious na kuachia maadili ya uongozi yapimwe na masuala ya kodi tu? Fine, tuseme suala la kodi ni muhimu, je nani asiyejua kwamba Azimio la Arusha lilivunjwa ili kuhalalisha wanasiasa kuwa na mshahara zaidi ya mmoja, nyumba za kupanga, na hisa katika publicly traded companies, na nyingi ya kampuni hizi zikiwa mstari wa mbele kuhujumu uchumi wetu?? Na je hivi kuna any transparency katika masuala ya ‘tax returns’ miongoni mwa wanasiasa wetu wafanyabiashara? Lakini swali muhimu zaidi hapa ni je, hatia kwa kiongozi nje ya kodi hakuna kweli? What about kujihusisha rushwa na matumizi mabaya ya madaraka? What about kubaka au kutafuta hongo za ngono? What about kuwa raia wa nchi zaidi ya moja kinyume cha sheria? The list goes on and on…


Wana CCM wenzangu, tusiogope kushindwa hoja kuhusu CCM kufilisika kihoja mbele ya umma, kwani badala ya kutibu tatizo, tunaficha ugonjwa ambao utakuja kutuadhiri. Tukubali kwamba nchi yetu imeshakomaa kuruhusu demokrasia ya kupokezana vijiti. Wana CCM wenzangu, kushindwa 2015 (kama itatokea) sio mwisho wa dunia, and as a matter of fact, tutakuwa kwenye nafasi bora zaidi ya kujipanga upya tukiwa nje kuliko tukiwa madarakani kwa sababu moja kubwa: Tukipoteza madaraka ya nchi, hapo ndio tutajua kina nani walikuwa wapo CCM kimaslahi na kina nani walikuwa wapo CCM kwa dhati kwani ni dhahiri kwamba wengi watakimbilia upinzani, na hii itawapatia nafasi wale wachache watakaobaki CCM kwani watakuwa na nia ya kweli ya kukirejesha Chama kwenye mstari.

Wana CCM wenzangu, CCM ni chama pekee katika dunia ya tatu kilichokaa madarakani kwa zaidi ya nusu karne, hasa katika mazingira ya liberal democracy. Sasa kama vipo vyama vinavyopoteza madaraka ya nchi kwa kutawala miaka mitano au kumi, sisi ni nani kuwa immune kiasi hicho? Unless madaraka kwetu ni kwa ajili ya kujipatia immunity na ufisadi ili tusifikishwe mbele ya sheria pale chama kingine kitakapochukua madaraka; au unless lengo letu ni kutumikia matumbo yetu na sio wananchi, vinginevyo watanzania wakiamua kututoa madarakani 2015, tukubali maamuzi ya wengi, lakini isiwe mwisho wa dunia kwetu kwani kwa mfano:


  • Ghana, kwa mfano Chama cha NDC kilipoteza madaraka mwaka 1992 kwa chama cha upinzani, lakini kikarudi madarakani mwaka 2008;
  • Uingereza, chama cha Labour kilikuwa cha upinzani kwa miaka 17 mpaka pale Tony Blair alipokirudisha madarakani;
  • Japan, chama Cha DP kilitawala kwa miaka 50, lakini kikashindwa miaka michache iliyopita, na hivi sasa kinajipanga na kina nafasi kubwa ya kurudi uchaguzi mkuu ujao;
  • Zambia, CCM ya Zambia (UNIP) ilitawala kwa miaka 27 na kuja kupoteza uchaguzi kwa Chadema ya Zambia (MMD), ambayo ilitawala kwa miaka 20 kabla ya kupoteza kwa chama kipya (DP) cha Satta ambacho tayari wananchi wengi wanaanza kufikiria tena kuwapa ridhaa yao MMD au UNIP. Hii ni ishara kwamba tatizo linalowakabili waafrika kwa ujumla ni umaskini lakini kuna uhaba wa vyama vyenye itikadi ya kutatua tatizo hili. Ndio maana huwa napingana na mawazo wa baadhi yetu humu kwamba hatuna haja ya vyama vingine vipya kwani CCM na Chadema wametosha.


Last but not least, niseme tu kwamba pamoja na haya yote, binafsi bado nina jina moja ambalo nina imani mtu huyo ana uwezo wa kulitumikia taifa hili vizuri (ngazi ya Urais) hata kama anatokana na wabunge wa sasa (CCM), kwa sababu amekuwa anapingana na the existing state of affairs (some of which nimezijadili) kwa muda mrefu. Lakini haina maana kwamba yeye ni bora kuliko wengine wa upinzani, na muda ukifika nitamtaja ili tumpime kwa hoja (sio kwa ushabiki, mazoea au maslahi).

Vinginevyo naunga mkono hoja ya Mwanakijiji kwa maelezo niliyotoa.
 
Back
Top Bottom