Lowassa: Kiongozi na wananchi wote wanalalamika

Lowassa: Kiongozi na wananchi wote wanalalamika

sasa braza hapa pana speech gani?

amejaribu kuelezea kuwa haina haja ya kuwa na vipaumbele lukuki kama zilizopo kwenye ahadi ya Rais ni muhimu kwa nchi yoyote kuwa na priority chache na ambazo zinatekelezeka pia ameonyesha jinsi gani waziri mkuu alivyofanya vibaya kwa kumwigilia mh.John pombe maguful katika kazi zake.
 
Duh mahaba hayo. Nn cha maana katika kauli hiyo? Mi nilifikiri EL kataja wanaomaliza tembo wetu au wale wanaoangamiza taifa kwa dawa za kulevya. Hakika tumechoka kufikiri.
 
watanzania bhana wanazubaishangwa kwa kitu kidogo tu leo watamuona wa maana kwani wamesahau kuwa huyu bwn alisha kuwa waziri mkuu kwanini hakuyafanyia kazi hayo anayoyasema amewahi kuwa waziri kwa mda mrefu tu.akili mkichwa watanzania 2015
 
Natamani uchanguzi uwe mwaka huu december tumkabidhi inchi ili tupunguze msongo wa mawazo.
 
Hayo ya Lowasa juu ya priorities chache alishaongea mbunge wa Kigoma kwa NCCR mageuzi Bwana Machali, Hamkuona kama ni hoja za msingi mpaka aongee Lowasa???
 
tatizo la watanzania hatupendi kufikiria hata kama jambo liko wazi, mfano ni nchi gani iliyoendelea inakiongozi mwizi madarakani anaendelea kula mema ya nchi, kwani lowasa ndiye kiongozi pekee, hatuwezi badilisha? Mungu wangu cjui tumelogwa na nani,
 
Hana mpango wwote si ndo huyu alipokuwa Waziri Mkuu akiwaibia wa Tanzania jasho lao kwa kujirundikia mimali nje ya nchi., maneno haya aliyotamka leo anajaribu kutaka kujisafisha ndivyo walivyo viongozi wa Tanzania wakiwa wameshiba hela.,
 
Huyo ndo raisi wako,baba yako na mtu atakayerejesha Tanzania tuitakayo,pia kaongelea kuhusu EAC badala ya kuvimbiana macho kumwandama Kagame kasema tusipoteze muda na haraka tuiwahi DRC. wimbo babababaa kiitikio: babaaa,baba huyo babaaa baba huyo......., hapo vipi?

kama kweli kaongea haya huyu jamaa anazidi kujipalilia.
 
Lowassa kawa mbunge na waziri miaka nenda rudi...je alifanya nini ambacho kwa hicho ndio ajitambishie kwa wenzake wa sasa??

Jibu ni kwamba HAKUNA, hayo aliyoongea bungeni ni porojo tu maana mtu yoyote anaweza akaongea hivyo kwa kuwa ni vitu dhahiri.

kuwa Serious Kaka.
 
Back
Top Bottom