Lowassa: Kiongozi na wananchi wote wanalalamika

Lowassa: Kiongozi na wananchi wote wanalalamika

watanzania bhana wanazubaishangwa kwa kitu kidogo tu leo watamuona wa maana kwani wamesahau kuwa huyu bwn alisha kuwa waziri mkuu kwanini hakuyafanyia kazi hayo anayoyasema amewahi kuwa waziri kwa mda mrefu tu.akili mkichwa watanzania 2015

Miaka mingapi hivi.
 
Huyo mwakyembe si ndio alimmwagia kitumbua mchanga?
Akamdhalilisha sana,akamfedhehesha sana hadi akang'atuka
 
Mzee wa maamuzi magumu

Mmmhhh, unanikumbusha siku Mheshimiwa Magufuli aliposema kuwa 'kuchukua maamuzi magumu tu haitoshi, kwani hata jambazi, jangili, mwizi au kibaka anapoamua kuanza shughuli ya kumwibia mtu (kuvamia nyumba, gari, nk) huwa amechukua maamuzi magumu. Cha muhimu ni kuchukua maamuzi yenye tija kwa umma!!!'
 
...Alisema
"Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa Jiwe kuu la pembeni!" na kumalizia na maneno haya " wewe ni mwamba, na juu ya mwamba huu nitalijenga taifa langu!"

Na kuwaondoa wasiwasi wale wanaodhani hili haliwezekani nawahakikishia "lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu linawezekana!"
Pasco
 
tatizo la watanzania hatupendi kufikiria hata kama jambo liko wazi, mfano ni nchi gani iliyoendelea inakiongozi mwizi madarakani anaendelea kula mema ya nchi, kwani lowasa ndiye kiongozi pekee, hatuwezi badilisha? Mungu wangu cjui tumelogwa na nani,

Tatizo Wapinzani hawajitambui,Kili siku wanafukuzana,wanagombana na hata kufikia hatua ya kutwangana na matofari je unadhani wananchi watatuchukulia serious si watatuona ni wahuni tu?Amini nawaambia upuuzi alioufanya Lema kule Arusha na kuungwa mkono na baadhi yenu msiojielewa kimeishushia hadhi sana Chadema na madhara ya upuuzi wa Lema mtakuja kuyaona huko mbeleni,subiri mtaniambia!!You had the chance to defeat CCM but all of the sudden you blowed it!!
 
Lowasa ni chapakazi na anafaa kuiongoza nchi hii kwani anazo sifa zote za kiongozi bora
 
Hivi ni kweli Lowasa amempongeza Mwakyembe? SIAMINI! kWELI? HAPANA! INAWEZEKANA?:shut-mouth:
 
Lowassa kama mmoja wa wachangiaji kaongelea mambo ya msingi,tuweke chuki,fitna pembeni,tusiwe watu wa kuropoka,ni kiongozi gani leo msafi anaweza kusimama na kumnyoshea lowassa kifole?
 
sasa mbona watu wamekuza as if hii ni point ambayo hakujawahi kuwepo kama hiyo before...wanaisema ni super...mi nimeielewa ila ni point ya kawaida kwangu...

amejaribu kuelezea kuwa haina haja ya kuwa na vipaumbele lukuki kama zilizopo kwenye ahadi ya Rais ni muhimu kwa nchi yoyote kuwa na priority chache na ambazo zinatekelezeka pia ameonyesha jinsi gani waziri mkuu alivyofanya vibaya kwa kumwigilia mh.John pombe maguful katika kazi zake.
 
na el ni mnafiki yeye ndie alisponsor sumu ya mwakyembe afu leo eti anamsifia shame on you lowassa
Huyo mwakyembe si ndio alimmwagia kitumbua mchanga?
Akamdhalilisha sana,akamfedhehesha sana hadi akang'atuka
 
sasa mbona watu wamekuza as if hii ni point ambayo hakujawahi kuwepo kama hiyo before...wanaisema ni super...mi nimeielewa ila ni point ya kawaida kwangu...

yaa inawezekana ni kawaida kwako kutokana na jinsi gani wewe ulivyoipokea
 
basi yawezekana hawa ccm tena team ya lowasa iq yao ni ya chini sana....sitaki hichi ndicho kitu super anachoweza kusema mtarajiwa mgombea nafasi ya urais ccm...ngoja nimsubiri na membe aseme super yake...na sitta pia..!!!! haha ha ha ha ha

yaa inawezekana ni kawaida kwako kutokana na jinsi gani wewe ulivyoipokea
 
Kwa mara adimu sana Edward Lowasa alichangia Hoja ya Mpango tarehe 4 Novemba 2013 lakini badala ya kujikita kwenye vipaumbele akaibuka na kipaumbele chake binafsi ambacho ni "ajira" kwa nia ya kuwadanganya vijana wamuone ni mkombozi wao. Ajira ni matokeo sio nyenzo hivyo vipaumbele vinabaki vilevile walivyochangia wabunge wengine kwa weledi wakati huyu anayetafuta kura kwa kuwadanganya wananchi ametuhidhirishia kuwa hana mawazo na uwezo wa kuwa Rais. Ajabu ni kuwa mamluki wake bado walifikiria ameongea la maana wakapiga makofi na kumsifu nje ya bunge. Mungu ainusuru nchi yetu!
 
Kwi kwi kwi kwi.... mleta uzi umefanya nicheke hadi nimepaliwa, ulivyokurupuka inaonesha kabisa umekimbizwa na bosi wako Membe!

Afu mwambie ule mpango wa kuwapeleka marais wa vyuo china siyo deal. hzo pesa bora atoe misaada ya madawati!
 
Lowasa ni "low hasa"; anashindwa kutenganisha vipaumbele na matokeo! Katika kipanga, "ajira" ni matokeo sio kitendea kazi. Vipaumbele ni vitendea kazi vya kuletea matokeo. Ajira hazishuki kutoka mbinhuni. Sikujuwa kuwa huyu ni kilaza msanii kiasi hiki.
 
Ujumbe huu ukufikie Mh. Rais wetu.
Watanzania tuna hamu kubwa ya kusikia utakacho kizungumza Bungeni Alhamisi hii. Katika hotuba zako nyingi hivi karibuni umekua ukilalamika sana bila kutoa tamko. Juzi juzi Ndg. Lowasa alinukuliwa akisema tumekua Taifa la walalamikaji kuanzia kiongozi wa juu hadi chini.

Mh. Rais; tunatarajia kwamba katika hotuba yako bungeni utakemea rushwa kwa nguvu, madawa ya kulevya, ujangili, mateso na mauaji ya raia, ukabila na udini ambao unatishia umoja wa taifa letu. Zungumzia hatma ya elimu ya Tanzania, ajira kwa vijana, kupanuka kwa pengo kati ya masikini na matajiri nchini. Toa msimamo kuhusu Afrika Mashariki na usalama wa mipaka yetu.

Don't complain again Sir; you are the President of Tanzania!
 
Back
Top Bottom