Lowassa: Kiongozi na wananchi wote wanalalamika

Lowassa: Kiongozi na wananchi wote wanalalamika

Mahaba ni upofu aisee.seriously,kabisa mtu kusema serikali iwe na vipaumbele vichache vya muhimu,kupongeza utendaji wa mawaziri napo ni "kuunguruma"!!! Au tayari zile "kambi" kuelekea 2015 zimeanza!!! Anyway,mleta thread ameshindwa kuficha mahaba yake kwa Ustaadhi Lowasa. Ntarudi... Waiter,please ongeza Kinana Lager nyingine bariiiiiiidi...
 
Je kaelezea richmond ni ya nani?.
Alishaielezea kuwa ni ya mkuu mwenyewe maana kila kitu walikuwa wanawasiliana naye. Si unakumbuka hata yule jamaa aliyekuja kudai kuwa ndiye mkurugenzi alifika mpaka ikulu akaonana na makamu na kumwachia salamu za mkuu wakati huo mkuu alikuwa majuu kama kawaida yake?
 
Edward Ngoyai Lowassa AKA Mwamba wa Kaskazini!
 
lowasa kwisha kazi , hana kipya tena, majuto ni mjukuu , alipewa nafasi akaichezea , amevuna alicholima , kumsifia Mwakyembe ni unafiki wa kiwango cha kutisha mno , maana tunajua kilichompata Mwakyembe baada ya Richmond , hadanganywi mtu hapa !
 
Namkubali sana huyu jamaa,
Ni jasiri sana anapambana kiume hana ile ya "umemwaga ugali mimi nimwage Mboga" kwa manma issue ya richmond ilivyokuwa naamini wangekuwa vioongozi wengine wangetajana hadi wakome lakini jasiri amepambana kufa kupona hadi mwisho na 2015 lazima ataingia white house.

Pamoja na Membe kutumia mbinu ya kuwarubuni baadhi ya marais wa vyuo vikuu kuwapeleka china ili warudi na kutengeneza mtandao wake wa kufanikisha adhima ya kukaa Ikulu kwa Lowassa atangoja sana!

Alipambana kiume kwa kutotaja waizi wenzake then unamsifia?? Ujambazi umehalalishwa Tanzania
 
Monday, November 4, 2013

Edward Lowassa.

Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka vipaumbele vingi visivyotekelezeka kwa wakati.

Alitaka serikali kuweka nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na miundombinu.

Aliwapongeza mawaziri John Magufuli kwa kuimarisha barabara na Dk. Harrison Mwakyembe kwa kubuni mbinu za kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, alizosema zinachangia kuharibu uchumi kwani watu wengi wanakaa barabarani badala ya kufanya kazi.

Na wewe uko kwenye payroll yake?
 
Monday, November 4, 2013Edward Lowassa.

Katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, ambaye huongea kwa nadra bungeni, Edward Lowassa leo amenguruma na kutaka taifa kuacha kuweka vipaumbele vingi visivyotekelezeka kwa wakati.

Alitaka serikali kuweka nguvu katika vipengele vichache vya msingi kama ajira, afya, elimu na miundombinu.

Hii tunaita "self promotion by window dressing".

Lowasa anasema serikali iweke nguvu katika vipengele vichache kama ajiria, afya, elimu na miundo mbinu. Atuambie ni vipengele vipi ambavyo kwa sasa serikali inatia nguvu lakini tunaweza kuviacha, maana alivyoviacha kutaja vya msingi ni kama ifuatavyo, kwenye red;

1. Ajira
2. Afya
3. Elimu
4. Miundombinu
5. Nishati (umeme)
6. Maji
7. Kilimo
8. Madini

Kwa hiyo, aseme wazi, serikali iache nini kwa sasa, michezo na utamaduni?

Pili, Lowasa aidha hana ufahamu wa uchumi au alikuwa anaongea ili watu wasikie sauti yake. Ajira si kipengele ambacho serikali inaweza kushughulikia "in isolation". Ajira ni matokeo ya serikali kushughulikia sekta nyingine. Kwa hiyo kama ana busara kama anavyotaka tufikirie atuambie ajira zitaongezwa kwa kushughulikia nini, sio kwamba serikali ishughulikie ajira. Huko ni kujipendekeza kwa watu wasio na ajira. Kwa mfano ukisema shughulikia miundo mbinu au nishati tayari unashughulikia ajira. Hivyo asitoe maneno ya kuremberemba hapa, watu tuna akili zetu za kutosha japo hatujawahi kuwa Mawaziri Wakuu kama yeye.
 
Na wewe uko kwenye payroll yake?

Kivipi? ninaweza kuingia kwenye PAYROLL yake ? wakati ninaishi NJE ya NCHI? NIPE BASI hizo CONNECTION niache kubeba MABOX huku? Winter inakuja sitaku kubabuka...
 
Jamani huyu lowasa c yule alikua waziri mkuu nn alifanya viingozi wetu waccm ban wakiondoka madarakani woooote ndo wako hv
 
Hii tunaita "self promotion by window dressing".

Lowasa anasema serikali iweke nguvu katika vipengele vichache kama ajiria, afya, elimu na miundo mbinu. Atuambie ni vipengele vipi ambavyo kwa sasa serikali inatia nguvu lakini tunaweza kuviacha, maana alivyoviacha kutaja vya msingi ni kama ifuatavyo, kwenye red;

1. Ajira
2. Afya
3. Elimu
4. Miundombinu
5. Nishati (umeme)
6. Maji
7. Kilimo
8. Madini

Kwa hiyo, aseme wazi, serikali iache nini kwa sasa, michezo na utamaduni?

Pili, Lowasa aidha hana ufahamu wa uchumi au alikuwa anaongea ili watu wasikie sauti yake. Ajira si kipengele ambacho serikali inaweza kushughulikia "in isolation". Ajira ni matokeo ya serikali kushughulikia sekta nyingine. Kwa hiyo kama ana busara kama anavyotaka tufikirie atuambie ajira zitaongezwa kwa kushughulikia nini, sio kwamba serikali ishughulikie ajira. Huko ni kujipendekeza kwa watu wasio na ajira. Kwa mfano ukisema shughulikia miundo mbinu au nishati tayari unashughulikia ajira. Hivyo asitoe maneno ya kuremberemba hapa, watu tuna akili zetu za kutosha japo hatujawahi kuwa Mawaziri Wakuu kama yeye.

Sijui kwanini haukutaja; Safari za NJE ya NCHI... YEYE LOWASSA kutembelea BALOZI na Rais TRIP zake kama Waziri wa Mambo ya NJE
 
Back
Top Bottom