Hivi huyu Lowassa ni genius kiasi gani? Hakuna mtu anayeweza kumzuia kufanya lolote nchi hii? Inawezekana kweli? Ni huyu huyu Masaburi wakati wabunge wa Dar wanamshambulia bungeni kuwa kauza UDA alisema wabunge wa Dar wanafikiri kwa kutumia Makalio. Leo hii nae Kaanza kufikiri kwa kutumia makalio?
Kila kitu lowassa, basi lowassa ndiye anayewateka albino!!!
Kwa hiyo kila ufisadi ni lowasa!!mnajiaibisha wenyewe tumieni vichwa kufikiri na si vinginevyo.
Akizungumza kwenye mdahalo uliondaliwa na kurushwa na AZAM TV jana, Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo, , Dr. Didas Masaburi(CCM), alisema anayepaswa kulaumiwa kwa uuzwaji holela wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) ni LOWASSA, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, kwani ndiye aliyekuwa msimamizi wa mchakato huo mwaka 2006 hadi 2008.
"Kwa mujibu wa sheria , Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa Serikali za Mitaa", alisema Dr. Didas Masaburi katika mdahalo uliohudhuriwa pia na wgombea wengine, Said Kubenea wa Chadema, Zangina Shangana(ACT-Wazalendo) na Renatus Muhabi(CCK).
Awali ilidhaniwa kuwa hoja ya uuzwaji wa UDA ungempa wakati mgumu Dr. Masaburi, lakini hali haikuwa hivyo kwani alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi ulioeleweka na kumtupia lawama Lowassa. Mbali na Richmond, Lowassa pia anatuhumiwa kuwa na hisa katika kampuni ya Integrated Property Limited inayohusishwa na ujenzi ambayo haikuiorodhesha kwenye Tume ya Maadili kwa mujibu wa sheria kama mtumishi wa Umma.
Mimi sijahusika na ufisadi katika uuzwaji wa UDA, nilichokifanya ni kupandisha bei yake kutoka bil.1 hadi sh.bil. 5.7nilipoingia kwenye UMEYA na kukuta shirika hilo limeuzwa isivyo halali.
Meya 2011niligundua mkataba usio sawa wa uuzwaji wa UDA baada ya kuajiri kampuni ya Ukaguzi wa hesabu ya KPMG, Bei yake haikulingana na thamani ya mali za shirika hilo, hivyo niliamuru mnunuzi, Simon group kuongeza fedha.
Soma zaidi RAIA TANZANIA.
View attachment 289852
Huyu mzee sasa anatia uvivu hata wa kudhani kuwa angegombea urais. Watanzania tuamke nchi inaenda kuuzwa hiii. Mtu anakuwa na kashfa lukuki za uuzwaji wa ranchi za ufugaji ng'ombe taifa, richmond na sasa UDA. Tuachaneni na huyu mtu jamani.
ukifuatilia kwa makini mazungumzo yote ya CCM ktk kipindi hiki cha kampeni utagundua kuwa kwa hakika ni wakati madhubuti wa kufanya mabadiliko ya UKWELI
ukimsikiliza MAGUFULI analalamika kwa dhati kuwa khali mbaya ya WATZ imesababishwa na uongozi dhaifu wa CCM
mf akiwa KAGERA analalama kuwa alikerwa na kuumizwa na ubinafsishaji kiholela wa ranchi 52 za Taifa na kuongeza hata rais KIKWETE naye alikerwa pia. JIULIZE ni muda gani umepita mpaka leo wananchi wameumia kiasi gani? rais anahuzunika na waziri wake anahuzunika nani wa kutoa maamuzi,
vinginevyo alipaswa atuambie kuwa wakati akiwa waziri alimshauri rais wawanyan"ganye wale waliobinafsishwa akakataa au akagwaya hivyo apewe rungu sasa ili atekeleze urejeshwaji huo vinginevyo na yeye ni DHAIFU, mdanganyifu muomba kura kwa hila.
akumbuke kuwa kama yeye anakerwa na uuzwaji wa ranchi 52 nasi pia tunakerwa na uuzwaji wa nyumba za serikali na hata rais KIKWETE alisema kuwa si vyema kuuza mali za serikali kiholela wakati alipoulizwa juu ya urejeshaji wa nyumba hizo alikerwa na maamuzi hayo ya uuzwaji lkn alibanwa na mfumo, hivyo mgombea wa CCM hawezi fanya mabadiliko ya kweli ni kiini macho tu. tusisite UKAWA kuna majibu ya mahitaji yetu.
Kila kitu lowassa, basi lowassa ndiye anayewateka albino!!!