Lowassa katika kashfa mpya! Ni ya uuzwaji kiholela wa UDA

Lowassa katika kashfa mpya! Ni ya uuzwaji kiholela wa UDA

ukifuatilia kwa makini mazungumzo yote ya CCM ktk kipindi hiki cha kampeni utagundua kuwa kwa hakika ni wakati madhubuti wa kufanya mabadiliko ya UKWELI
ukimsikiliza MAGUFULI analalamika kwa dhati kuwa khali mbaya ya WATZ imesababishwa na uongozi dhaifu wa CCM
mf akiwa KAGERA analalama kuwa alikerwa na kuumizwa na ubinafsishaji kiholela wa ranchi 52 za Taifa na kuongeza hata rais KIKWETE naye alikerwa pia. JIULIZE ni muda gani umepita mpaka leo wananchi wameumia kiasi gani? rais anahuzunika na waziri wake anahuzunika nani wa kutoa maamuzi,
vinginevyo alipaswa atuambie kuwa wakati akiwa waziri alimshauri rais wawanyan"ganye wale waliobinafsishwa akakataa au akagwaya hivyo apewe rungu sasa ili atekeleze urejeshwaji huo vinginevyo na yeye ni DHAIFU, mdanganyifu muomba kura kwa hila.
akumbuke kuwa kama yeye anakerwa na uuzwaji wa ranchi 52 nasi pia tunakerwa na uuzwaji wa nyumba za serikali na hata rais KIKWETE alisema kuwa si vyema kuuza mali za serikali kiholela wakati alipoulizwa juu ya urejeshaji wa nyumba hizo alikerwa na maamuzi hayo ya uuzwaji lkn alibanwa na mfumo, hivyo mgombea wa CCM hawezi fanya mabadiliko ya kweli ni kiini macho tu. tusisite UKAWA kuna majibu ya mahitaji yetu.
Hata EL ni CCM,ndio maana hapendi kuvaa sare za chadema..
 
Hili ni papa la mafisadi yeye kivuli wapo majangiri wenziwe lakini tumestuka
 
ukawa bado wana maumivu ya tafiti ya twaweza, wanaona wanaonewa.
 
Jaman tuna mchagua rais wa nchina wala siyo mcheza mieleka ikifika sehemu kigezo cha uongoz ni kupiga push up basi tumpe matumla urais ama cheka na cena angekuwa rais wa state
Obama na Putin mbona si mabondia? Jamani, mbona mnaumia sana?
 
Aisee huyu lowassa ni sheeda kila pahala yy yupo na anatupiga tuu...unamteteaje mtu kama huyu ambae ni mroho wa mali, madaraka na ni mwizi asie stahili kuishi au hata kuitwa mh katika namna yeyote ile
 
Eee Mungu tunaomba ukawa tuchukue nchi ili kila kitu kikawe wazi, huyu masaburi na wenzake watatueleza hiyo uda walimuuzia nani, yaani uongo mpaka hata mtoto wa darasa la 4 anajua ccm ni waongo, dah, lazima mtoke madarakani..!!
 
haa haa hiyo serikali iliyouza UDA ilikuwa ya chama gani? ndo maana tunasema ccm ipumzike...
 
haa haa hiyo serikali iliyouza UDA ilikuwa ya chama gani? ndo maana tunasema ccm ipumzike...

Mafisadi waliokuwa CCM kipanda chao ni cha moto sana wamekimbilia Chadema,angalia kampeni urais ya Chadema utaiona ile CCM ingine ambayo ndio mbaya zaidi.

Magufuli atawashughulikia wote hao kwenye mahakama ya mafisadi.
 
leo hii magenius wetu wanatuuzia DRT kuwa ni UDA ile ile ya zamani... kumbe washagawana wanakula tu sasa...
 
haa haa malori mangapi yalitumika?

Ni aibu kucheka kitu ambacho na wewe umeshaanza kua muumini nacho,CDM wao wako mbali zaidi kwenye makusanyo ya wana UKAWA mikutanoni,kwa sasa CCM hawafui dafu,CDM Wanatumia malori na mabasi kama wafanyavyo CCM,ila kupitia l'wasa na mapesa yake sasa CDM watu wanakatiwa mpaka tiketi za ndege kutoka kila kona ya tz ili kujaza shazi kwenye mikutano,Hio ndio CDM mpya,ni aibu kubwa bora mkae kimya kwani wananchi haya yanatokea kwenye mazingira yetu na tunaona
 
Sera za wagombea urais bukoba

1 lowasa-nitahakikisha wanabukoba wanapata soko la kahawa nje nchi kama Burundi na Rwanda

2.daktari mkemia
Magufuli-nitawahakikishia wanabukoba viwanda hapa hapa nchini ambapo watauuza kahawa zao kwa bei nzuri

Kichwa maji na lofa kati ya hao wawili n lowasa
Anawaza kuuza raw material nje
kuliko na kuwa na viwanda vya ndani
alafu eti anataka mabadiliko

Kibaya zaidi Rwanda na.Burundi wanalima
hiyo hiyo kahawa kama zao Lao kuu la kibiashara....
 
halafu kuna watu wapo humu kutwa kuchwa kumpigia kampeni huyo jamaa. ama kweli watanzania tunatafuta laana.
 
Watanzania wanahamishwa kwenye mjadala wa namna gani gas, dhahabu, Tanzanite, Nickel, Uranium, wanyama wasivyowanufaisha chini ya CCM ... wanajadili ujinga ujinga ... CCM lazima waambiwe kuwa hawatakiwi tena
 
Aisee huyu lowassa ni sheeda kila pahala yy yupo na anatupiga tuu...unamteteaje mtu kama huyu ambae ni mroho wa mali, madaraka na ni mwizi asie stahili kuishi au hata kuitwa mh katika namna yeyote ile

Hasira ni kwa ccm waliyemlea mwizi badala ya kumfunga jela
 
Back
Top Bottom