1. Mimi naona kuwa na kashfa kwa Tanzania ni kitu cha kawaida.
2. Nakumbuka Dr Slaa alivyoandamwa wakati ule alipokuwa mgombea urais.
3. Kwa hiyo, mimi hainipi shida sana maana kura yangu iko palepale ampapo nilishaamua iwe.
4. Tunachotaka ni kuwa na serikali yenye mfumo utakaowawezesha Watanzania kupata maendeleo.
5. Mfumo huo umeshindikana kwa muda wa miaka 50 na ulishindikana pia kwenye bunge maalum la katiba.
6. Waliochakachua maoni ya wananchi hawawezi leo kuja na kutudanganya kuwa wateleta maendeleo kwa mfumo gani?
7. Yale maoni ya tume ya warioba ndiyo yamebeba mfumo mpya - wa kupunguza madaraka ya rais, kuwawajibisha viongozi (mfano wabunge wasio'deliver') na ndio mfumo unaoufanya uadilifu, uwazi na uwajibikaji kuwa tunu za taifa.