Mkuu!! naomba nitofautiane nawe. Hivi ukisema takukuru unamaanisha nini? kama ni Taasisi ya kupambana na rushwa. You are very wrong!!Lowassa kweli sasa kaamua kurudi ulingoni, ndio maana;
- Katuma mtu wake kujiingiza JF, hii ikiwa ni post yake ya kwanza ili kutuletea hizi picha za kampeni yake.
- Baada ya mafanikio ya harusi ya bintiye aliyoweza kuhakikisha analambwa miguu na vibosile wote wa CCM, sasa inaelekea anaelekeza nguvu zake jimboni.
- Swali kwetu ni kuwa, ni vipi mtumishi wa serikalini anaweza kujilimbikizia mali na kufanya sherehe na kampeni za kifahari bila TAKUKURU kumchunguza?
Hakuna kiongozi ninayempenda,kuamini kama Lowasa,(sitoi sababu)
ni mchapa kazi kweli kweli
mawazo yangu tu
Watanzania tuna unyonge wa kupambana na viongozi wa abovu. Mtu akishakuwa kiongozi basi tunamwona kama vile ni Mungu. Tusbiri tuje tuone picha za Chenge, na za Rostam Aziz.
Hebu angalia wenzetu Marekani. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, kuna Maseneta na Makongressmen karibu kumi waliofungwa kwa miaka 7 na zaidi kwa ajili ya ufisadi- tena mdogo sana kulingana na uchumi wa nchi yao. Hebu tuambizane kama kweli kuna mbunge au Waziri yeyote aliyewahi kufungwa kwa ufisadi wowote hapa kwetu- tena ufisadi mkubwa unaolingana na nusu ya bejeti ya wizara nzima.
Kha nywele nyeupe pe kama Nyerere. Kifimbo cheusi ti kama cha Mwalimu. Kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa!