Lowassa is back!

Tumeshuhudia vyombo vya habari mbalimbali na hasa magazeti yakijitahidi kwa hali na mali kukumbusha yale mazuri aliyoyafanya(kumsafisha) mh. Lowasa kwa kuchambua enzi za uwaziri mkuu wake, ni kweli alifanya mazuri amabayo anasitahilli kupongezwa.

Ninachoshangaa sana ni kwanini wameamua kuyasema mema ya Lowasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu? Wakati wa anguko(kujiuzulu) mbona waliungana na Dr. Mwakyembe katika kumbomoa, huu ni nini kama si unafiki?

mimi binafsi najua ni mengi mazuri ambayo Mh Lowasa aliyafanya kwa nchi hii, kama wao walivyoeleza kwenye magazeti, lakini kwanini wasingeyaandika hayo wakati huo ili kupunguza kasi ya yeye kushambuliwa? Je, hii inamanisha kuwa hawa ni rafiki wa mheshimiwa wakati wa raha tu? na hawawezi kumtetea wakati wa mateso?

Waandishi hawa siwatofautishi kabisa na Mwanafunzi wa Yesu Kristo aliyekuwa mwelevu kuliko wenzake alieitwa Petro, huyu(Petro) aliahidi kumlinda Yesu hata kwa upanga, lakini tumesoma jinsi ambavyo alimkana Yesu wakati wa mateso.

Majuto ya Petro baada ya jogoo kuwika mara tatu ndo anakumbuka kosa lake.

Mimi nadhani haitoshi kumuandika mazuri yake pekee kwenye magazeti, ila ni vyema tujue mbinu iliyotumika na kusababisha nchi kuyumba baada ya Lowasa kujiuzulu.

Poleni kwa kujutia uamuzi wa kuchelewa kumuokoa Lowasa.
 
wewe mkuu ndio lowassa mwenyewe nini???
monduli2009 Junior Member
Join Date: Tue Dec 2009
Posts: 6
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
 
Back
Top Bottom