Lowassa is back!



Hii picha nzuri sana anadumisha mila.Kuna jamaa hapo kavaa koti la suti la dark blue anasindikiza kibuyu na dole sijui anaashiria nini

Anaashiria ushindi mkuuu!!!

Swala la kujiuliza hapo ni, kwakuwa watu hao wote kwa picha wanaonyesha kumkubali;

swali sasa Je kwanini ahonge tena kipindi cha uchaguziiiii???

 
Kweli Watanzania!!!Mmmh!

Ndio ni kweli mtu si hatia mpaka mahakama itaposema kuwa ni hatia LAKINI kwa nini basi tuendelee kuwakumbatia hawa watu wakati ushahidi umetolewa kuwa wamehusika kuhujumu uchumi wetu?

Kwa hiyo tusubiri miaka 15 ya kesi halafu mahakama ije isema ni kweli alikuwa na hatia,hapo kweli itakuwa jamii imetendewa haki??Watu kama hawa ni wabunge kwenye sehemu zao,wanahusishwa na wizi,kweli wameshindwa kuji-organise na wezi wengine basi wakawaletea maendeleo wananchi wao iwe kama kiini macho?

Maendeleo hakuna,bado tu wananchi wanafurahia na kuzunguka na mtu ambaye barabara za kwenda kwenye mashule,hospitali na kwenye huduma nyungine muhimu,hazipitiki?Kweli hapo mtu utasema umekuwa Mbunge kwa miaka zaidi ya kumi na tano??where is your track record?Angalia tu hiyo picha uone tofauti za hao watu na mazingira waliyopo.Halafu linganisha picha za marehemu E.M. Sokoine uone tofauti.Hapo kweli mtu mwingine akitutukana tunaweza kujitetea?

Ni nchi hii tu amabyo unaweza kuona upuuzi kama huu.

TUBADILIKE.
 
Kama Lowassa anajiamini kwa nini awe na Kifimbo hiki?
Hii picha wakati anatembelea huko kwao.
i1278_img0015.jpg
 
Hayo ni madoido tu ya kujifanya na yeye mchungaji akifika huko. Nadhani umasaini fimbo ni ishara ya uzalendo.
 
Mkuu!! naomba nitofautiane nawe. Hivi ukisema takukuru unamaanisha nini? kama ni Taasisi ya kupambana na rushwa. You are very wrong!!
ile ni Registered trust ya kuwalinda wala rushwa. na ndiyo maana iko ndani ya ikulu-mahali usipoweza kuingia kirahisi.

Mkuu Lumbe,
Unaongea jambo la maana, TAKUKURU yetu ya sasa ni ya kuwalinda wanene. Lakini bado tusiache kuiongelea kwenye mantiki yake halisi kama ingetumiwa ipasavyo.

Inashangaza kuwa hata wa-Pakistani wametushinda maana TAKUKURU yao moto wa kuotea mbali. Imemlima mpaka mkuu wao wa nchi.
 


Embu tazama anvyopenda ufahari, sasa ametembea kwenye vumbi kote mara tu carpet jipya. Alafu akishuka hapo anarudi kwenye hilo hilo vupi. au alikua anabebwa, if u ask that is a waste of shillingi kazaa kuridhisha ego ya Lowassa. Anapenda kujifanya babu kubwa sana huyu Molel na tofauti na sisi wengine uamini angalia tena



Hadi kofia hiwe ya pekee if your ask me tabia zake he is more of a cowboy than a masai, kitabia. Sijui kwanini hawa wamasai awamuoni kama ni fake huyu.
 
Tatizo ni kwamba hoja kali tunazotoa humu haziwafikii wananchi hivyo ana kila sababu ya kutamba apendavyo kwani robo tatu ya wabongo hawajui effects za mitandao
 
Kwani hicho kifimbo kina nini cha ziada mpaka kukifanya kiwe 'topic?'
fimbo kama hizo zipo! kwa taarifa yako zingine ni ala ya kuwekea kisu tembea uone...unawezakusema ni fimbo kumbe kabeba kisu huyo...

Note: fimbo na kisu ni asili ya mmasai...
 
Mnawaona watu waliemzunguka? Wanaupeo mkubwa wa kuelewa mstakabali wa uchumi na siasa za taifa?
Sasa kama hawana, kwanini walaumiwe kwa kumlaki Lowassa? Kumbuken kwamba mtaj wa mafisadi na CCM ni watu kama hawa wasioelewa mwenendo wa nchi. Hawa ndie mtaj wa uongozi huu.
 
Lowassa kavaa kofia kama la ki-Texas!

Oh boy! Once a Texan, always a Texan = Richmond Connection!
 
7238d1261467693-lowassa-is-back-img_0021.jpg


Mi-Asilimia 70 hiyoooo inapelekwa MACHINJIONI ya Ubongo.

Kikwete inawezekana ni dhaifu ila kwa hili, anaonekana anawaahamu sana Watz.

Lowassa, Kamua tu COWBOY wetu. Watu kama wewe huwa kazi saana kuwatoa.

Siku tukimuondoa Lowassa/CCM basi Tanzania itakuwa imepigania UHURU WAKE WA KWANZA.
 
Hana lolote hii ndio safari yake ya mwisho kisiasa...baada ya 2010 asipojiangalia mwenenndo wake kutoka sasa (yaani ataegemea upande gani?) atazama kwenye tope baya na gumu kutoka

wananchi wa monduli kama wananchi walio wengi ni maskini na hawawezi kuelewa uhusiano wa uwizi wake na umaskini wao..wao wanamuona kama successfully person..shame

Upinzani kwenye grassroot ni muhimu mno kuwaeleza wananchi uhusiano wa uwizi wake na umaskini wao..but wapinzani hawako ila maelezo dar
 
- Lowassa ni beneficiary wa kelele za wananchi zinazoendelea sasa hivi juu ya mapungufu ya Rais wa sasa, huyu ndiye hasa beneficiary wa lile Kongamano la Foundation majuzi na sitashangaa kama hakukuwa na mkono wake kule!

- Sasa politically, huu ndio wakati wake wa kuanza kujitokeza as the alternative, lakini kwa ujanja sana kama huu wa huko Ummasaini, ninatabiri one thing kwamba in the end Muungwana atakata deal, ambalo litamrudisha Lowassa kwenye cabinet level with condition ya kuachiwa urais 2015!

- I mean lets face it ni huyu Lowassa peke yake sasa hivi ndiye mwenye uwezo wa kuivunja CCM vipande viwili na hilo linamuogopesha sana Rais wa sasa kwa sababu anajua kuwa linawezekana na Lowassa analiweza, tena sana kwa sababu 2/3 ya uongozi wa CCM sasa hivi unam-support Lowassa, na wala sio siri ukifanyika uchaguzi wa haraka leo kati ya Muungwana na Lowassa nani awe Rais, Lowassa anamshinda tena hands down! Ninasema tena kwamba ukifanyika uchaguzi wa dharura leo Muungwana hawezi simama na Lowassa! and yes I said it!

- Ili kuendelea na Urais 2010, Muungwana anahitaji sana support ya Lowassa, tena bila hata ya wapiganaji, ndio maana kwenye uchaguzi wa UWT Muungwana ali-side na Lowassa kumfagilia Sophia Simba, pamoja na kwamba huko nyuma na mapema alishasema kwamba wagombea wote hawafai kwa sababu hawana afya nzuri! Kwenye ile NEC sio siri kwa wale wote waliokuwepo kwenye kile kikao kwamba Muungwana, alikuwa side ya Lowassa, against Sitta ni baada ya mabalozi wa nje hasa wafadhili kuingilia kati ndio akajifanya hayuko huko upande wa pili, lakini hakujua kwamba pamoja na kujaribu kujisafisha na ule mkutano wake wa kujibu simu, it was too late!

- Muungwana na Membe, peke yao hawawezi kuzima sauti za kina Butiku na Quaresi ni lazima nguvu ya Lowassa isaidie, ndio maana sasa unaona maajabu mengi yanatokea katika kuwajibu na kujaribu kunyamazisha sauti mbadala! No wonder Lowassa is so confident wala hayumbi au kubabaika, anapanga operation moja baada ya nyingine na zinafanikiwa, I mean look what happened to Nape, where was Muungwana to rescue him kama kweli anakijali chama kuliko kujikomba kwa Lowassa and the gang?

- Wa-Tanzania tufike mahali sasa tutafakari hali ya siasa ya taifa letu kwa kina na umakini, na it is simply a fact kwamba anayeweza kutukomboa sasa hivi ni Lowassa peke yake, sasa either tusuke au tunyoe maana hapa tuna-face mikuki miwili tena ya moto, upi ni afadhali? Ninasema hivi kWa sababu sio siri kwamba Lowassa is not going anywhere soon na hakuna wa kumuondoa! Na mimi ninashangazwa sana na confident aliyonayo yeye na wapambe wake, huwa ninajiuliza wanajua nini hasa kuhusu taifa letu I mean wana ujeuri flani ambao sio wa kawaida kwa sisi tunaowajua na kuongea nao kwa karibu,

- Wanajiamini nini hasa? I mean ni mawazo yangu tu madogo thinking aloud! Na I could be wrong pia!

Respect.


FMEs!
 
FMES,
No matter how powerful Lowassa maybe hawezi kutukomboa. Lowassa si mkombozi. Ni mafia anayetaka kuitumbukiza Tanzania nzima chini ya himaya ya umafia wake. Labda ungechagua neno jingine badala ya "kutukomboa." Ukombozi wa Mtanzania utakuwa ni kuachana na ufisadi. Lowassa hawezi. Ukombozi wa Mtanzania utakuwa ni kulinda mali zetu kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Lowassa hawezi.
 
FMES,
No matter how powerful Lowassa maybe hawezi kutukomboa. Lowassa si mkombozi. Ni mafia anayetaka kuitumbukiza Tanzania nzima chini ya himaya ya umafia wake. Labda ungechagua neno jingine badala ya "kutukomboa." Ukombozi wa Mtanzania utakuwa ni kuachana na ufisadi. Lowassa hawezi. Ukombozi wa Mtanzania utakuwa ni kulinda mali zetu kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Lowassa hawezi.

- Nilimaanisha kutukomboa kutoka mikononi mwa Muungwana!

FMEs!
 
He is back in full swing not only in his constituency but also at the national level as evidenced in the send off party for his daughter lasdt week.
 
Mhe Edward Lowasa akiwa katika mikutano ya kuhamasisha maendeleo katika Jimbo lake. Picha hizi ni harakati zake katika Kata ya Lolkisale tarehe 16/12/2009.

Huu ni mkutano uliotia fora wiki hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom