Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Ikulu siyo pango la mafisadi.
VOTE FOR UKAWA.

wala sio makazi ya mabepari ambao wadharau wakulima haliyauwa zaidi ya asilimia 75 ya watanzania ni wakulima, wakati watoto wetu wanakufa njaa wao wanakwenda kula bata ujerumani.
 
ImageUploadedByJamiiForums1432650608.032080.jpg
 
Nimesoma post nyingi sana hapa jf za kumkubali na kumkataa mh. Lowasa. Ila cha ajabu wanaomkataa lowasa hawasemi ni nani hasa anaweza kuchaguliwa ndani ya ccm mwenye uwezo wa kuchuana na upinzani. Inaonekana maji yamewakaa shingoni hawana la kusema. Sasa tuwe wawazi semeni sasa nani ni mbadala wa Lowasa. Kama hamna jengeni umoja mmsapoti kwenye mbio hiz za urais.
 
Ukweli ikiwa Edo ataupata uraisi itakuwa ni janga la kitaifa . Kwa nini

(1) Lazima hao marafiki zake waliomchangia watataka kurudisha hela zao na yeye pia atataka kurudisha fedha zake alizotumia kwani kila mtu anajua jinsi alivyomwaga fedha kununua kuungwa mkono. Wote tunajua hakuna atakayetoa hela yake bure bila kujua atazirudisha vipi kwani kama ungekuwa ni msaada basi hata hao watoa msaada wangeweza kunipa mimi nipeleke kanisani na msikitini lakini hawakufanya hvyo kwani walikuwa wanajua wanachokitafuta kupitia kwa Edo. Uraisi wake utakuwa wa kununua na si vinginevyo. Angalia tangazo la kwenye gazeti la Mwananchi la tarehe ya leo 26/5 ni tangazo la bei mbaya. Kizuri kinajiuza kibaya kinajitangaza.

(2) Uraisi wake utaongeza mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi na serikalini hasa kwenye vyombo vya usalama na kutakuwa na kulipiza visasi na kuhujumiana sana kuonyesha kila upande ulivyo na uwezo mdogo wa utendaji jambo litakaloongeza gharama za uendeshaji na matumizi mabaya wa taasisi za serikali

(3) Kutokana na mambo hayo mawili ufanisi wa serikali na vyombo vyake utakuwa mdogo sana hivyo uchumi utayumba, rushwa itaongezeka sana na itatuumiza, kutakuwa na Serikali ya kulazimishana na kutokana na hilo vyama vya upinzania vitapata nguvu sana (4) Kuongezeka kwa nguvu ya vyama vya upinzania kutafanya Serikali izidi kuwa ya kigandamizi kuua kabisa haki za msingi za kiraia. Hivyo fedha nyingi sana na nchi zitatumika kwa ajili ya kugandamiza haki za binadamu badala kulipia gharama za maendeleo.

Kitendo cha kusema eti kama angeendelea kuwa Waziri Mkuu hii nchi ingekuwa na maendeleo zaidi ni kitendo cha kuiponda Chama Chake na Serikali iliyoko madarakani ambayo ni kitu kibaya sana kwa mshikamano wa Chama na Serikali. Sidhani kitu hicho kitavumiliwa na Watanzania wenye nia njema na nchi hii.

Vile vile kule kusema kuwa eti walimvizia Mkurugenzi wa Kampuni ya Maji ili wamfukuze kabla hajaenda mahakamani kupata zuio la kimahakama inaonyesha kabisa akipata Urais atakuwa Rais wa namna gani. Kila mtu awe mtanzania au sio ana haki ya kupata haki yake kupitia mahakami na hairuhusiwi Serikali wala mtu yeyote kuzuia haki kwa sababu yeyote.

Ninaomba Watanzania watafakari hilo.


Supreme leader , kakupa ruhusa ya kuandika haya? Maana mlimwalika rasmi kwenye Kaupatu kenu .....
 
Ukawa hamtapata usingizi kwa kumuwaza Lowasa poleni sana
 
Elimu jimboni kwake imemshinda , ataiweza nchi Nzima?
Mamvi akipata urais basi wakulima waandike wameumia hasa wale wa kilosa ambao kila uchao wanaugomvi Na wafugaji !
Huwezi kuwa Na elimu bora kama huna uhakika wa chakula !

Siyo hivyo tu; kama kweli ana namna ya kutaka kuinua elimu si angeleta hata mswada wa sheria ambao labda ungeshughulikia matatizo yaliyoko kwenye elimu? hivi anajua ni kwa kiasi gani ufisadi umeharibu elimu yetu? au anafikiria ubora wa elimu utakuja kwa kunuia?
 
Nimesoma post nyingi sana hapa jf za kumkubali na kumkataa mh. Lowasa. Ila cha ajabu wanaomkataa lowasa hawasemi ni nani hasa anaweza kuchaguliwa ndani ya ccm mwenye uwezo wa kuchuana na upinzani. Inaonekana maji yamewakaa shingoni hawana la kusema. Sasa tuwe wawazi semeni sasa nani ni mbadala wa Lowasa. Kama hamna jengeni umoja mmsapoti kwenye mbio hiz za urais.

Nyie ndio wale mwenyekiti wenu jana aliwaita Makuwadi jana ?
 
Ndani ya ccm hakuna labda nje ya ccm.
VOTE FOR UKAWA
 
Nimesoma post nyingi sana hapa jf za kumkubali na kumkataa mh. Lowasa. Ila cha ajabu wanaomkataa lowasa hawasemi ni nani hasa anaweza kuchaguliwa ndani ya ccm mwenye uwezo wa kuchuana na upinzani. Inaonekana maji yamewakaa shingoni hawana la kusema. Sasa tuwe wawazi semeni sasa nani ni mbadala wa Lowasa. Kama hamna jengeni umoja mmsapoti kwenye mbio hiz za urais.


dondola hakumbatiwa hata siku moja
 
Mzee MM ninaunga mkono hoja yako. Kama kweli Watanganyika mlozi wetu angekuwa bado yu hai tungempigia magoti atuondolee ulozi wake na kwanza kabisa tutambue kuwa adui namba moja wa jamii yetu ni UFISADI na pili tumtafute kiongozi ambaye ana dhamira ya kweli ya kuutokomeza UFISADI. Serikali yetu inakusanya kodi kubwa na kama wangekuwa wabunifu wangekusanya zaidi. Lakini kukusanya kodi bila udhibiti wa UFISADI hakuwezi kuboresha elimu wala huduma za afya, wala miundombinu (majukumu makuu ya mkusanya kodi, yaani serikali). Hivyo Ndugu yetu huyu, mtunzi wa tamthlia ya 'maisha bora kwa kila mtanzania' na hii tamthlia iliyo jikoni ya 'safari ya matumaini kwa kila mtanzania', anaposema kuwa ajenda yake ni 'elimu kwanza' bila kugusia ufisadi, tunauona huo ni usanii ule ule. "Kilimo kwanza' kimekuwa 'kilimo mwisho' kwa sababu ya ufisadi huo huo (ref kwa nini wananchi huko mitaani wameyabatiza ma-VX 'kilimo kwanza'? Wananchi wanajua ila tu basi tu waoga wa kuchukua hatua za kujiwekea misingi ya maisha bora kama jamii - kuleta mabadiliko ya kiutawala). Ndiyo EL hafai.
 
CCM kumbukeni ikulu siyo pango la mafisadi .wala siyo ya wagonjwa.
VOTE FOR UKAWA
 
Binafsi nachukua form za upresidaaa mwaka huu, nina hakika mm ni bora mara elfu ya lowasa
 
Mwanakijiji mzee wa kanzi leo hii amegeuka mwanasiasa bila data; Unajulikana kuwa uko TIMU Membe, Unajulikana kuwa ww ni Vatican Mkereketwa, unajulikana kuwa Mzee Mwanakijiji anajaribu kupotosha ukweli ulio wazi kuwa Kilimo kwanza ililetwa na USA kupitia UN organs FAO, UNDP kwa maslahi ya Land Grabbers wa Dunia hii!!! Leo hii watanzania wanamiliki sehemu ndogo sana ya ardhi yao wakati makampuni makubwa ya kimarekani yakimiliki malaki ya hekari na mengine yanawakodishia wananchi!!!! Mzee Mwanakijiji anajua kuwa tatizo kubwa la nchi hii ni 1. EHM 2. EHM 3. EHM wanaolazimisha hata Gesi yetu ichukuliwe na wageni... MM anajua kuwa Richmond ni mradi wa Marekani, anajua kuwa Lowassa hakubaliani na ujinga wa kuwanufaisha wageni kwanza then wananchi wapewe makombo au kutumiwa kama vibarua!!! MM anadai kuwa hajui kuwa sasa hivi tunatazo la ajira lililosababishwa na watu wa Vatican kwa kiasi kikubwa ... Itoshe kusema Mzee Mwanakijiji na EHM wengine hamtaweza kumzuia Lowassa kuingia Ikulu this time ..
 
tunatata mabadiliko ya system sio mabadiliko ya mtu.
kwa miaka 53 tuko chini ya system ya wezi ambayo ni CCM,
hatuwezi kumchagua mwizi kutoka ktk system hiyo alafu tutegemee mabadiliko.
Tunahitaji mtu mwingine nje ya CCM ambayo ni system ya wezi.
 
lowasa anaweza akawa bora ndani ya ccm lakini sio bora nje ya ccm kamwe.
 
Back
Top Bottom