Lowassa atua Mwanza kusaka wadhamini, umati wampokea

Lowassa atua Mwanza kusaka wadhamini, umati wampokea

Kuweni makini watanzania, Italy walimwondoa bilionea wakamweka mtu mwenye maadili, Tazama wenzenu wanavyoendelea,japo walipata misukosuko kihistoria. Wengi wetu njaa,na wenzetu matajiri wanatumia mianya hiyo hiyo. Mliwapa mawazo yenu yawemo ndani ya katiba wakayaondoa. Waluchukia hasa kipengere cha mgombea binafsi(hapa wengi walichukia fungua macho hata Zito kanyamaza alikitaka,lowasa akikatwa jina angeingia nk.) Ndio maana kwa kuwa kimeondolewa wanatumia kila namna wateuliwe.
 
Mtu anae mtetea lowasa ni mrundi aende kwa Nkurunzinza hana uzalendo.


sipati jb kwa haya mambo mkuu.

je akipitishwa anavyotembea ataweza kukagua gwaride za wanajesh ninavyozionaga na atamaliza saa ngapi?

je akipitisha na mwaka huu kuna midaharo ataweza kujibu hoja au ni hasira nyingi posipo kujibu hoja,

je kwa anavyoonekana ataweza kuzunguka nchi nzima mjini na vijijini katika kipindi cha kampein maana ​niliona 2010 wenye afya zao nzuri walidata je yeye?
 
Lowasa ameshaanza kuwa na hofu anajua NEC hawawezi kumptisha kuwa mgombea uraisi kupitia ccm ndo maana ameanza kupaniki..
Kutafuta mgombea msafi ndani ya ccm ni sawa kutafuta mwanamke bikra kwenye wodi ya wazazi.

ccm ndo wanapaniki, safari hii hatutaki mgombea wa mfukoni na hatutaki mgombea wa kushikwa pua.
 
Huu uwongo kabisa .Dr.Mengi hawawezi kusapoti mchafu.
Nillikuwa naamini hivyo lakini kabadilika sana ...kiasi kuwa siamini..imani yangu ilikuwa kubwa sana kwa mzee huyu toka enzi ya kesi ya na Mzee Masilingi najisikia vibaya nikikumbuka nilivyomuona Mzee Masilingi kama ni Mkosaji kwa Mzee Huyu.Kweli hata kama ulikuwa Blackmail unapaswa kusimama na kusema hapana hili hstoria iandikwee.Kweli Dunia hii ya ajabu...na kisa changu cha mwisho ni Muhongo...japo nilisimama upande ule ule kwa kumuona mzawa lakni kwa hili na hawa jamaa nimefunga break...Its too much to swallow.
 
Umasikini wa watanzania hauwezi kuondolewa na malofa, ili uondoke lazima watu wawekeze kuuondoa nao ni lowasa pekee ndo mwenye huo uwezo.


mkuu siri ya kuondoa umasikini wa watanzania ni kumpata rais asiyeendekeza urafiki kazini,asiyependa rushwa na mchapa kazi, ambaye atawambia watanzania tufanye kazi na wao wakakubali maana na yeye atakuwa mchapakazi.
 
Yeye mwenyewe alishikwa pua kwenye sakata la RICHMOND angekuwa kweli MTU wa maamuzi magumu angesema ukweli ikajulikana,lakini akashikwa pua kama Mtoto kasusa akakaa pembeni,wapi maamuzi magumu laigwan?

Leo umepanick brother ikibidi kuwa pembeni utulie usiendelee kujidhalilisha
 
ripoti ya CAG bilioni 262 kwenye wizara ya ujenzi hazijukani zimeenda wapi ?Magufuli atuambie kwanza hizo pesa ziko wapi?

Pia atuambie atarudisha lini zile nyumba za serikali za pale Ubungo alizowagawia kimada wake aitwaye Sundi Malomo na mdogo wake (Magufuli) aitwaye Joseph!
 
CCM ilimtega vizuri sana Lowassa kwa makusudi au kwa bahati tu viongozi wao wengi sana wanaokutana na makada wa diaspora wamekuwa wakimtumia Karamagi kwa miaka mingi kama mfano wa mwanachama mmbovu yaani kama ulikuwa humjui shetani anafananaje kwa mujibu wa CCM basi Karamagi ndio shetani mwenyewe ata huyo Lowassa ajapondwa kama Karamagi over the years.

Sasa tena kitendo cha Lowassa kujitokeza hadharani na huyu bwana dhamira yake imewazidishia mashaka watu kuliko kuwaondolea wasiwasi watu wanaona kama kuna ni ill-motive kutokana na hii association. Kama kulikuwa na ambao walikuwa na doubts kuhusu shutuma zake huu urafiki wa Karamagi ndio umewathibitishia (imekuwa kama vile alichokuwa anasema Nape uthibitisho si tuliwaambia huyu bwana afai).

Kwa sasa watu wanaangalia nguvu ya hela maana mgombea wa CCM anachaguliwa na watu wachache hila product wise Lowassa to many is all what is wrong in a politician ata kama kweli anania yakuifanyia mema Tanzania safari hii historical facts do not support the future conduct.
 
Kwangu mimi naona LOWASSA hafai...
TIBAIJUKA, ROSTAM, KARAMAGI wote wapigaji tu.
Halafu kwa nini wote waliojeruhiwa awamu ya nne ndo wanaomuunga mkono EL? JE, WALIONEWA??
 
Naikiwa lowassa atakuwa rais chenge atakuwa mwanasheria mkuu wa serikali rostam waziri wa fedha na karamagi waziri mkuu.

Mungu aepushe mbali.
 
Wakuu wa mwanza nauliza hiviii, je mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza mh. Dialo alikuwepo kwenye mapojezi?
 
Mungu alisema dhambi zote zaweza kusamehewa isipokuwa kukufuru...maana yake nini?? Ni kusema kitu ambacho wewe mwenyewe unajua kuwa si sahihi na unawaaminisha watu kuwa sahihi
Unaona mungu anafanya kitu ww unakiita shetani
My take: huyu mwnye thread hii kuna azma maalumu anayotekeleza aidha kwa kutumwa so anachezea sehemu mbaya sana..awe makini...ni ushaur tu
 
Back
Top Bottom