Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,175
- 43,936
hahahaha.. Nitawapeni hiyo scenario:
a. Kikwete anaamua kutokugombea mwakani kwa sababu x,y. WanaCCM wanaanza kumpigia kelele sana kuwa awe mgombea "pekee" lakini anazipuuzia na kuamua kuwa hataki tena mzigo huu wa urais kwani umejaa lawama sana (kumbuka JK hapendi kubebeshwa lawama na miaka hii mitano imekuwa mitamu na michungu). JK alitaka kuwa Rais kutimiza ndoto ya kuwa Rais. Period. Ameshaitimiza ndoto hiyo na milele ameingia kwenye historia. Sasa agombee tena 2010 ili kiwe nini? So, tu assume JK hatogombea 2010.
b. Nani ataweza kugombea ndani ya CCM zaidi ya Lowassa? HAKUNA. Hapa ndipo utaelewa "Agenda 21" ni ni nini (2010) ambayo niliielezea mwaka jana ilipoundwa tu na sasa iko full throtle. Kuna imani ya wabunge na viongozi wengi sana kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kukiongoza Chama na Taifa kwa uwezo mkubwa, kufanya maamuzi magumu n.k kama Lowassa. Wapo ambao wanamdharau kabisa JK na kumuita the "so called president". Hawa wanaelewa udhaifu wa JK kuliko mtu mwingine yeyote (ule wa kiongozi, msiende mbali...).
c. Lowassa anafuata ushauri wangu to the core kama nilivyoandika. Wengi labda hamjakumbuka kuwa wiki iliyopita alikuwa Mwanza na Rais ambako alishangiliwa na pole pole mtaona akirudi kwenye sura ya taifa na kilele chake cha kurudi rasmi na moto ulimini itakuwa Bungeni wiki chache zijazo. Ushauri mmoja ambao hatoufuata ni wa kuachana na kina Mwang'onda, Rostam na wengine. Hii kwake ni timu ya ushindi.
d. Atakapofanikiwa kuwa Rais au kumsaidia mtu wake (always ana plan b) kushinda basi tarajieni kisasi.
Ukiweza copy hii na iweke mahali fulani usije ukaanza kuitafuta huko mbeleni.

Mimi, Edward Ngoyayi Lowassa, naapa kuwa:
Nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote, na kwamba nitaihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Nitatenda kazi zangu za Urais kwa uaminifu na kutimiza wajibu wa kazi hizo kwa bidii na moyo mkunjufu, na kwamba nitawatendea haki watu wote kwa mujibu wa Sheria, mila na desturi za Tanzania bila woga, upendeleo, huba wala chuki.
Nitatetea na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mungu nisaidie
Nchi inahitaji RAIS ambaye ni semi dikteta.
EL ni semi Dicteta. EL ameshakusanya mali. Inachobakia ni kuongoza nchi. Mimi nitampigia kampeni za nguvu 2015
Swali litakuwa ni kwanini Lowassa autake Urais wakati alishawahi kuwa Waziri Mkuu?
yale yale ya MALECELA na laana za NYERERE sembuse Lowasa! wala msiogope JF tuko pamoja tutamuangusha kirahisi sana tumuombee mema ili aonje nguvu ya umma ikoje naona anaamini sana nguvu ya pesa
Jeuri wanayo kwa sababu wanajua watanzania wakisha pewa pilau na kanga uwezo wa kufikiri unakuwa umefikia kiwango chake.
pili wanajua kabisa kuwa mbinu za ccm na vyombo vya dola hakuna mwananchi wala nguvu ya wananchi iliyo na ubavu wa kuvipangua.
wanajua kabisa kuwa vyama vya siasa a.ka. vya uinzani vyote ni vyama vyua ubinafsi hakuna siku wamewahii kuamua kutetea mwananchi bali wana tetea masilahi yao kama ilivyo kwa chama tawala, kama wangetetea masilahi ya wananchi hawakuwa na sababu ya kushindana katika jimbo moja vyama lukuki badala ya kusimamisha mgombea mmoja kulingana na mwelekeo au mwanendo wa uchanguzi.
Kwa hivyo jeuri ya chama tawala itaendelea na wana uwezo wa kumweka wanayemtaka kwa kuzingatia uwezo wa pesa za walala hoi/walipa kodi na za wafanyabiashara wakuu wanaolinda mali zao/mafisadi.
politically EL is over.....
EL hawezi kuwa rais wa TZ 2010 or 2015 ana roho mbaya na chuki na watu wengi sana...............................................ni bora kikwete awe rais kwa ajili ana ubinadamu kuliko EL. EL rais na RA chief of staff sijui watu kama wakina mengi sijui watapitia wapi.....
kamwe EL hawezi kuiongoza TZ
6.Kundi la Lowassa limefanikiwa kuwakamata wanasiasa machachari wa Upinzani na mmoja wao ambaye bado uchunguzi unaendelea kama anafanya kwa bahati mbaya ama ni kwa kutumwa ni mbunge mmoja kijana ambaye anataka iundwe tume ya majaji kwa ajili ya kujadili masuala ya Richmond .Hii imekuwa ni mbinu ambayo imetumiwa na mafisadi wengi duniani katika kujisafisha kwani mwisho wa siku ni kuwa mahakama itatakiwa kupata ushahidi usiokuwa na shaka , kitu ambacho hakiwezekani kwani mpaka sasa serikali imeshasema kuwa maafisa wake waliohusika kuandaa mikataba hiyo hawakusika na ufisadi wowote ule. hivyo tume ya majaji kwa sababu itategemea ushahidi kutoka serikalini na serikali ushahidi wake ndio huo majibu yanajulikana kuwa majaji watasema nini.
Mbona hatusemi paundwe tume ikachunguze meremeta, Tangold,Kiwira,Deepgreen n.k?
.
4.Wapo waandishi wa habari na wengine ni wahariri ambao mara nyingi walionekana kama ni watetezi wa Taifa lakini kwa sasa wanafanya jambo jingine , wengine wakiwa wanafikiri kuwa wanafanya kwa kushirikiana na ubalozi wa Iran kuandaa kijarida ambacho miongoni mwa wahariri wake ni dada Sakina Datoo na Hawra Shamte.
Wazo la Jopo la Majaji sio Bahati mbaya. Bali ni hatua ambayo itaweka kila kitu wazi - kwani majopo haya hufanya kazi kwa uwazi kabisa na wakati mwingine kurushwa 'live'. Huoni jopo la Majaji litatufanye tujue yale ambayo Dokta Mwakyembe alisema hawakuyasema?
Mhe. Zitto, japo siungi mkono mkakati wowote wa unaoitwa wa kumsafisha Lowasa ila naomba tusimame kwenye haki.Mbunge pekee ambae ametoa wazo la kuunda jopo la majaji ni mimi. Hii inatokana na imani yangu ya kupata haki na ukweli. Sina sababu yeyote ile kumtetea Lowasa. Sina interest yeyote ile na Lowasa. Ndio kwanza nasikia kwako kuwa Jopo la Majaji laweza kumsafisha Lowasa. Nimetoa mawazo haya kwa nia njema kabisa nikiamini kuwa Serikali imelikosea Bunge kwa kutototekeleza maazimio na kusafisha wakosaji. Nikadhani kwamba, iwapo mihimili miwili ya Dola inagongana, mhimili wa Mahakama ndio utaweza kutenda haki.
Kumbe hili laweza kumsafisha Lowasa? Kwamba inawezekana kabisa mtu mwenye akili timamu akahisi kuwa mimi ninaweza kutumika kumsafisha Lowasa? Hata kwa mikakati ya kisiasa ya badae ni kosa kubwa mimi kutaka Lowasa atakate.
Mimi ninadhani huu mzimu wa Lowasa huu usizibe fikra huru. Haiwezekani hata kidogo watu tuache kufikiri kwa kumwogopa Lowasa. Ifahamike kuwa Maamuzi ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond ni maamuzi bora kabisa kufanywa na Bunge na ni maamuzi ambayo yamelipa Bunge heshima kubwa sana. Siwezi kuwa mmoja wa watu ambao wanataka heshima ya Bunge kuporomoka. Wazo la Jopo la Majaji sio Bahati mbaya. Bali ni hatua ambayo itaweka kila kitu wazi - kwani majopo haya hufanya kazi kwa uwazi kabisa na wakati mwingine kurushwa 'live'. Huoni jopo la Majaji litatufanye tujue yale ambayo Dokta Mwakyembe alisema hawakuyasema?
Hata hivyo, kama tunaamini kuwa jopo la majaji litamsafisha Lowasa, basi tusiunde! Nilidhani jopo la majaji ndio limwadhibu Lowasa na wengineo waliopanga kutuibia kupitia Mkataba wa Richmond.