Kwa mtizamo wangu (ambao unaweza kuwa finyu) jitihada za Lowassa kujirejesha ni jambo ambalo linafahamika kwa wengi wanaofuatilia nyendo za mwanasiasa huyo.Kuna scenario mbili,zote ni hypothetical,however:
1st.Lowassa anagundua kuwa 2015 ni mbali sana,na political landscape ya Bongo inaweza kuwa imebadilika muda huo,hivyo kukwamisha aspirations zake za kuwa the 5th president of Tanzania.Anaamua liwalo na liwe,anatumia influence yake ndani ya CCM na serikalini (inadaiwa JK trusted EL with the task of kuwachagua na kuwapanga watendaji wa serikali katika ngazi ya mikoa na wilaya) na nguvu yake ya fedha akisaidiwa na mafisadi kama Rostam Aziz,pamoja na vyombo vyake vya habari (inadaiwa amenunua FM Station moja huko Arusha anayodhamiria iwe ikisikika nchi nzima) ku-challenge utaratibu wa CCM kwamba the incumbent (JK,in this case) should stand unopposed in 2010.Unless JK atakuwa amegundua kuwa uraisi umemshinda,atapambana vikali sana kuhakikisha kuwa anamalizia miaka yake mitano iliyobaki.Direct confrontation kati ya JK na EL ni lazima immalize mmoja wao kisiasa,and I assume JK would emerge a winner and EL a permanent loser.
2nd.EL anatengeneza mazingira kwa nguvu zote kuhakikisha anakuwa mrithi wa JK mwaka 2015.Jina lake kupitishwa is not an issue,kwa CCM hata Rostam akiamua kugombea 2015 jina lake linaweza kupitishwa.Chama mufilisi hakina muda wa kuangalia kama mtu anafaa au la.Atakumbana na akina Membe,Mwinyi Jr,Mwandosya na aspirants wengine kadhaa wanaotajwatajwa.Tatizo hapa liko Zanzibar.I cant imagine Wazenji kukubali mika zaidi ya 20 ya rais kutoka bara.Mtandao wa JK ulifanya kazi ya ziada kupoza opposition kuhusu kukiukwa kwa "utaratibu" wa "awamu hii rais anatoka bara awamu ijayo rais anatoka zenji".Lakini kwa namna huyu jamaa anavyotaka kuandika historia yake (kwamba lazima siku moja awe rais wa TZ) kelele kutoka Zenji zitapuuzwa,hence signifying the official dissolution of the Union.
All in all,huyu mtu anapaswa kudhibitiwa kwa nguvu zote asipate urais kwani katika muda mfupi alokuwa PM ametuthibitishia ni namna gani alivyo hatari kwa ustawi wa taifa letu.Nothing personal but the guy is a fraud.