Kwani kumtetea kuna kosa gani hasa ikiwa una uhakika kaonewa? Unataka ajisemee mwenyewe kwani hujui jinsi ushahidi wa second person ulivyo na nguvu kuliko wake mwenyewe?
Niliwahi kuandika na sasa naandika tena iko siku wote mtaona aibu mtakapojua kilichotokea!!!
kwa nini unaweka assumption?kwa nini asirudi kwao?subiri utaonaIwapo yaliyojiri kwenye majengo ya Bunge yata transpire kuwa kweli, Je, Mh. Chenge atarudi kwao tena safari hii na kulakiwa kwa vigelegele na WanaBariadi?!
Hollo, je kweli unaona yote yanayosemwa si ya kweli?! In a way I can understand, maana jamaa kashavumishwa kaaga dunia tayari...na ikatokea sivyo hivyo!! May be, and may be you know everything going around in these two days ni uzandiki mtupu... but again, as always, time will tell.kwa nini unaweka assumption?kwa nini asirudi kwao?subiri utaona
Lowassa, Karamage, Rostam na usanii wa Kifisadi,
Tumeambiwa kwamba katika kikao cha CCM kilichokaa jana (15/06/2008) Dodoma, Bw. Lowassa alijitete kwamba; alitaka kuufuta mkataba wa Richmond mara mbili akakataliwa!! Haya ni madai ya kinafiki kabisa ya hadithi ya Sungura na Zabibu; Mbichi hizi..... Ukweli ni kwamba: Bwana Lowassa alijaribu kuusitisha mkataba wa Richmond baada ya kuona kwamba mbinu zao (Lowassa na Rostam) za kutuibia hazitafanikiwa kupitia kampuni hiyo (Richmond) baada ya Mabenki mawili City Bank na HSBC kukataa kupokea CL kwa niaba ya matapeli wa Richmond,
Kwa mara ya kwanza City Bank walipokataa kupokea LC ya Richmond ndipo Lowassa alipotoa wazo la kufuta mkataba, Tamaa ya Kifisi ya Bw. Rostam ndiyo iliyomshawishi akaipa muda Richmond kujaribu kupitisha LC katika Bank HSBC. Bank ambayo pia lipokataliwa! Ndipo kwa mara ya pili Bw. Lowassa akata mkataba Ufutwe.
Ikumpukwe kwamba njia ya kukamilisha wizi wao (Lowassa na Rostam) wa kifisadi ilikuwa mpaka pesa zitoke ( LC ipokelewe)
Baada ya jitihada zote kushindwa kupitia Richmond ndipo Lowassa, Karamage na Rostam waliposafiri kwenda Calgary Canada nakufanya mbinu za kufaulisha makataba kutoka Richmond kwenda Dowans;
Mwenyekiti Tanesco (Balozi Kazaura) alipokea simu kutoka kwa Bw Karamage iliyomuarifu kwamba Richmond wanataka kuuza mkataba kwa Dowans. Ikumpugwe kwamba simu hii aliipiga Bw Karamage akiwa Calgary Canada katika ziara pamoja na Bw. Lowassa na Rostam na hii ni coincident?? La hasha huo ulikuwa ni U-MAFIA wa genge la kifisadi.
Ndugu zangu hawa ni wezi - wauwaji wa Kifisadi Ni Watanzania wagapi wanakufa kwa kukosa dawa ama huduma za kawaida kabisa za kijamii huduma ambazo zingeweza kulipiwa na zaidi ya Million 150 kwa siku Mafisadi hawa wanazotuibia? Tusikubali au kudhani kwamba CCM yaweza kuwadhibu wakati mising ya CCM kuingia katika madaraka ni Ufisadi, wamefika hata kusema kwamba walikuwa washindwe Kiteto kama sio pesa za EPA toka kwafisadi Rostam zilizokodisha Helicopta, sasa vipi Nyani atakuwa hakimu katika kesi dhidi ya Tumbiri na mlalamikaji akadhani atapata haki?
Dawa yao ni kuwazomea wakati wote tukisubiri kuwaonyesha ukweli wetu 2010.
Kazi kwenu.
Kiganja
Nashukuru sana Kiganja kwa kutuupdate na hizi news
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, ametetewa na wajumbe wengi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).
Habari za ndani ya kikao hicho kilichojadili juzi pamoja na mambo mengine uhusika wa Bw. Lowassa katika sakata la mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Richmond, zilisema baada ya Bw. Lowassa kujieleza wajumbe waliuona ukweli na kubaini kuwa uhusika na Richmond si wa moja kwa moja.
"Sisi tunaamini kuna vikundi ndani ya CCM ndivyo vinavyoshinikiza hali hii itokee ili Bw. Lowassa aonekane mbaya mbele ya jamii, lakini tulifikia muafaka kuwa alijiuzulu si kwa kuhusika moja kwa moja na Richmond, bali aliwajibika ili kukiokoa chama kwa wadhifa wake," kilisema chanzo chetu cha habari.
Chanzo hicho kilisema kilichojitokeza ni kuwa Bw. Lowassa alionewa katika sakata hilo na kwamba la muhimu ilikuwa ni kuwasilisha ushahidi muhimu, kama upo, katika kujihusisha moja kwa moja na Richmond.
"Hata Mwenyekiti wa Kamati teule ya Bunge, Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa anahitimisha hoja yake, alisema Kamati haikubaini kuwa Bw. Lowassa alihusika moja kwa moja mbali ya kuwajibika kama Waziri Mkuu," kilisema chanzo hicho ndani ya NEC.
Mmoja wa wanachama wakongwe na kada wa siku nyingi wa CCM ambaye pia ni mjumbe wa kikao hicho, alisema maelezo yaliyotolewa na Bw. Lowassa katika NEC juzi, yalitosha kumwondoa katika kashfa ya moja kwa moja ya Richmond.
Habari zaidi zilisema wajumbe hao wa NEC walikubaliana kutoendeleza hoja hiyo na kutaka Serikali iachiwe majukumu yake na badala yake CCM ijiimarishe na iendelee kutekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa maslahi ya wananchi.
Kauli ya wajumbe hawa ambao hawakutaka kutajwa majina yao gazetini kutokana na sababu za kisiasa, zilikuja kutokana na mgawanyiko ambao awali ulishajitokeza ndani ya NEC.
Mgawanyiko huo ulitokana na baadhi yao kutaka waliotuhumiwa kwa ufisadi wachukuliwe hatua za kichama ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya chama; lakini kutokana na mjadala mkali, ikabainika kuwa papara zinaweza kukiathiri chama hicho na kusababisha mgawanyiko mkubwa.