Lowassa anasafishwa!

Binafsi sipingi kwamba Lowassa alikuwa mchakalikaji mzuri (alipotaka kufanya kazi).Some may even say he was Kikwete's "policy wonk" whom such mediocre figures like Sumaye and Pinda may never dream to rank as.Some may even reason that the arrogance borne out of the knowledge of his "wonkness" contributed a lot to his demise, he saw himself above reproach and indispensable to an intellectual weakling of a president.

Wala, unlike many members here, sipingi kwamba Lowassa kwa kutopewa fursa ya kujitetea hakufanyiwa haki (I recall FMES called it "the rule of politics" as opposed to "the rule of law")

Ila naona muandishi kwa kujifanya hajui bin maamuma wa cardinal rules za uandishi/ sheria, mojawapo ikiwa suala zima la paradox ya anonimity na credibility.Katika uandishi wa habari / ripoti za aina hii, the more anonymous your source is the better chance of getting more information and even quality information, even rising to the level of classified information.People simply do not want to risk exposure and easily muddy their career waters to say nothing of creating enemies.So a certain level of anonimity is allowed in journalism to protect the identity of the whistleblower.

The problem with anonimity is credibility, or to be precise lack thereof.An anonymous source commands less credibility than a named one.And perhaps as our esteemed brother pointed out, the report was as much accomplishing "the rule of politics" as it was "the rule of law"

The bottom line, at least in principle if the practicality of the matter was deemed implausible, is that Lowassa could have seized his moment in parliament and brandished a resolute, fact based (if he was really in a position to do so) counter attack aimed at self exoneration.

He did not do that, either because it did not matter to him or because he had no ammunition (facts) to fire back.

So who are you to speak for he who could not speak for himself?
 
Ifahamike wazi kuwa simtetei Lowassa

Hapo Mwanakijiji umenichanganya kidogo,maana heading inasema "mtetezi mpya wa Lowassa" at the same time unasema humtetei.

Kwa maoni yangu naona Lowassa mwenyewe alijua kuwa hakuna cha kufanya and that his only defence was to say kuwa hakutendewa haki.Lets say, for example,ile report ya Hosea,kuwa Richmond ni safi ingekuwa ndio mwisho wa haya yote.Maswali mangapi yangekuwa yameachwa bila kujibiwa? Na tukumbuke madhumuni ya ile report ya Hosea ndio ilikuwa kum-exonerate Lowassa.JK was right kusema kuwa Lowassa kakutwa na ajali ya kisiasa,kwa sababu yeye as PM alikuwa ana muda mrefu sana wa kulirekebisha hili swala,lakini yeye aliamua kutumia shortcut ya PCCB.Sasa limemtokea puani,issue inageuka na kuwa tena hakupewa muda wa kujitetea.Mpaka leo hii hajatokea hata mmoja wao ku proove kuwa hawahusiki na Richmond,zaidi ya kusema kijuujuu tu.Kama alivyosema Pundit,alipata muda bungeni baada ya report kusomwa,lakini yeye akaamua kujibu mashambulizi kama vile yeye ni amateur kwenye haya mambo.Msabaha alifanya vizuri kuliko hata yeye.

Thats my take...
 
achaneni naye huyo mmeru,

yeye si aliamua kuzira kwa vile "watu" walikuwa wanautaka uwaziri mkuu?Ina maana bila Lowassa tanzania haiwezi kwenda mbele?Mbona huyo "mwandishi maalum" hataki kuonesha mapungufu ya huyo Lowassa?Kwa hiyo anataka kutuaminisha kuwa Lowassa was, and still is, a saint?
 
Nakubaliana na watu wote wanaosema EL was a right man for kikwete, serikali atleast ilikuwa active sio kama sasa imeibiwa, hiko kama haiko lakini tunaingia kwenye maadili hatuwezi kumuacha EL madarakani hata kama amefanya madudu ya makusudi kuliibia Taifa kwa kuwa alikuwa right man kwa kikwete.

Unless EL na RA waje mbele ya watu na kuwaeleza wananchofaamu kwenye RD ndo tutaacha kutuhumu kama mafisadi, watueleze ukweli badala ya kusimamia ibara ya 15:1 ya katiba ya CCM. Watangulize masirahi ya taifa na kutumbia RD ilikuwa ya nani na Dowarns ni ya nani, hicho ndo wananchi wanataka kupata na sio kutetewa kwa maneno yasikuwa na maana.
 
Mh!

Huyu mwandishi wa hii makala anadai hamtetei EL wakati amefanya hivyo kwa nguvu kabisa! Kukumbusha aliyofanya kama sehemu ya WAJIBU wake hakufanyi hiyo kuwa utetezi wa kilichotokea!

maadamu hii makali imetoka kwen gazeti la Rai, tunaelewa nini maana yake....
 
Nimeipenda hii mada kwa sababu kuu mbili

  1. Imekuja na hoja, leaving room for discussion

  • Inatazama pande zote mbili na sio ushabiki tu! Imefikia stage ata wale safi wanaitwa mafisadi..utabaki nani?
 
Nimeipenda hii mada kwa sababu kuu mbili

  1. Imekuja na hoja, leaving room for discussion

  • Inatazama pande zote mbili na sio ushabiki tu! Imefikia stage ata wale safi wanaitwa mafisadi..utabaki nani?

Mapambano,

Ni kweli hii hoja ina room of discussion lakini zidhani kama kweli inatazama pande zote mbili za shilingi. Kwa mtizamo wangu imeletwa kwa ajili ya kumuokoa EL kisiasa. Kama kweli EL ni kibangusilo mbona alikuwa na nafasi ya kujieleza bungeni ambako media yote ilikuwa imeelekzwa lakini hakufanya hivyo zaidi ya kudai kuwa kuna watu wanakitaka cheo cha uwaziri mkuu. Kwa upande wangu bungeni jamaa alikuwa nafasi lakini hakuitumia badala yake akaenda kusemea kijijini (jimboni ) kwao amboko amezoea kuwadanganya ili wampe kura na ambako yeye ni mfalme!!!
 
Tangu nianze kupitia hii JF nimekuwa nikiridhishwa na arguments na analysis zako, lakini kwa hili la EL, kwa kweli nashindwa kukubaliana moja kwa moja.
1. Mtu kufanya mengi mazuri hakuondoi haki ya kukosolewa pale unapokosea. Ukosolewaji wako utaendana na ukubwa wa dhara ulilotenda. Hivyo EL pamoja na hayo mazuri mengi aliyofanya bado haitosha kuoverlook upotofu na uharibifu alioufanya. Issue ya umeme sidhani kama ni jambo dogo kwa watanzania na uchumi wao na maendeleo yao.

2. EL kwa nafasi yake kama mtanzania tu wa kawaida alikuwa na haki ya kushiriki zoezi la kutoa taarifa kama alikuwa nazo ili kusaidia uchunguzi uliokuwa unafanyika. Lakini kama waziri mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali, na hasa kwa kuzingatia kumbe ni swala alilowahi kulishughulikia, alikuwa na wajibu wa kufika mbele ya kamati na kueleza alichokijua na alichokifanya. Ni mara ngapi tumeona polisi wakifanya upelelezi kwa kuomba mwenye taarifa aende polisi kutoa? Ni mara ngapi upelelezi wa polisi umesaidiwa na raia wema ambao walijitolea kwenda mbele na kusema walilojua au kuona. EL alitakiwa afanye HILO tu na si zaidi kwa nafasi mbili alizokuwa nazo. Kama raia wa kawaida wa Tanzania na kama waziri mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali.

3. Kama kweli EL alikuwa na maelezo basi alikuwa hana budi kuyatoa kwa watanzania wote na sio tu kwa watu wa jimbo lake la uchaguzi. Ni sababu ipi kabla Mhe. Spika hajawaonya kuhusu kusema sema kwao kulikomfanya akaona watu wa Monduli ndio waliokuwa wameathirika zaidi na kujiuzulu kwake na sio watanzania wote waliostahili maelezo, kwani swala la umeme lilikuwa haliigusi Monduli peke yake. Je, ni sahihi mtu akifikiria kwamba aliwasize up watu wa Monduli na akaona watamsikiliza bila maswali na sisi wengine huenda tungeuliza au kutaka maelezo zaidi.

4. Kwa kiasi fulani nakubaliana na hofu yako "Kwa utamaduni wa kumalizani tunaelekea wapi?" Hilo ni swali zuri na nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu kwani binadamu sote tuna mapungufu na hasa unapokuwa kiongozi iwe kwenye level ya familia, jamii au taifa. Ninachoamini ni kwamba familia, jamii au taifa hutoa hukumu kwa misingi fulani ambayo inakuwa inakubalika kwa uwiano mkubwa. Ndio maana kwenye jamii kuna makosa makubwa na makosa madogo. Vivyo hivyo EL amehukumiwa. Kosa alilofanya ni kubwa na limeathiri wengi na kwa kiasi kikubwa. Mbona alivyosaidia kushinikiza yule mtuhumiwa Nyari atoke jela watu hawakulalamika. Ni kwa vile liliwagusa wachache. Huenda ni wale tu waliokuwa kwenye sekta ya madini ndio waliojua athari ya msaada ule lakini wengine hatukujua au hatuathirika.

Ni mambo mengi yanafanyika ambayo si sahihi, ni mengi Mwl. Nyerere alikosea wakati wa uogozi wake, lakini hakuhukumiwa kwa ubaya kama EL. Ni nini umekosea na ni namna gani unajieleza au unajiweka ndiko saa zingine kunapelekea hukumu mbaya. EL alijiweka mahali pa (i) hakuna wa kumgusa (ii) kujipa uhalali (Sense of entitlement) ambako kulimfanya ashangae pale alipoulizwa kwani hajazoea au anaona hastahili kuulizwa na ndio maana akazira. Hiyo ni hali mbaya kweli unapokuwa kiongozi. Kiogozi ni lazima unyeyekea waliokuweka pale. Huu si ufalme, na huo nao siku hizi watu wanauliza ukifanya ujinga ujinga iwe sembuse uwaziri mkuu waliogawaiana kama njugu, ubunge ambao wengi wamepata kwa kununua?

Kufanya kwako mazuri hakukuepushi na dhahama ya kusulubiwa ukikosea. Ni kosa gani na ni adhabu ipi unastahili ndio issue itakayojadiliwa. Utendaji wako mzuri unaweza ukawa a good mitigating factor, but until we have turned everything upside down and have all the facts correct and proved ndipo hilo linaweza kuapply.
 
Let me put it very clear... mimi siyo mwandishi wa makala hiyo, nimeikopi toka Rai ya juzi! Sorry for the confusion.
 

What makes you think so? EL might have been the right man for Kikwete but not for this Tanzanians!

Mwanakijiji > who's mwandishi maalum - Rai?? this person could be even EL himself trying to clean up the mess! I just don't know what's wrong with us Tanzanians....we hear something and believe it with all our heart but the moment we hear something else we dont even reason we change our minds! Hivi haya tunayoandika kila kukicha ya kuwatetea watu ambao hata wenyewe hawawezi kujitetea ndio UZALENDO???

Haikuwa Lazima EL kuhojiwa na Kamati teule provided they had all the hard evidence they needed. Hata huyu EL mwenyewe analielewa hilo na ndio maana aliuchuna kimya akisubiri kuitwa mbele ya kamati teule....why couldn't he just walk over maana alisema ofisi za bunge ziko karibu sana na ofisi yake! Kamati ilikuwa open for anyone who could talk to them.....

Watetezi wa EL watakuja wengi tu lakini they wont make any substantial change unless huyo EL, na Muasia wake RA waje mbele na kuongelea kile wanachokijua kuhusiana na hili la Richmond/Dowans na hata mengine mengi waliowahi kufanya.

Huu utetezi hautoshi......
 

Kuna mkakati wa magazeti ya mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata - Rostam Azizi wa kumsafisha Lowasa na kuwachafua wapinzani wake. Katika hili usishangae kuwa Lowasa na Rostam walipitia final draft kabla haijawekwa hapo kwenye gazeti la udaku la rai.
 
Jamani Nimeshasema Na Ni Mawazo Ya Wengi....sijui Mtakuja Na Mpya Gani Kumpa Tena Nafasi Kugombea Chochote..........katika Nchi Hiii...akae Kimya Aachane Na Nchi Yetuuu
 
Tatizo hasa ni njaa za waandishi ndizo zinawafanya kuwa wanafiki kwani hapo hawazungumzii nafsi zao bali matumbi yao.
 
Hata tusiposikiliza kile mwl. nyerere alisema juu ya lowassa, kiongozi gani asiyeweza hata kujitetea mwenyewe!! lakin angalia mtiririko huu wa matukio:

1.wakati mkataba tata wa buzwagi unasainiwa hotelin uk, lowasa alipitia uk akitokea paris.

2.Anahusishwa na richmond, alishindwa kuvunja mkataba kama alivyofanya kwa city water.

3.Alisafiri kwenda thailand kwa rafiki yake shinawatra eti kutafuta mvua ya kutengeneza, miezi michache baadaye rafiki yake anabainika kuwa mwizi na kuondolewa madarakani.

NI KWA NINI LOWASA KILA PALIPO NA DOSARI YEYE YUPO??? AU YUKO KARIBU NA MUHUSIKA AU KARIBU NA MAZINGIRA YANAYOLETA UTATA!

HAFAI KUWA KIONGOZI, HATA UBUNGE NI BUDI AONDOLEWE!!!
 
Hata tusiposikiliza kile mwl. nyerere alisema juu ya lowassa, kiongozi gani asiyeweza hata kujitetea mwenyewe!! lakin angalia mtiririko huu wa matukio:

1.wakati mkataba tata wa buzwagi unasainiwa hotelin uk, lowasa alipitia uk akitokea paris.

2.Anahusishwa na richmond, alishindwa kuvunja mkataba kama alivyofanya kwa city water.

3.Alisafiri kwenda thailand kwa rafiki yake shinawatra eti kutafuta mvua ya kutengeneza, miezi michache baadaye rafiki yake anabainika kuwa mwizi na kuondolewa madarakani.

NI KWA NINI LOWASA KILA PALIPO NA DOSARI YEYE YUPO??? AU YUKO KARIBU NA MUHUSIKA AU KARIBU NA MAZINGIRA YANAYOLETA UTATA!

HAFAI KUWA KIONGOZI, HATA UBUNGE NI BUDI AONDOLEWE!!!
 
Nimeipenda hii mada kwa sababu kuu mbili

  1. Imekuja na hoja, leaving room for discussion

  1. Inatazama pande zote mbili na sio ushabiki tu! Imefikia stage ata wale safi wanaitwa mafisadi..utabaki nani?

Naona ile mada yako imeunganishwa na ile ya SHY!
Kwi kwi kwi!
 
Mzee Mwanakijiji umenikuna, ingawa nimechelewa kuona taarifa yako hii nzito. Nimesoma kwa makini makala ya kumtetea Lowassa. Haisemi kipya, ni bla bla bla zile zile za akina Balile, Mhingo Rweyemamu, Manyerere na Bagenda zinazochapishwa kwenye gazeti la RAI ambalo kirefu chake ni Rostam Agency for Information na magazeti mengine mengi mapya yaliyoanzishwa na Lowassa, Karamagi na Rostam. Swali: ikiwa Lowassa aliona kaonewa, kwa nini alikimbilia kujiuzulu? Jibu jepesi ni kuwa alijua kuwa angeng'ang'ania kwenye Uwaziri Mkuu, Dk. Mwakyembe na timu yake wangelimraruararua. Vilevile nataka kujua kama Lowassa alikuwa na washauri wazuri wa sheria. Inashangaza kuwa Waziri Mkuu ambaye ni Mtawala, analilia haki ya kusikilizwa na subordinate body, yaani Kamati Teule ya Bunge. Forum yake ilikuwa Bunge ambalo hakutaka kulitumia. Lowassa ajue kuwa kadiri wapambe wake wanavyoandika makala za kumtetea kitoto-toto, ndivyo wananchi tunavyozidi kukasirika na kutamani tumfunge huyo jamaa kutokana na uroho wake wa "dili". KUNDADIDEKI! Ijabu
 
Mwandishi wa makala hii kweli ameandika kitoto.
Anampa credit mtu kwa vitu alivyotakiwa kufanya kama wajibu wake!Na alitakiwa kuwa mwema siku zote ndio yasingemkuta yaliyo mkuta.
Yeye alitaka kuwa smart kubana wengine na kuwa mkali (vizuri) ili ku win trust kwa wananchi waamini kuwa ni safi na ndio wale kiulaini (mbaya).
Ripoti ya Mwakyembe iko crystal clear sijuhi mwaandishi wa makala hii anazungusha maneno kiasi cha kunifanya nihisi katumwa na mtuhumiwa au mtuhumiwa mwenyewe akaandika.
Anadai hatetei wakati hata ukimpa mtoto wa shule ya msingi asome atasema nani mwandishi anamtetea au what is the bottom line of the story.
Ametoa reference kuwa kuna viongozi waliojiwa nyuma ,je issue zinafanana vp na je kwa kuwa walihoji huko nyuma ndio sahihi kwa siku zote za mbeleni ?kama kufanya kwao hivyo kulionyesha kuharibu uchunguzi na wao wafanye hivyo,au kila virivyo fanyika nyuma ndo good approach.
Kwani tume ilikuwa ni ya kumchunguza Waziri mkuu au kampuni ?
Mawili yaliopo kama hana maslahi na kampuni hiyo basi ni mzembe mkubwa kuipatia serikali maskini hasara na hastahiki hata ujumbe wa nyumba 10 /10.Ila ukiangalia with naked eyes hata bila microscope uhusiano wa hao viongozi na kampuni ya sasa na viongozi wao ni wazi si wazembe bali wana maslahi na kampuni.
Mwisho alikuwa na nafasi ya kujitetea hata bungeni ila hakuwa na la kujitetea .
 
Kwani kumtetea kuna kosa gani hasa ikiwa una uhakika kaonewa? Unataka ajisemee mwenyewe kwani hujui jinsi ushahidi wa second person ulivyo na nguvu kuliko wake mwenyewe?
Niliwahi kuandika na sasa naandika tena iko siku wote mtaona aibu mtakapojua kilichotokea!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…