Nilipata kigugumizi, na kusikia mwili ukilegea niliposikia eti "Shujaa Kapokelewa kwao" nilipata nafasi kidogo ya kuangalia baadhi ya watu waliompokea kwa haraka haraka wale watu ni wa kukodishwa, kwanza haiwezekani watu wote wale wawe ni wa jimbo la Monduli, wale ni watu ambao wamenunuliwa ili kuonyesha kuwa anakubalika kwao.. Mbona sikusikia kauli ya kiongozi wa juu wa CCM akisimama jukwaani na kusema shujaa amerudi? Unajua bwana Usanii sio mahali popote kuna sehemu nyingine huwezi kucheza usanii... Ina maana hao wananchi wa Monduli wanaishi peponi? ina maana kuwa hawapati hii adhabu ya kulipa gharama kubwa ya umeme? Yes nimeshaenda Monduli mara nyingi tuu wala sijaona hayo maisha yao mazuri kiasi hicho. Barabara sio za kuridhisaha sana zaidi ya ile lami na ni kwa ajili ya TMA na sii vinginevyo? Hizo hela walizotumia kukodisha magari yote na Zulia kwa nini wasijenge machinjio ya kisasa wakaweza kuuza ng'ombe nje ya nchi? Watanzania tuache unafiki na njaa zisizokuwa na maana.. palipo na ukweli usimame ukweli sio wahariri kununuliwa kirahisi namna hii. Hivi haiwezekani vyombo vyote vya habari wakaamua kukaa kimya bila kuandika habari zake?
HIVI huyu Lowassa anapata wapi ujasiri wa kifisadi namna hii?
Mbona kama vile hasikii hata sauti ya kundi kubwa la wana wa nchi (Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu) ambao walimshauri kukaa kimya ili labda historia ije imuibue, yeye hataki kusikia na anapanga kila aina ya makombora kuhakikisha kuwa anarejea serikalini na ikiwezekana kwenye kinyang'anyiro cha 2015.
Mbali na waandishi wachache wenye tamaa, wajinga wa nyakati, wasiokuwa na visheni na zaidi sana bootlickers, sasa ameamua kuwabakiza waandishi ao huko huko Arusha hadi wakachapisha gazeti.
Gazeti hilo liitwalo 'Arusha Raha Kweli' limeingia mitaani muda huu na kumkuta Kamanda mimi nikiwa nimejipumzisha na ka-bia kangu pale Hilfishers Pub mitaa ya jiji la Lusaka. Hapa kuna kibaridi kidogo.
Ilibidi nipumzishe mkono wangu kunyanyua glasi ya bia na kuanza kusoma mara nilipowasilishiwa na hawa jamaa wa kampuni ya kusafirisha vifurushi. Network bwana ni nzuri sana
Hebu sikiliza: Lead story ni 'Lowasa ajibu mapiga na baadaye kukawa na vibwagizo kibao: *awataja waliohusika, wamo vigogo wa serikali * Kuna njama za kuigawa CCM *Alia na Mwakyembe *Madiwani Monduli wacharuka *mahojiano yake yakatizwa ghafla TvT. Limechapwa Dar na kiwanda cha Printech, kile kilichokuwa kinamilikiwa na kina Habari Corporation- Mtanzania, Rai, Bingwa, The African kabla ya kuwashinda na kunyang'anywa na wale waliowakopesha.
Nasikia limesambazwa nchi nzima na linauzwa 300/-, ingawa nasikia liko kwenye mikakati ya kuuzwa 200/- ili lisomwe sana.
Jamani huo ni mkakati, ambao yeye na watu wake wanadhani ni kabambe kumbe masikini ndiyo anamalizika kabisa na muda si mrefu atazimika.
Jadili hatua hii.
Ewe Mama Tanzania, twakulilia. Tutakulinda hata kwa matone ya damu.
HIVI huyu Lowassa anapata wapi ujasiri wa kifisadi namna hii?
Mbona kama vile hasikii hata sauti ya kundi kubwa la wana wa nchi (Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu) ambao walimshauri kukaa kimya ili labda historia ije imuibue, yeye hataki kusikia na anapanga kila aina ya makombora kuhakikisha kuwa anarejea serikalini na ikiwezekana kwenye kinyanganyiro cha 2015.
Mbali na waandishi wachache wenye tamaa, wajinga wa nyakati, wasiokuwa na visheni na zaidi sana bootlickers, sasa ameamua kuwabakiza waandishi ao huko huko Arusha hadi wakachapisha gazeti.
Gazeti hilo liitwalo 'Arusha Raha Kweli' limeingia mitaani muda huu na kumkuta Kamanda mimi nikiwa nimejipumzisha na ka-bia kangu pale Hilfishers Pub mitaa ya jiji la Lusaka. Hapa kuna kibaridi kidogo.
Ilibidi nipumzishe mkono wangu kunyanyua glasi ya bia na kuanza kusoma mara nilipowasilishiwa na hawa jamaa wa kampuni ya kusafirisha vifurushi. Network bwana ni nzuri sana
Hebu sikiliza: Lead story ni 'Lowasa ajibu mapiga na baadaye kukawa na vibwagizo kibao: *awataja waliohusika, wamo vigogo wa serikali * Kuna njama za kuigawa CCM *Alia na Mwakyembe *Madiwani Monduli wacharuka *mahojiano yake yakatizwa ghafla TvT. Limechapwa Dar na kiwanda cha Printech, kile kilichokuwa kinamilikiwa na kina Habari Corporation- Mtanzania, Rai, Bingwa, The African kabla ya kuwashinda na kunyanganywa na wale waliowakopesha.
Nasikia limesambazwa nchi nzima na linauzwa 300/-, ingawa nasikia liko kwenye mikakati ya kuuzwa 200/- ili lisomwe sana.
Jamani huo ni mkakati, ambao yeye na watu wake wanadhani ni kabambe kumbe masikini ndiyo anamalizika kabisa na muda si mrefu atazimika.
Jadili hatua hii.
Ewe Mama Tanzania, twakulilia. Tutakulinda hata kwa matone ya damu.
Lowassa ni hatari kuliko nyoka. Ashughulikiwe mapema kabla hajaleta maafa nchini. Nadhani hata ile kauli ya Ole Naiko inatoka kwenye hilo kundi la kina Lowassa. Ni mikakati michafu imeanza.
Waziri wetu mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda yuko ziarani Rukwa kwa siku saba 'kukagua' shughuli za maendeleo huko na nadhani sana sana ni kuwaona ndugu na jamaa zake baada ya kupata nafasi ya ukulu, ukubwa na uzee aliouachia Lowassa.
Sasa akiwa katika kijiji cha Kakese leo asubuhi amemtetea Edward Lowassa akisema kuwa kosa alilotenda Lowassa ni la kwanza na kwamba Waswahili husema kosa siyo kosa hadi utakapolirejea.
Pinda akizungumzia kashfa ya Richmond alisema Lowassa hapaswi kulaumiwa kwa kuwa yaliyomkuta ni miongoni mwa changamoto za uongozi na kwamba alifanya vyema kujiuzulu baada ya wanaomsaidia kuhusishwa na sakata la kampuni ya mfukoni ya Richmond ambayo ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.