Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

1. Mlungura

2. Masrahi yao yanashabihiana (Exploiters/Bourgeoisie)
 
Lazaro Nyarandu kavunja rekodi ya kupata wadhamini wengi zaidi mkoani Arusha. Kamfunika Edward Lowassa tena nyumbani kwao. Hapo kuna kitu nimejifunza.
 
Niliangalia chanel 10, walisema nao laki 2 ila nina mashaka nao pia kama itv, habari zingine za kitaifa ilikuwa ni kama dk 1 na nusu hivi, ya lwasa ilichukua ka dk tano na ushee hivi tena wakati wa habari!

Wewe nae ni muongo wa kutupwa ina maana leo ITV walikuwa na habari moja? Unafikiri hatuangalii TV...habari ya lowasa imeambatana na ya Membe ,january makamba na ya Nyarandu....!
 
Channel Ten pia je ni waongo?
Wao wamesema kapata zaidi ya 212,000
hao 95,251 ni wilaya ya kinondoni tu lakini jumla ya wilaya zote ndio 212,000 futilieni mambo sio mnakurupuka!!
 
hao 95,251 ni wilaya ya kinondoni tu lakini jumla ya wilaya zote ndio 212,000 futilieni mambo sio mnakurupuka!!

Sijakurupuka, mimi nimesema kwa Dar nzima kama mleta mada alivyosema
 
Ee Mwenyenzi Mungu endelea kumpigania Edward lowassa.
 
Hivi mtu anawezaje kuhonga nyomi yote hii!?? Ifike mahali watu wakabiliane na ukweli tu na ngonjera kwamba Lowassa anahonga watu zisipewe nafasi
 
ITV wameonyesha huko Monduli katika kijiji cha Kapenjiro wazee wakilima barabara kwa panda na majembe ili waweze kusafirisha wagonjwa kwa punda.
Nimejuuliza iweje tuhadehiwa kwamba mgombea urais anauchukia umaskini na iyo wote tutakua matajiri, wakati ni mbunge wa sehemu hiyo kwa zaidi ya miaka 25?!
 
Atajaza malori yake barabarani hatutakuwa na reli wara air tz hatari hii
 
Umeiona ITV tu vyombo vingine vya habari haujasikia? Acha ubwege sikiliza vyote kisha ndio useme sio unatuhumu chombo kimoja mwehu wewe
 
Sijakurupuka, mimi nimesema kwa Dar nzima kama mleta mada alivyosema

Mleta mada hajaelewa, naamini akipewa mtihani hapati kila swali kuna baadhi huwa anayakosa sasa kwa hili ni miongoni ya maswali aliyokosa hajaelewa kakurupuka!!!
 
Kwani alishindwa kuyafanya hayo kwa miaka 30 au tokea 77 ndani ya miezi ndo aifanye ama kweli sie manyumbu tunaliwa
 
tulikuepo mwanzo mwisho,tulianzia lumumba tukafata temeke na kumaliza na kinondoni.jumla yake ni takriban wadhamin 217000,huku kinondon pekee wakitia fora kwa wadhamin takriban laki na kitu

sasa watu wote lowasa anapeleka wapi maana nimeona wezake wakikabizi majina yasiyo zidi 30-35 kwa kila mkoa,sasa hayo majina ya watu wengi hivyo anampelekea mke wake?
 
AMKA TANZANIA

Mpuuzi yeyote hufurahi mno anapomwona mtu analalamika, na mimi nasema Watanzania tulio wengi tunachukua muda mwingi mno kulalamika na si kuweka mipango, Oktoba ni kesho kutwa na tumeshamwona nani mwenzetu na nani mpuuzi, tufanye maamuzi, majitu sahiz yamekomaa na #team badala ya kupigania Nchi, hela zikiisha yalizohongwa ndo utayasikia yanalalamika shemeji katufanya hivi shemeji katufanya vile ujinga mtupu, hivi tumerogwa na nani?

Mkulima unadanganywa na sera dhaifu za kilimo kwanza, kilimo kiko kijijini pembejeo ziko Dar zinafanya nini? Kulima mnalima, masoko hakuna na wala hakuna anayejishughulisha na hilo, mtakufa njaa nyie

Kijana unapelekwa VETA kusomea ufundi, Viwanda hakuna huo ufundi unaupeleka wapi zaidi ya kuanzisha vijiwe vya kutengeneza vibatari, shtuka mtanzania

Hospitali hazina Dawa, unaenda Hospitali ya Wilaya hadi Panadol eti unaelekezwa kanunue duka lilee, hilo Duka la mtu binafsi lilipataje Dawa hospitali ikakosa?

Kila siku majitu mazima yanapiga kelele eti vijana mjiajiri vijana mjiajiri, familia zao Baba, Mama, Mtoto, wote wajumbe wa NEC, saa ngapi watajua kama Mtaji ni tatizo? Hivi unawezaje kujiajiri bila mazingira wezeshi?

Wafanyakazi wengi wanakufa maskini kwa sababu Serikali inawanyonya mpaka kwenye mifupa, mtu mshahara 400,000/= halafu take home 290,000/=, kweli are you serious? Huko mijitu bila aibu inasema tumeongeza mafao ya wastaafu kwa 100% (kutoka 50,000/= hadi 100,000/=) kweli, yani mzee aliyelisotea Taifa lake kwa zaidi ya miaka 30 ya maisha yake leo unaona raha kumpa Mil.1 kwa mwaka is it possible, aibu huwa mmezihifadhi wapi mnapotamka mambo kama haya? Mzee huyu bila shaka hata kiinua mgongo chenyewe alipata Mil.7, leo hii Mbunge mmoja anajinyakulia Mil. 230, halafu eti majitu hata hayashtuki?

Tatizo la watanzania tumeshakubali kutenganishwa, hatuko pamoja tena, ukiona mfanyabiashara anasumbuliwa na miradi isiyoeleweka kama ile ya mashine za EFD basi wewe Mwalimu unaona halikuhusu, unapomwona Mkulima analalamika Pembejeo basi wewe Dereva wa Basi unaona halikuhusu wakati huo huo unasahau kama familia yako inategemea Kilimo, amkeni watanzania, tuzungumze kama Taifa, tunategemeana ktk mahitaji, udogo wa mshara wa Mwalimu una athari ya moja kwa moja kwako mfanyabiashara wa Viazi

Wakati wa kumwondoa asiyefaa ni sasa, kajiandikishe, mwamshe aliyelala mwambie Nchi imeshauzwa, mwambie ukweli kwamba Mwekezaji wa madini anapokuja anapewa miaka5 ya kufanya kazi bila Kodi huku mzawa akifungua kibanda cha Saluni, hata kabla hajamaliza kukipaka rangi anatakiwa aonane na TRA, mwambie mwaka jana pekee ripoti ya CAG inaonyesha zaidi Bilioni 800 zimepigwa na familia zisizozidi sita, ndo mfumo wa sasa.

Ni wakati wa #team Tanzania, achaneni na #team matumboyawatu
 
Nionyeshe marafiki zako namie ntakuambia tabia yako.
Mie ni helA ya mboga pesa ya ugoro aka Rugemalira vijisenti mengi rostam na bakheresa
 
watu wa dar wanatia aibu ete wenaenda kusikiliza lowasa kwa lipi analoongea huyo nimewazarau
 
Back
Top Bottom