Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Wakati huu mchakato wa wanachama wa CCM waliochukua fomu kuwania kuteuliwa kukiwakilisha chama katika kinyang'anyiro cha urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu 2015 wakizunguka mikoa mbali mbali kutafuta wadhamini, waziri mkuu aliyejiuzulu ambaye naye anawania kuteuliwa anaonekana kupewa upendeleo wa wazi kwenye vyombo vya habari kama televisheni, redio na magazeti.

Mimi binafsi sijaelewa kama upendeleo huu ni kutokana na mhusika mwenyewe kuwagharimia waandishi wa habari au ni vyombo vyenyewe ndio vinaonesha upendeleo huo au kuna asali imepitishwa ili jamaa apewe promo kubwa. Ukweli ukifuatilia taarifa za mizunguko ya watia nia wakitafuta wadhamini, Lowassa anapambwa sana na vyombo vya habari hasa TV kuliko wenzake.

Yaani wengine hata hawasikiki utadhani wamechukua fomu na kwenda nazo nyumbani. Mimi nashauri vyombo vya habari kutupa habari kwa haki na usawa kwa watia nia wote hasa kama taarifa zao zinagharimiwa na vyombo husika.

Lakini Kama ni watia nia wenyewe ndio wanaogharimia waandishi hapo sina neno kwani jamaa yule mpunga kwake sio tatizo na kila mwandishi angependa kuambatana naye maana wahenga walisema "Fuata asali ule nyuki"

Jamani hebu ifike mahali tuangalie ukweli na uhalisia uliopo mbona vyombo vya habari vinavyomkebehi lowassa kuutwa kila siku mbona hamsemi kwamba vinampendelea?

Kwa maajabu yanayotendeka katika mikusanyiko ya anapokua lowassa jamani hata kama Mimi mwandishi lazma ningechukua habari na kupiga picha maana inapendeza jinsi watanzania walivyokua na muamko wa mabadiliko jinsi watanzania sasa wameamua kumpa support mtu wanaeamini kua ndie atawapa Tanzania waliokua wanaitamani.

Haijawahi kutokea katika historia ya tanzania mafuriko ya watu katika wagombea wa ccm na wengine kwanini vyombo vya habari visikusanye habari hizo na kuweka historia?

Hyo dhana ya kwamba mtanzania hafanyi jambo jema bila pesa mmeitoa wapi mbona mnawadhalilisha watanzania mwenzenu kwa shutuma ambazo hata hazina ukweli

Mnawadhalilisha waandishi wa habari kua wana njaa wakati ni kazi yao kutoa habari pale inapobidi.

Kwani wagombea wengine habari zao hazitoki? U nadhani hawataki? Ni kwamba wamezidiwa na mafuriko wanaona aibu kwa majigambo yao sasa magazetini wakaonekana watu hata mia hawafiki kwao ni fedheha sio kwamba vyombo vya habari vinapendelea.

Lowassa watu wanamhitaji jamani acheni utani, acheni chuki tena bila kumung'unya maneno
 
Lowassa n chaguo la watz wengi wanaoamini mabadiliko ktk utendaj na utoaji wa maamuz sahih kwa wkt shh,mtu yyte anaempinga Lowassa haitakii mema nchi yetu tumpuuzen hana maana kbsa,watanzania tumeamka hatuburuzwi tena kama zaman kipndi tunachaguliwa viongoz sasa tunachagua wenyew tunaemtaka cc,ambaye c mwingine n Lowassa chaguo la watu,
 
Jana Makongoro Kaongea na Vyombo vya Habari lakini tofauti na mwanzo Kabla hajawa Tishio inaonekana Sasa kuna mkakati wa wazi wa kuhakikisha Habari zake haziandikwi au kutoka TV na redio ..,haya ndio madhara ya TV kumilikiwa na matajiri Wenye malengo maalum ...Sasa Tanzania hatuwezi Tena Kusema tuna Vyombo Huru vya Habari au waandishi Huru .
Majuzi kahojiwa na Vyombo vya Habari vya Kimataifa ikiwemo BBc ,..utashangaa Habari nayo ikahujumiwa kutoka hewani ....Pengine uingereza na marekani nao wameambiwa kuna wagombea hAwatalinda maslahi Yao hivyo Vyombo vyao visiwape umuhimu ???
Tutasema tuna uchaguzi ..?? Basi tuacheni matajiri watuamulie Rais ..Sio uchaguzi Huu ..Bali ni Mtandao ...unaendelea
 
Mkuu imenisikitisha sana Jana , vyombo kama Itv , star TV,channel ten n k vilikuepo msasani lakini havikurusha na aliongea vitu vya msingi mno , lakini nawapongeza RAIA Tanzania , wametoa habari yake Leo bila hata shilingi moja huo ndio uzalendo , Leo kaongea na azam TV hivyo usiku tuangalie habari tuone kazungumza nini

Kiukweli mafisadi wamedhamilia kuiteka hii nchi lakini wazalendo tunasema tuko nae mpka mwisho na mpka aingie ikulu kurudisha nidhamu ya serikali na chama na tatizo kubwa nchi hii n CCM , ikishajirekebisha nchi itasonga mbele tofauti na hapo mwaka huu ukawa wanachukua nchi kwani wazalendo tuna hasira sana na CCM
 
Mkuu ingekuwa vizuri kama angeshauriwa awe anarekodi tu mazungumzo yake kwa audio au video kwa camera ya kawaida tu na kuturushia humu. Akifanya hivyo sisi wenyewe tutasambaziana kwa wasap. Media za bongo zinamilikiwa na mafisadi, no way wakampa promo, hata mzee machache naye si unaona yuko kwa fisadi

cc DSN
 
Last edited by a moderator:
Naanza kuelewa umuhimu wa kurudisha NCHI kwa wananchi ...yaaani Vyombo Sio Huru na hata waandishi Sio Huru ..hata wawakilishi wa Vyombo vya kimataifa wanaweza kutumika ...haiwezekani matajiri wanahodhi Hadi Habari gani tusome ..ipi tuone ....TULIKUA na Berlusconi mmoja Sasa Hivi wamekuwa wawili au watatu ...
Kwenye Vyombo vilivyobakia wanawaandishi ambao kazi Yao Kuchuja hata Kama gazette la chama ...au serikali ...Leo Mtanzania Daima pia imetoa Habari ya Makongoro ..nikaona kaongea mambo ya Msingi sana ..waliobakia hakuna KITU ...ifike mahala waandishi waone Aibu hata Kama ni njaa
 
Philemoni Mikael na Baro, nsugu zangu nilihisi kuumwa hata kulala sikupata usingizi vizuri. Hawa mafisadi wameamua kununua vyombo vyote ila kama mlivyosema, nahisi tunaweza kuwaambia CCM ni nini tunataka na tukafanya kweli, sijuhi tufanyaje lakini sisi wazalendo tuna haja ya kuanzisha kitu cha kupambana na hawa mafisadi kwa ajiri ya kumpigania mwenzetu Mako. Inasikitisha na inauma mno, tuwaambie tu CCM kama wanaamua vinginevyo basi sisi wazalendo wa Taifa hili tutakula na tutakufa pamoja tukiwa na Makongoro. Tupinge waziwazi kwa sauti kuu ili wajue huko waliko nchi hii, nchi yetu haiuzwi ..it is not sale, full stop!
 
Hahahahah unataka naye iwe kama nywele nyeupe eheeee

Ingependeza wote wapewe Haki sawa ...lakini media zote za wana Mtandao wa 95 todate ....haya Hao TBC one wanaoendeshwa kwa Kodi ingetakiwa watende haki kwa wote na vyama vyote ..lakini nako kuna waandishi na waharirii wanaofugwa

Nadhani Mdau Kusema vyema watangaza nia Kama Makongoro ,Agustine Ramadhani ,MAHIGA ..mhuongo etc ambao Sio wana Mtandao wawe wanarekodi warushe YouTube

Wanamtandao wanatuzungua tu ,..wote Lao moja
 
Huo ni mtazamo wako tu kwamba anapendelewa
Badala useme nyota yake inang'aa kila kona anaonekana yeye tu ina maana hata tukishinda pamoja utasema wapigakura wamempendelea badala ya kusema ameshinda

ila sishangai mtu mwenye id kama yako akimshangilia fisadi, najua upo kwenye harakati zakutaka ule kwa mgongo wake
 
Mkuu ingekuwa vizuri kama angeshauriwa awe anarekodi tu mazungumzo yake kwa audio au video kwa camera ya kawaida tu na kuturushia humu. Akifanya hivyo sisi wenyewe tutasambaziana kwa wasap. Media za bongo zinamilikiwa na mafisadi, no way wakampa promo, hata mzee machache naye si unaona yuko kwa fisadi

cc DSN

Mkuu umeleta wazo zuri, nilikuwa nawaza njia gani tunaweza tukaitumia ili tukapambana na hawa makuhadi wanaoiteka nchi yetu nyara kwa pesa. Naamini hii njia itatusaidia turushiwe hotuba zake zote tuanze kuzipitisha mitaani ili wananchi waelewe, kama tunataka kulikomboa Taifa letu ni lazima tukawaelemisha wananchi kwa njia zote na kwa vile naelewa Jana kuna watu wamerekodi basi zisambazwe pote kwenye mitandao na hata kwenye CDs ikibidi watu waelimishwe
 
Kweli kabisa mkuu, hatuba zake zikishawekwa hapa tunadownload tunasabambaza kwenye magroup yetu mbalimbali ya wasap, facebook, insta, tweeter n.k ujumbe utafika tu. Tena kwa taarifa yako ujumbe wa audio unawafikia wananchi wengi zaidi, maana kuna wale wasio na smartphone so hawana hizi jamii za kina wasap. Halafu ujue kuna kundi kubwa sana la watu hasa kinamama na wadada wengi wao hawaangaliagi taarifa ya habari, ila kwa njia hizi nilizozitaja ujumbe utawafikia tu.
 
nimewafatilia sana ITV,wamekuwa wakimrusha sana lowassa au ndio mambo ya ukanda?mbona watia nia wako wengi sana ccm lakini chombo hicho kimekuwa kikirusha sana lowasa kuliko wagombea wengine.....tumesha jua ajenda yenu ninyi watu wa lowassa na ukaskizini.

huyu nayee usiangalie I T V amgalia TBC wako CLAUD TV wengine STARTV pamoja na CHANEL 10 bila kusaha ATN hata BBC SWAHILI au hamia DSTV ili uweze kuwaona hao umaotamani kuwaona:bathbaby:
 
Makongoro yuko vizuri....wezi na matapeli wa nchi hii hawampendi makongoro maana wezi hao na washirika wao wanaomoliki vyombo vya habari(...
..)hawataki aje mtu kama makongoro maana atawanyima adhima yao.....wengine walifilisi NBC
...usizani hatuwajui.
 
Kuunganisha thread Hii ndio sehem moja nyingine ya kubana Habari ...Habari hapa ni Makongoro na wagombea wengine wa Aina yake Kama Augustin Ramadhani..MAHIGA ..etc kubanwa....hili la anayependelewa ni tofauti
 
Mkuu umeleta wazo zuri, nilikuwa nawaza njia gani tunaweza tukaitumia ili tukapambana na hawa makuhadi wanaoiteka nchi yetu nyara kwa pesa. Naamini hii njia itatusaidia turushiwe hotuba zake zote tuanze kuzipitisha mitaani ili wananchi waelewe, kama tunataka kulikomboa Taifa letu ni lazima tukawaelemisha wananchi kwa njia zote na kwa vile naelewa Jana kuna watu wamerekodi basi zisambazwe pote kwenye mitandao na hata kwenye CDs ikibidi watu waelimishwe

Kweli kabisa mkuu, hatuba zake zikishawekwa hapa tunadownload tunasabambaza kwenye magroup yetu mbalimbali ya wasap, facebook, insta, tweeter n.k ujumbe utafika tu. Tena kwa taarifa yako ujumbe wa audio unawafikia wananchi wengi zaidi, maana kuna wale wasio na smartphone so hawana hizi jamii za kina wasap. Halafu ujue kuna kundi kubwa sana la watu hasa kinamama na wadada wengi wao hawaangaliagi taarifa ya habari, ila kwa njia hizi nilizozitaja ujumbe utawafikia tu.
 
Kuunganisha thread Hii ndio sehem moja nyingine ya kubana Habari ...Habari hapa ni Makongoro na wagombea wengine wa Aina yake Kama Augustin Ramadhani..MAHIGA ..etc kubanwa....hili la anayependelewa ni tofauti

Sijui kwanini mods wanaunganisha habari za Makongoro kwenye huu uzi wa fisadi, ilihali kuna nyuzi kibao humu za Makongoro
 
Back
Top Bottom