Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Acha ujinga.Wenzio walikuwepo kwenye mkutano wa EL,wewe ulikuwa kwenu unakula maharage afu unapinga.

ITV wamewapa airtime karibu wagombea wa-4 leo;hao wengine hukuwasikia?.
EL Atawatesa sana mwaka huu.
 
hao 95,251 ni wilaya ya kinondoni tu lakini jumla ya wilaya zote ndio 212,000 futilieni mambo sio mnakurupuka!!

212,000 .. badala ya 30! (ziada ya 211,970). Huu ni upuuzi mtupu na ni matumizi mabaya ya resources. Halafu naona Edward ana mlinzi wake na Regina naye ana mlinzi. I bet .. huyu mtu atakuwa mfujaji kuliko wapangaji wa Ikulu waliomtangulia
 
Wewe nae ni muongo wa kutupwa ina maana leo ITV walikuwa na habari moja? Unafikiri hatuangalii TV...habari ya lowasa imeambatana na ya Membe ,january makamba na ya Nyarandu....!

Mwambie huyo anafikiri taarifa ya habari kaicheck peke yake!
 
Ujinga mtupu mpaka dar,sijui tusubir nani aje atuzibue akili watanzania hatujielew kabisa
 
Alafu huyu jamaa muongo sana, kumaliza tatizo la foleni dar ndani ya miezi sita?? alikuwa waziri mkuu kwa miaka kadhaa, akashindwa, alafu cha ajabu HASEMI atalitatua vipi, anasema tuu tatizo la foleni nitalimaliza ndani ya miezi sita na wapumbavu wanashangilia!
Watanzania wengi kweli tuna ufinyu wa akili, dar ikiongozwa na Wabunge wake wa sisiemu! Zungu nilikuwa namuona angalau kama jembe fulani, leo KANITAPISHA!
Na Yule babu aliyenyonyoka nywele naona anaanza kuwa "dogo" tena, diapers nafikiri zinamuhusu!
 
Hiyo idadi inajaa uwanja wa Taifa?
Vp uwanja wa arusha ule ulikuwa na watu kiasi gani?
Mahesabu hayajakaa vizur.....iliwachukua muda gani kila mmoja kusaini na huku wakisubiriana...katibu hao walikuwa wanahakiki vp...watu laki mbili...dah...hongereni
 
AMKA TANZANIA

Mpuuzi yeyote hufurahi mno anapomwona mtu analalamika, na mimi nasema Watanzania tulio wengi tunachukua muda mwingi mno kulalamika na si kuweka mipango, Oktoba ni kesho kutwa na tumeshamwona nani mwenzetu na nani mpuuzi, tufanye maamuzi, majitu sahiz yamekomaa na #team badala ya kupigania Nchi, hela zikiisha yalizohongwa ndo utayasikia yanalalamika shemeji katufanya hivi shemeji katufanya vile ujinga mtupu, hivi tumerogwa na nani?

Mkulima unadanganywa na sera dhaifu za kilimo kwanza, kilimo kiko kijijini pembejeo ziko Dar zinafanya nini? Kulima mnalima, masoko hakuna na wala hakuna anayejishughulisha na hilo, mtakufa njaa nyie

Kijana unapelekwa VETA kusomea ufundi, Viwanda hakuna huo ufundi unaupeleka wapi zaidi ya kuanzisha vijiwe vya kutengeneza vibatari, shtuka mtanzania

Hospitali hazina Dawa, unaenda Hospitali ya Wilaya hadi Panadol eti unaelekezwa kanunue duka lilee, hilo Duka la mtu binafsi lilipataje Dawa hospitali ikakosa?

Kila siku majitu mazima yanapiga kelele eti vijana mjiajiri vijana mjiajiri, familia zao Baba, Mama, Mtoto, wote wajumbe wa NEC, saa ngapi watajua kama Mtaji ni tatizo? Hivi unawezaje kujiajiri bila mazingira wezeshi?

Wafanyakazi wengi wanakufa maskini kwa sababu Serikali inawanyonya mpaka kwenye mifupa, mtu mshahara 400,000/= halafu take home 290,000/=, kweli are you serious? Huko mijitu bila aibu inasema tumeongeza mafao ya wastaafu kwa 100% (kutoka 50,000/= hadi 100,000/=) kweli, yani mzee aliyelisotea Taifa lake kwa zaidi ya miaka 30 ya maisha yake leo unaona raha kumpa Mil.1 kwa mwaka is it possible, aibu huwa mmezihifadhi wapi mnapotamka mambo kama haya? Mzee huyu bila shaka hata kiinua mgongo chenyewe alipata Mil.7, leo hii Mbunge mmoja anajinyakulia Mil. 230, halafu eti majitu hata hayashtuki?

Tatizo la watanzania tumeshakubali kutenganishwa, hatuko pamoja tena, ukiona mfanyabiashara anasumbuliwa na miradi isiyoeleweka kama ile ya mashine za EFD basi wewe Mwalimu unaona halikuhusu, unapomwona Mkulima analalamika Pembejeo basi wewe Dereva wa Basi unaona halikuhusu wakati huo huo unasahau kama familia yako inategemea Kilimo, amkeni watanzania, tuzungumze kama Taifa, tunategemeana ktk mahitaji, udogo wa mshara wa Mwalimu una athari ya moja kwa moja kwako mfanyabiashara wa Viazi

Wakati wa kumwondoa asiyefaa ni sasa, kajiandikishe, mwamshe aliyelala mwambie Nchi imeshauzwa, mwambie ukweli kwamba Mwekezaji wa madini anapokuja anapewa miaka5 ya kufanya kazi bila Kodi huku mzawa akifungua kibanda cha Saluni, hata kabla hajamaliza kukipaka rangi anatakiwa aonane na TRA, mwambie mwaka jana pekee ripoti ya CAG inaonyesha zaidi Bilioni 800 zimepigwa na familia zisizozidi sita, ndo mfumo wa sasa.

Ni wakati wa #team Tanzania, achaneni na #team matumboyawatu

Uko sahii mkuu ila kila siku najiuliza wale waishio vijijini tens ndio kuna shida na matatizo lukuki ndio haohao wanaiona CCM ni mkombozi wao ili hali kwa miaka yote waliokaa madarakani haijawaletea nafuu yoyote ile.
 
Hiyo idadi inajaa uwanja wa Taifa?
Vp uwanja wa arusha ule ulikuwa na watu kiasi gani?
Mahesabu hayajakaa vizur.....iliwachukua muda gani kila mmoja kusaini na huku wakisubiriana...katibu hao walikuwa wanahakiki vp...watu laki mbili...dah...hongereni

Wadhamini wanatafutwa kabla kama hujui ..kichwa kama dafu
 
Hata akipata watu laki mbili kwani wanaohitajika si 90 tu? Hao wengine ni useless

kaka ni 30 tu na form ina mpaka 45, huyu jamaa na watu wake wanapropaganda kubwa sana maana kusajiri wadhamini 200,000 au hata 50,000 unahitaji wiki hata mbili so hao wote ukusanye kadi zao na wajisajiri sio mchezo. jina lazima likatwe na mwacha aende ACT

Sasa watakatwa 35 akiwemo ndani sasa ulalamike ili iweje hao wengine mbona wamekatwa. hapo ndio patamu leo nakuambia makundi yote yanakatwa kuvunja mzizi wa fitina so enzi za mkapa kurudi tena
 
Niliangalia chanel 10, walisema nao laki 2 ila nina mashaka nao pia kama itv, habari zingine za kitaifa ilikuwa ni kama dk 1 na nusu hivi, ya lwasa ilichukua ka dk tano na ushee hivi tena wakati wa habari!

Mkuu hiyo sio TV ya Taifa na wala huchangii hata kumi katika kurusha matangazo yao

Hivyo huwezi mpangia mmiliki nini cha kutangaza na kwa muda gani ili mradi tu asivunje sheria za nchi

IPP Media ni wafanya biashara na wanataka faida kwa hiyo lazima warushe zile habari ambazo zitawapa watazamaji wengi ili wapate matangazo mengi ili kuendesha kituo chao.
 
kaka ni 30 tu na form ina mpaka 45, huyu jamaa na watu wake wanapropaganda kubwa sana maana kusajiri wadhamini 200,000 au hata 50,000 unahitaji wiki hata mbili so hao wote ukusanye kadi zao na wajisajiri sio mchezo. jina lazima likatwe na mwacha aende ACT

Sasa watakatwa 35 akiwemo ndani sasa ulalamike ili iweje hao wengine mbona wamekatwa. hapo ndio patamu leo nakuambia makundi yote yanakatwa kuvunja mzizi wa fitina so enzi za mkapa kurudi tena

usiwe mpumbavu kam nyumbu au farasi
 
Back
Top Bottom