Kwanza ninampa Hongera sana Zitto kwa kufika salama nyumbani kwao Kigoma ya watanzania. Nina imani ujio wake huko utakuwa na maana sana kwa watanzania wanaoishi huko. Kwa kuangalia viunga vya mahali msafara umepita unaonyesha kabisa Zitto hajamaliza kazi ya kusaidia kuwaletea maendeleo watanzania waishio Kigoma.
Madhumuni ya 'post' hii ni kuonyesha kutofurahishwa na maneno ambayo yasemekana Zitto. Maneno hayo nimeyapaka rangi Nyekundu hapo juu.
Kama kweli Zitto ameyasema , basi amethibitisha kuwa ana udhaifu mkubwa wa kiuongozi. Ni udhaifu mkubwa kwa sababu huwezi kumtofautisha na Idd Amini (aliyekuwa Rais wa Uganda). Ni watu jamii ya Idd Amini waliokuwa wanajikweza kwa kujipa vyeo lukuki mbele ya wale anaowaongoza ni hii ni dalili ya ubinafsi, ambayo haifai kuwa sifa ya kiongozi bora. Sote tunajua alichoifanyia Uganda na Tanzania Idd Amini.
Pia nimesoma baadhi ya mabango kwenye picha yakisema " Zitto kama Mandela, Zitto kama Nyerere". Hao wote waliofananishwa naye hakuna hata mmoja ambaye alikuwa anajikweza juu ya wenzake , kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.
Ni haki ya watanzania waishio Kigoma kumpokea mbunge wao kama walivyofanya, lakini kama wanataka aendelea kuwawakirisha basi hawana budi ku'mfunda' Zitto zaidi kuwa kiongozi mwenye sifa zinazofaa.