Lowassa aenda Ujerumani kwa matibabu

Lowassa aenda Ujerumani kwa matibabu

Subirini msemaji wake wa JF aje atuambie anaumwa nini.

cc: Pasco wa JF
 
Last edited by a moderator:
Aende CCBRT? We unadhani ye ana uwezo mdogo wa kufikiri kiasi gan? Unakumbuka mwenyekiti wa chama chao alisema wazi hawaaminiani ata kuachiana glass za maji? Jinsi alivyotishio ndani ya chama wanatamani ajichanganye popote wamdhibiti maana kwa utaratibu wa kawaida imeshashindikana. Pia tatizo la macho sio kigezo za kushindwa kuongoza TZ, hamkumbuki kuna mwingine alikuwa anazimika zimika ghafla lkn mambo yameenda japo kiugumuugumu?

Hilo nalo neno mkuu.
 
Get well soon EL! ila hufai kuwa president! ukitoka ujerumani pitia houston,Texas, kuangalia kampuni yako ya richimonduli.
achana na siasa ili utibie macho yako.
 
Ile pressure ya macho imezidi kumsumbua.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huyu Mmasai hana tofauti na huyu Mkwele wetu.

Wote wako kwenye Palliative care, wao kila siku ni dawa, vipimo na daktari.

Kuwapa uongozi wa juu kama urais ni kuwachosha zaidi na kuwaua mapema.
 
Ee mola mchukue hukohuko lakini si kama tutavyo sisi bali mapenzi yako yatimizwe, kwa jinsi alivyowanyonya watz anasitahili kuja kwako huko mbinguni umshughulikie hukou ameendelea kutumia fedha aliotuibia kutuhonga wenyewe yuaani anatukaanga kwa damu na mafuta yetu wenyewe. Rip EL.
 
Ngoma ni kama mimba chalie yangu, lazima itajitokeza tu. Huyu hafasi kuwa kiongozi on health grounds. Atatutia gharama za mazishi na kubwa zaidi za uchaguzi. Dhooful Khaali..!
 
Afya mgogoro, huyu hafai kuwa rais, ataliingiza taifa kwenye mzigo mkubwa wa gharama kuandaa msiba wa kitaifa

Mkuu wewe unajua siku yako ya kufa??
Grow up
Mbaya zaidi unajiita GT hiyo comment imekaa ki GT?
 
Nimepunguza credit kwake, anawapuuza madaktari wetu tuliowasomesha kwa gharama kubwa kama alivyotoa hoja Spika Makinda kuhusu afya za wabunge. Kweli Magamba ni Magamba tuuuu!!!!!




Mkuu hawa jamaa siyo kuwa hawamini wataalam wetu wa ndani yaan DR but worry yao nazani hawataki wafamike nini has kinawasumbua!!!!!!
 
edward_lowasa.jpg



Edward Lowasa

ALIYEKUWA Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa yupo nchini Ujerumani kwa matibabu na uchunguzi wa kiafya.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli jana hakuwapo katika uzinduzi wa mradi wa Barabara ya Minjingu hadi Arusha na shule jimboni kwake, uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete aliye ziarani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga na baadaye kusambazwa kwa waandishi wa habari, Lowassa alieleza kusikitishwa kutokuwapo jimboni kwake wakati huo ambao Rais Kikwete anatembelea jimbo lake.

Lowassa alisema kuwa, hali hiyo imetokana na kuwa safarini kwa ajili matibabu lakini akasema anaamini mambo yataenda vizuri si kwa ziara hiyo ya Rais Kikwete bali hata vikao vya juu vya CCM vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika taarifa hiyo, alimsifu Rais Kikwete kuwa, kutokana na kutekeleza vizuri na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, wiki mbili zijazo wanaCCM watakwenda Dodoma kuidhihirishia dunia na Watanzania wenye shaka kwamba wanamwamini na kuuthamini uongozi wake.

Katika maelezo hayo, Lowassa alieleza tatizo linalomsumbua kuwa ni macho, lakini pia atatumia nafasi hiyo kuchunguza afya yake.

Aidha, alimshukuru Rais Kikwete kwa kuzindua miradi hiyo akisema inadhihirisha mambo mawili makubwa aliyoyafanya kwa kiwango cha juu chini ya uongozi wake akiwa Rais wa Tanzania.

“Mosi, chini ya uongozi wako shule nyingi zaidi zimejengwa kuliko awamu zote zilizotangulia. Pili, kilomita za barabara za lami zilizoongezeka wakati wa awamu yako ni ndefu kuliko wakati mwingine wowote,” alisema Lowassa na kuongeza:

“Kwa hakika umetekeleza vizuri, kikamilifu na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, mwaka 2005 na 2010. Sisi wanachama wa CCM na wananchi wa Monduli ni mashahidi wa jambo hili. Tunaamini ndivyo ilivyo kwa nchi nzima.”

Mwishoni mwa wiki ijayo CCM itafanya uchaguzi mkuu wa uchaguzi ngazi ya taifa kuanzia mwenyekiti wa chama na viongozi wengine, ili kukamilisha kupanga safu mpya ya uongozi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015.

CCM ipo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ambapo tayari jumuiya zake za Wazazi, Vijana na Wanawake zimekamilisha chaguzi hizo, huku kambi ya Lowassa ikitajwa kuibuka kidedea kwa kunyakua nafasi mbalimbali zilizowaniwa, kuanzia ngazi za wilaya hadi jumuiya za chama kitaifa.

Katika uchaguzi wa UWT, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa, Sophia Simba ambaye alitetea nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa, huku wajumbe sita kati ya wanane waliochaguliwa kuwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambi hiyo.

Wajumbe sita kati ya wanane walioshinda nafasi za ujumbe wa NEC kupitia jumuiya hiyo wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa, huku mmoja akitajwa kuwa hana kundi lolote huku mwingine akitajwa kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa UWT na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Killango Malecela.

Kwa upande wa UVCCM, Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kura 483 na makamu wake, Mboni Muhita pia wanatajwa kuwa wafuasi wa kambi ya Lowassa.

Waliotwaa ujumbe wa NEC na ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja huo, pia wanatajwa kuwa waumini wa kambi hiyo.

Hata hivyo, katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi uliokuwa wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili, waliokuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na masilahi na makundi huku Martha Mlata akikataa kuzungumzia uchaguzi huo.

Mambo mengine ni ya kipumbavu kabisa, umekoswa kitu cha kupost mpaka ulete huyo Lowassa, aende tu, kwani akiugua sisi inatusaidia nini. kwanza ni kejeli kubwa ina maana Tanzania hakuna hospitali ya kumtibu? Shenzi kabisa.
 
Lile dongo la zzk kuhusu kwenda kutibiwa daily linamuhusu eh?
 
kaenda ku withdraw cash, chezea uchaguzi, lazima zilipungua.Huyu mtu ana account kila mahali
 
Ee mola mchukue hukohuko lakini si kama tutavyo sisi bali mapenzi yako yatimizwe, kwa jinsi alivyowanyonya watz anasitahili kuja kwako huko mbinguni umshughulikie hukou ameendelea kutumia fedha aliotuibia kutuhonga wenyewe yuaani anatukaanga kwa damu na mafuta yetu wenyewe. Rip EL.

Nina amini kwa dhati kabisa; Mungu huwa hapokei maombi ya jinsi hii. Usimuombee mabaya mwenzako Mkuu.
 
Back
Top Bottom