Lowassa aenda Ujerumani kwa matibabu

Lowassa aenda Ujerumani kwa matibabu

SIASA
Na Mwandishi Wetu (email the author)

Imetumwa Jumapili,Novemba4 2012 saa 9:22 AM

KWA UFUPI
Katika taarifa hiyo, alimsifu Rais Kikwete kuwa, kutokana na kutekeleza vizuri na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, wiki mbili zijazo wanaCCM watakwenda Dodoma kuidhihirishia dunia na Watanzania wenye shaka kwamba wanamwamini na kuuthamini uongozi wake.



Monduli

ALIYEKUWA Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa yupo nchini Ujerumani kwa matibabu na uchunguzi wa kiafya.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli jana hakuwapo katika uzinduzi wa mradi wa Barabara ya Minjingu hadi Arusha na shule jimboni kwake, uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete aliye ziarani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga na baadaye kusambazwa kwa waandishi wa habari, Lowassa alieleza kusikitishwa kutokuwapo jimboni kwake wakati huo ambao Rais Kikwete anatembelea jimbo lake.

Lowassa alisema kuwa, hali hiyo imetokana na kuwa safarini kwa ajili matibabu lakini akasema anaamini mambo yataenda vizuri si kwa ziara hiyo ya Rais Kikwete bali hata vikao vya juu vya CCM vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika taarifa hiyo, alimsifu Rais Kikwete kuwa, kutokana na kutekeleza vizuri na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, wiki mbili zijazo wanaCCM watakwenda Dodoma kuidhihirishia dunia na Watanzania wenye shaka kwamba wanamwamini na kuuthamini uongozi wake.

Katika maelezo hayo, Lowassa alieleza tatizo linalomsumbua kuwa ni macho, lakini pia atatumia nafasi hiyo kuchunguza afya yake.

Aidha, alimshukuru Rais Kikwete kwa kuzindua miradi hiyo akisema inadhihirisha mambo mawili makubwa aliyoyafanya kwa kiwango cha juu chini ya uongozi wake akiwa Rais wa Tanzania.

"Mosi, chini ya uongozi wako shule nyingi zaidi zimejengwa kuliko awamu zote zilizotangulia. Pili, kilomita za barabara za lami zilizoongezeka wakati wa awamu yako ni ndefu kuliko wakati mwingine wowote," alisema Lowassa na kuongeza:

"Kwa hakika umetekeleza vizuri, kikamilifu na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, mwaka 2005 na 2010. Sisi wanachama wa CCM na wananchi wa Monduli ni mashahidi wa jambo hili. Tunaamini ndivyo ilivyo kwa nchi nzima."

Mwishoni mwa wiki ijayo CCM itafanya uchaguzi mkuu wa uchaguzi ngazi ya taifa kuanzia mwenyekiti wa chama na viongozi wengine, ili kukamilisha kupanga safu mpya ya uongozi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015.

CCM ipo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ambapo tayari jumuiya zake za Wazazi, Vijana na Wanawake zimekamilisha chaguzi hizo, huku kambi ya Lowassa ikitajwa kuibuka kidedea kwa kunyakua nafasi mbalimbali zilizowaniwa, kuanzia ngazi za wilaya hadi jumuiya za chama kitaifa.

Katika uchaguzi wa UWT, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa, Sophia Simba ambaye alitetea nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa, huku wajumbe sita kati ya wanane waliochaguliwa kuwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambi hiyo.

Wajumbe sita kati ya wanane walioshinda nafasi za ujumbe wa NEC kupitia jumuiya hiyo wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa, huku mmoja akitajwa kuwa hana kundi lolote huku mwingine akitajwa kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa UWT na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Killango Malecela.

Kwa upande wa UVCCM, Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kura 483 na makamu wake, Mboni Muhita pia wanatajwa kuwa wafuasi wa kambi ya Lowassa.

Waliotwaa ujumbe wa NEC na ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja huo, pia wanatajwa kuwa waumini wa kambi hiyo.

Hata hivyo, katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi uliokuwa wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili, waliokuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na masilahi na makundi huku Martha Mlata akikataa kuzungumzia uchaguzi huo.

Rais Kikwete
Akizungumza katika hafla hiyo, Kikwete alisema kwamba ni lazima barabara zote ziwekwe matuta ili kuzuia ajali za barabarani, akieleza kuwa mara nyingi baada ya ujenzi wa barabara, kinachofuatia ni vifo vinavyotokana na tabia ya madereva wakorofi.


 
EL bado anasumbuliwa na macho?au ndio waliosema alipata minor stroke?kazi kweli kweli tunamuombea apate matibabu mazuri na arejee salama!tuombeane heri siasa si uadui!
 
Ufisadi mbaya sana. EL ameoana ajitambulishe kuwa anathamini sana kilometa za barabara na mashule kuwa mengi awamu ya nne bila kujali ubora wa huduma husika na gharama zake eti ndo uongozi bora nakujithaminisha kuwa ndo aina ya viongozi bora taifa linawahitaji na kwamba uchaguzi huu ujao wa magamba ni nuhimu sana kupata viongozi bora sampuli yake.
 
Du matatizo tayari au hayaishi?
mm KURA yangu 2015 kwenye Ballot Box waniwekee jiwe nitalipa V sio huyu EL au Dr labda nione Dovutwa au Mziray
 
Hawa wanasiasa ni wazee umri unakimbia sana kwa sasa maradhi hayakosekani hasa sababu ya stress.....
 
Mungu mponye na umpe roho yakutosheka kwa kila kitu
 
...afya imeishakuwa tia-maji tia-maji kutokana na dua mbaya za watanzania kwa mafisadi...
 
Jamaa kuchekiwa macho tu anaenda Ujerumani kwani CCBRT hapajui? viongozi wetu bwana badala ya kutufundisha uzalendo wa kuthamini vya kwetu ndio kwanza wanavizarau na kutukuza vya wengine, poa lakini namtakia safari njema na afya tele aende arudi aendeleze mapambano ya kukivuruga chama.
Hata mie nashangaa macho tu aende Ujerumani? Anamengine.
 
Najua kuna wengi wanangoja kuandika RIP Lowassa. Maana asivyopendwa humu JF sitashangaa kuona watu wakinoa peni zao kuandikia RIP Edward Ngoyayi Lowassa aka Richmond. Baba yenu namuombea aende salama na afike salama hata kutangulia salama ikiwezekana.
 
Subirini msemaji wake wa JF aje atuambie anaumwa nini.

cc: Pasco wa JF
Mkuu Mzawa halisi, mimi sio msemaji wa EL!. Mimi ni mshabiki wake tuu, ila msemaji wake rasmi pia ni member humu jf!.

I has just happened niko hapa Dodoma na by chance niko na msemaji wake rasmi!.

Ni kweli El kaenda Ujerumani for medical check up ya jicho lake. Kwa msiojua, Wajerumani ndio mabingwa wa sayansi ya tiba duniani!. Tatizo lao ni very expensive!. India ndio the cheapest kwa matibabu tatizo lao ni walipuaji!.

El kama M/K wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, uwepo wake Ujerumani pia ni muhimu kimipango mkakati wa ulinzi!.

Kufuatia hali tete ya Ziwa Nyasa, kuna uwezekano wananchi wote wa kando ya ziwa Nyasa wakapatiwa Buretta, Brownies na Smith& Wesson ambazo zinatengenezwa Ujerumani.
P.
 
Last edited by a moderator:
Fisadi EL hana aibu yaani kweli atakuwa na uwezo wa kutuhonga watz wote ili tumchague awe pres.? Haya
 
Sorry Hii Sii Kweli!.
CCM itashinda tena 2015 kwa sababu zile zile zilizoifanya CCM ishinde chaguzi zilizotangulia kwa ku capitalize on Tanzanians ignorance!.

Chadema kupitia M4C are doing "the right thing" kuwaelimisha Watanzania maovu na mapungufu ya CCM!. Ili kupata kura za kutosha 2015, doing the right thing alone is not enough!, they got to "do things right" kwa kuwapatia Watanzania solid reasons to vote in CDM!. Lazima kijipambanue kitafanya nini tofauti na CCM!.

Hivyo 2015 CCM itashinda tena sio kwa sababu inapendwa sana!. No!. Itashinda kwa mtindo wa "zimwi likujualo!" kwa sababu mpaka sasa hakuna mbadala!.
P.
 
Itashinda kwa kuiba kura kama walivyofanya 2010 wakishirikiana na vyombo vya dola Polisi, FFU na JWTZ na si kwa sababu ya zimwi likujualo...Kwa kipi walichokifanya miaka yote hii? Malalamiko ya wananchi kutoridhika na utendaji wa Serikali hii dhalimu yapo kila kona ya nchi. Kama uchaguzi utakuwa free and fair na kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi ambayo haitakuwa tayari kuchakachua matokeo ya uchaguzi na kuwaachia magamba watoe rushwa za aina mbali mbali ili kuwanunua wapiga kura kamwe magamba hawawezi kushinda.

Sorry Hii Sii Kweli!.
CCM itashinda tena 2015 kwa sababu zile zile zilizoifanya CCM ishinde chaguzi zilizotangulia kwa ku capitalize on Tanzanians ignorance!.

Chadema kupitia M4C are doing "the right thing" kuwaelimisha Watanzania maovu na mapungufu ya CCM!. Ili kupata kura za kutosha 2015, doing the right thing alone is not enough!, they got to "do things right" kwa kuwapatia Watanzania solid reasons to vote in CDM!. Lazima kijipambanue kitafanya nini tofauti na CCM!.

Hivyo 2015 CCM itashinda tena sio kwa sababu inapendwa sana!. No!. Itashinda kwa mtindo wa "zimwi likujualo!" kwa sababu mpaka sasa hakuna mbadala!.
P.
 
Nashindwa kuelewa CCM wanapojisifia kwa kujenga shule na barabara katika awamu hii ya nne. Je walitegemea ni nani aje ajenge hizo barabara na shule? Wananikumbusha baba mzazi anaejisifia kwa kuwalisha na kuwasomesha watoto wake wa kuwazaa, je alitegemea jirani ndio aje afanye hivyo? Na nafasi yake kama baba itakuwa ni kufanya nini?

CCm lazima ifikie sehemu ibadilishe hali ya MTanzania wa kawaida sio kujisifia kwa kutimiza wajibu wake. Kodi zetu ndizo zinazofanya kazi sio weledi wa Rais Kikwete au Ilani za CCM.

Huo mimi nauita upumba vu mtupu na kujilisha upepo.
 
Unajua bro hiyo stroke au problems zinazomuanda EL ni kama setback fulani ambayo au kwa msemo wa pwani mtenda hutendewa.
 
stroke imehamia machoni,too dangerous

si ndio hapo....eti anaumwa macho...anafikiri hatujui kinachomsibu...si tunamsikiliza tu na uongo wake...akishinda urais huyu bwana itabidi hiyo hospital iwe na chumba maalum cha Rais wetu maana karibia kila mwezi atakua huko na atakua analipiwa gharama zote na walipa kodi...tutakua tumemalizana na mpiga safari za nje mmoja na kumkaribisha mpira safari za nje mwingine
 
Huyo ndo mnataka kumpa nchi? Jicho tu ulaya, pesa ya mtanzania si itaishia kwenye matibabu ya ikulu?
 
Back
Top Bottom