Njia mojawapo ya kumpa umaarufu mtu ni kumsemasema na kufuatilia kila anachokifanya na kukiripoti. Ukifuatilia utaona hakuna siku ambayo imepita bila kupost EL. Kwa mtazamo wangu huku ni kumpa mtu umaarufu hata kama sio post za kumsifia. Kweli EL ni maarufu ila kweli amezidi kuwa maarufu sana hapa jamvini, na sisi wenyewe ndio tunachangia hilo kwa njia moja au nyingine. Kwani tusipomuongelea kabisa itakuwaje? Anyway nawapongeza wana kampeni wa EL, mpaka sasa mmefanikiwa kutufanya tuendelee kumuandika huyu Bwana, naona itafikia wakati tutaanza kufuatilia Chai yake anaweka vijiko vingapi vya sukari....kaenda msalani mara ngapi.....haja ndogo au kubwa n.k....Hata kama ni kiongozi Afya ya mtu ni siri kati ya yeye na D.k wake na watu wake wa karibu kama akipenda kuwaambia. Yeye mwenyewe atatuambia anaumwa nini pale atapoona inafaa, na kama ni ugonjwa usiotibika...hauna siri unapofikia hatua mbaya....utajulikana tu...tumwache baba wa watu ajiuguze na sisi tuendelee na kazi nyingine......ingawa kwa wengine inawezekana kumsema EL kila siku ndio kazi yenyewe....