Lowassa adaiwa kutaka kuuawa!

Lowassa adaiwa kutaka kuuawa!

Wakuu heshima mbele, kwenye magazeti ya leo imefahamika kuwa Fredrick Lowassa mtoto mkubwa wa EL amereport kuwa UWT wana mpango wa kumuua baba yake kwa kile ambacho hakijawekwa bayana!

Kama ada wanajamvi kwa weledi, tunapenda kujua kimetokea nini ghafla hivyo au ni kujihami baada kushukiwa na kuwalisha sumu baadhi ya wapambanaji wa ufisadi?

Nawasilisha
Skills4Ever, update thread yako kwa post hii!
#112
 
Mwakiembe anataka kujibu mapigo? Ok wapi jkey?

Pengine inaweza kuwa kweli kwani naye Mwakyembe inasemekana ni mtu wa huko huko UWT, kwahiyo wanajuana mbinu zao lakini wanazidiana maarifa!!
 
DIRA YA MTANZANIA

ISSN 1821 – 641 TOLEO NO. 141 JUMATATU DESEMBA 19-21. 2011 BEI T.SH 500 KSH.80 USH.800

SIRI YA KUMUUA LOWASSA YAFICHUKA
· Mwanaye ahamaki, abugia kilevi, ashambulia usalama wa taifa
· Polisi wagwaya kumkamata, atoweka na kuzima simu yake ya kiganjani

Na Angela Kiwia

Siri ya kumuua Waziri Mkuu wa kwanza wa awamu ya nne aliyeondoka kwenye wadhifa huo baada ya kuhusishwa kweney kasha ya Richmond, Kapteni Edward Lowasaa, imefichulia. Aliyefichua siri hiyo ni mwanaye mkubwa wa kiume, Fred Lowassa ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alimshambulia kwa maneno makali mmoja wa maofisa usalama wa taifa mkoani Arusha, akimtuhumu kuwa ni mmoja wa watu wanaopanga njama za kumuua baba yake.

Taarifa zilizotufikia zimeelzea kuwa Fredo Lowassa ambaye wiki iliyopita alikuwa mkoani Arusha, alifikia Hotel ya Mount Meru akiwa na marafiki zake kadhaa kwa ajili ya kunywa pombe na kubadilishana mawazo.
Kwambba wakiwa hapo, mmoja wa maofisa usalama wa taifa mkoani hapo aliyetajwa kwa jina la Suleiman Mombo, naye aliingia katika hotel hiyo kwa lengo ambalo halijatajwa na kupita karibu na mahali ambapo Fred Lowassa na wenzake walikuwa wameketi wakifanya mazungumzo yaliyokuwa yakisindikizwa na unywaji wa kilevi.
Mashuhuda waliokuwa katika hoteli hiyo wamedokeza kuwa mara baada ya Mombo kuketi, Fred Lowassa alisimama na kumfuata alipokuwa na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku akimtuhumu kuwa ni mmoja ya wanausalama wanaopanga njama mbaya za kumuua baba yake.

"Fred alikutana na Mombo katika Hoteli ya Mount Meru, alikuwa na wenzake kadhaa wakipata kinywaji, Mombo naye alifika nadhani hakujua kam Fred alikuwa pale na alipoketi tu Fred alimfuata na kuanza kumtuhumu kuwa amepata taarifa kuwa jamaa ana mpango wa kumuua baba yake, Edward Lowassa. Watu walibaki wakiwa wameduwaa manake tuhuma hizo ni nzito", alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa wakati Mombo akituhumiwa kuhusika na njama hizo za mauaji alibaki akiwa ameduwaa lakini alipoona anazidi kushambuliwa kwa maneno makali aliamua kupiga simu polisi ili kupata msaada, ambapo haraka polisi walifika eneo hilo na kumchukua Fred Lowassa hadi kituoni ambako walimtaka aandike maelezo yake kuhusiana na tuhuma alizomuelekezea mombo. Wapasha habari wetu waliokuwa wakifuatilia sakata hilo kwa karibu wamedokeza zaidi kuwa Fred Lowassa hakuwa tayari kuandika maelezo kuhusiana na tuhuma alizomuelekezea Mombo na alipobanwa afanye hivyo aliangua kilio huku akiomba asamehewe kwa sababu kilichomsukuma kutoa thuma hizo ni kilevi kingi alichokuwa amekunywa.

"Polisi walitaka Fred aandike maelezo ambayo pia alitakiwa kuyatolea ufafanuzi ili jeshi liweze kutunza kumbukumbu dhidi ya tuhuma hizo na kuzifanyia kazi, lakini aligoma kabisa na alipobanwa aliangua kilio huku akidai kuwa ni pombe alizokunywa ndizo zilizosababisha amshambulie Mombo. Utetezi huo ulikubaliwa na polisi na kumtana kurejea kituoni hapo siku inayofuata."

"Kosa walilofanya polisi ni kumruhusu aondoke kwa makubaliano ya kurudi siku inayofuata ili kuandika maelezo akiwa hana kilevi, alipotoka hapo, alitoweka moja kwa moja na simu zake zote akazima", alieleza shuhuda mwingine wa tukio hilo.

Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kuondoka katika kituo cha polisi, Fred Lowassa alikwenda kujificha mahali pasipo julikana na kuzima simu zake zote kwa kuogopa suala la mauaji ya baba yake kuanza kuchunguzwa na vyombo vya usalama huku yeye akiwa shahidi namba moja na kwamba madai hayo aliyatoa pasipo kuwasiliana na Lowassa mwenyewe au watu wake wa karibu.

Hata hivyo, taarifa nyingine zinaeleza kuwa hivi sasa polisi mkoani Arusha wanahaha kuhakikisha taarifa za kuibuliwa mpango wa siri ya kumuua Lowassa hazivuji zaidi kwa kile kinachoelezwa kuwa Lowassa amekasirishwa na taarifa hizo kwa sababu zinaweza kuwa na athari mbaya kwake kisiasa.

"Kuna jitihada za kumaliza suala hilo ili taarifa zake zisitoke, inasemekana mzee wake amekasirishwa na taarifa hizo kwa sababu ni mbaya na hataki zikuzwe,hata hivyo hakuna polisi mwenye uwezo wa kumkamata Fred, anaogopwa sana hapa Arusha kutokana na jina la baba yake. Hivi ninavyokuambia kila anayeambiwa kwenda kumtafuta anagoma kwani hakuna wa kumgusa, hajarudi na wala hawajui alipo pamoja na kuwa Mombo kuwaambia anamuhitaji ili kupata maelezo yake, polisi wote wamenywea, alieleza mtoa habari wetu.

Jitihada za kumpata Fred kuzungumzia tuhuma hizo hazijafanikiwa kwa zaidi ya wiki moja sasa baada ya simu yake ya kiganjani kutopatikana na hata jitihada za kupata taarifa zake kutoka kwa watu wake wa karibu nazo zimeshindwa kuzaa matunda baada ya kueleza kuwa hawajui alipo na hawampati katika simu zake za kiganjani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikana kufahamu kwa kueleza kuwa hana taarifa zozote kuhusu madai mazito kama hayo kutolewa na Fred dhidi ya afisa usalama wa taifa.

Huku akionyesha kushangazwa na taarifa hizo alisema ndiyo kwanza anazisikia kutoka kwenye gazeti hili.
Wakati afabde Mpwapwa akikana kufahamu tukio hilo, Mombo amelithibitishia gazeti hili kuwa tayari amekwishatoa taarifa za tukio hilo la kushambuliwa kwa maneno makali na kutuhumiwa kupanga njama za mauaji dhidi ya waziri mkuu wa zamani, Lowassa, kwa polisiwa Arusha.

"Suala hili nililiwasilisha kwa kamanda wa polisi mkoa, hivyo yeye ndiye anaweza kukufafanulia ni hatua zipi zimechukuliwa mpaka sasa, ebu mtafute akwambie amefikia wapi kwani nilishatoa maelezo yangu polisi" alisema mombo.

Taarifa nyingine kutoka kwa watu walio karibu na familia ya Lowassa zimeelewa kuwa Fred lowass hakumshambulia kwa maneno makali Mombo bali alikwenda kueleza masikitiko yake kutokana na njama ovu za kumuua baba yake (Lowassa) zinazopangwa na wenzake.

"Hakukuwa na kurushiana maneno au kushambuliana kwa maneno, Fred na Mombo ni marafiki. Mombo akikwama kifedha huwa anapata msaada kwa Fred, sasa siku akiwa na taarifa mbaya dhidi ya Mombo alipomuona pale Mount Meru alimfuata na kumwambia wewe sio rafiki mzuri kwani licha ya kusaidiana katika shida na raha bado unashirikiana na watu wanaotaka kumuua baba yangu.

"Mombo alipotoka hapo, alikimbilia polisi na kufungua jarada, Fred akaanza kutafutwa lakini alikuwa amekwisharudi Dar. Alipigiwa simu na RCO akadokezwa kuwa amefunguliwa jarada na akamtaka afike kuandikisha maelezo yake. Baada ya hapo fred alimpigia Mombo na kumueleza masikitiko yake ya kulifikisha suala hilo walilokuwa wakiongea kirafiki polisi. Hapo ndipo akazima simu ili kujipanga", alisema mmoja wa watu waliokuwa karibu na familia ya Lowassa.

Aliongeza kuwa kilichofanywa na Mombo ni kumshughulikia Fred kupitia mtandao wa wanasiasa wanaohasimiana na baba yake kwa saabu suala hilo likifikishwa polisi na ushahidi kukosekana, atakuwa matatani.

Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kunzungumza na Lowassa mwenyewe hazikufanikiwa baada ya simu kuita mara kadhaa pasipo majibu.

***********
Nikipata nafasi ntawawekea:

DIRA LA TAREHE 22-25 Dec: TISHIO LA KUUWAWA LOWASSA😛OLISI WAFICHA SIRI - WAKATAA KUTOA TAARIFA ZA MWENENDO WA UCHUNGUZI;

DIRA DEC 26-28:TISHIO LA LOWASSA KUUWAWA: CCM YANAWA MIKONO:YASEMA SI JADI YAKE KUSUKANJAMA ZA MAUAJI: YAMTAKA FRED LOWASSA ATOE USHAHIDI WAKE:EDWARD SOKOINE, KOLIMBA WASIHUSISHWE.

Nawasilisha

Kumbe source ya yoote mtoto cheupe Freddy kazidiwa na pombe kabwabwaja na kushindwa ku back accusations? Au?

Fred ile scandal ya kununua nyumba kwa malaki ya pound Uingereza bila equivalent source of income uliimaliza vipi ?
 
Nape atuambie Ni nani aliwaua hawa?
  • Horace Kolimba
  • Edward Sokoine
  • Dr Nicas Mahinda
  • Abdallah Kassim Hanga
  • Sheikh Othman Shariff
  • Gibbons Mwaikambo
  • Ipyana Malecela
  • Immrani Kombe
  • Kigoma Malima
  • Julius Nyerere
  • Amina Chifupa

Wangwe alimuua nani?
Mgombea mwenza wa chadema alimuua nani?
 
Naona kuna mpango wa kumjenga Lowasa kisiasa, maana kila siku habari za kumhusu haziishi.
 
Edward Lowassa alikwenda Israel hadi kwa mchungaji emmanuel Joshua Nigeria ili aokoke na kashfa zinazomwandama na kutubu kumbe hakuiombea familia yake mwanaye kakutwa kwenye kilabu cha pombe akibweka kama mbwa asie na mwenyewe akaanza kuwabwekea Usalama wa Taifa, je kesho na kesho kutwa atambwekea nani?
 
Hii ni mbinu ya kuwatisha Usalama wa Taifa waogope kufutalia nyendo za huyu fisadi
 
Nisaidieni jamani! mimi sijaelewa vyema! ni sababu gani inayomfanya lowasa atake kuuwawa? kwani sisi tunaweza kumsaidiaje ili asitishe lengo lake la kutaka kuuwawa?amepanaga kuuwawa na nani? si atamlipa ghali ili afanikishe kazi hiyo? ila nadhani ufisadi wake nao ndio unamchanganya. kama mpo karibu mwaweza kumshauri aachana na mpango huo wa kutaka kuuwawa kwani sii mzuri utamgharimu kiukweli ingawa taifa litanufaika kwa kujiuwa kwakwe
 
Nisaidieni jamani! mimi sijaelewa vyema! ni sababu gani inayomfanya lowasa atake kuuwawa? kwani sisi tunaweza kumsaidiaje ili asitishe lengo lake la kutaka kuuwawa?amepanga kuuwawa na nani? si atamlipa ghali ili afanikishe kazi hiyo? ila nadhani ufisadi wake nao ndio unamchanganya. kama mpo karibu mwaweza kumshauri aachana na mpango huo wa kutaka kuuwawa kwani sii mzuri utamgharimu kiukweli ingawa taifa litanufaika kwa kujiuwa kwakwe
 
Tunapochangia mada lazima tuangalie mazingira ya tukio. Aliyeleta thread hii anasema ilitokea katika Hotel FL akiwa anapata kilevi!..... kwa hiyo ni wazi kuwa ni ulevi tu ndio unaomsumbua. UWT wamuue baba yake kwa lip? kama ni gamba alishagoma kulivua sasa yameanza maneno mengine.
 
Hii ni mbinu ya kuwatisha Usalama wa Taifa waogope kufutalia nyendo za huyu fisadi

Ni mbinu pia ya kumsafisha kuelekea nia yake ya kutaka kugombea Urais Mwaka 2015. Sasa kutuhumu vyombo vya Usalama si njia sahihi, huyo mtoto wake atumie njia zingine ziko nyingi tu ikiwemo aliyotumia baba yake ya kumgeukia Mwenyekiti wake kwamba suala la Richmond analijua na kumtaka awachukulie hatua wana CCM wanaomtuhumu kuwa yeye ni fisadi.
 
Jamani eeh yule Dictator wa kikwele,mzee wa double standard haaminik.i
 
alimuumbua jk kwenye kikao cha NEC kuwa ni fisadi wa richmond,..unafikiri mzee wa visasi atamwacha?mwakyembe and lowassa are now on the same boat,..m.kwe.re amewaweka kwenye target ready to shoot..
 
"Polisi walitaka Fred aandike maelezo ambayo pia alitakiwa kuyatolea ufafanuzi ili jeshi liweze kutunza kumbukumbu dhidi ya tuhuma hizo na kuzifanyia kazi, lakini aligoma kabisa na alipobanwa aliangua kilio huku akidai kuwa ni pombe alizokunywa ndizo zilizosababisha amshambulie Mombo. Utetezi huo ulikubaliwa na polisi na kumtana kurejea kituoni hapo siku inayofuata."

Nimesema awali ni ulevi tu unamsumbua huyu hata hivyo Polisi wanatakiwa kuchukua hatua dhidi yake na kuhakikisha Afisa wa UWT anakuwa salama pia dhidi ya vitisho vya FEL.
 
Hii ni tactic ya kujitoa uhusika wake katika matukio ya unyweshaji sumu wenzake. Hapa haijalishi alihusika au hakuhusika.
 
Ndani ya CCM huwa hakuna kupoteza sifa ikipotea inanunuliwa.

Mkuu naheshimu maoni yako, kwa bahati mbaya ni maoni yanayopitwa na wakati.
Ifikapo 2015 tutaongozwa na Katiba mpya, ni wajibu wa kila Mtanzania akiwamo mimi na wewe kuhakikisha kuwa Haitoi Mwanya Kwa hata Kibaka wa Mtaani wacha Majizi yenye Mapembe kusogelea hata fomu ya Ugombea. Wakati wa kuendekeza Umasikini Tonge unafikia mwisho, Elimisha Familia na Jirani zako.

 
Back
Top Bottom