Lowaasa Aiteka Zanzibar Xmass

Lowaasa Aiteka Zanzibar Xmass

Huyu fisadi mbona yuko kimya kuhusana na wizi wa zaidi ya shilingi bilioni mia tatu katika bank account ya Escrow? Je, anakubaliana na maamuzi ya DHAIFU au hakubaliani nayo? Je, anataka pesa zote zirudishwe hazina na wahusika wapandishwe kizimbani au la? Mtu anataka kuwa Rais ndani ya miezi 10 ijayo lakini kwenye issue nzito za Kitaifa anakuwa kimya kabisa akijaribu kuzikwepa kwa kila namna badala ya kutaka kuonyesha kama yuko tayari kutetea maslahi ya Watanzania, pale ambapo kuna wahuni na wezi wamejitajirisha, bila kujali nani ni muhusika. Ukimya wake kwenye hili sakata ni dalili nyingine huyu hafai kuwepa dhamana na Watanzania ya kuiongoza nchi.
 
Huyu jamaa hatufai watanzania ana historia chafu.hatuwezi kumkabidhi ikulu atashindwa kuwaonea haya marafiki zake.
 
Huyu ndie Raisi wetu ajaye, sauti ya Umma ni sauti ya Mungu! EL maombi yake yamepokelewa mbinguni. Kilicho baki ni muda tu ufike tumuingize Ikulu.
 
Kwa kuitazama hii picha, utakubaliana na mimi jamaa ni still going strong!, kazi ya urais sio kubeba zege!, kitu kizito kabisa ambacho rais anapaswa kuwa na uwezo wa kukibeba ni microphone kama hapo!, tena only pale inapobidi!.

Nimeisha mshauri yule 'Salva' wa EL, jamaa akiingia ni vihotuba vifupi vifupi maximum 3 pages only na sio mijihutuba mirefu very boring kama ya JK!, tena sio kwenye mijikaratasi, EL akiingia anaingia na ECO Government na E-Government, kwa sera ya paperless!, mambo ni kwenye I pad air, na transparent teleprompters kama Obama!.

Merry X-Mass

Pasco
Pasco anatafuta ugali wake kwa nguvu zote.

unikumbuke ufikapo peponi.
 
Last edited by a moderator:
Si bure wewe utakuwa umeahidiwa wizara ya gesi zetu kwenye ufalme wa Edo kama utatokea.

Pasco[/QUOTE]
 
He is building a winning coalition across the country. Keep up our next president
 
Pasco umeahidiwa wizara ya gesi zetu katika ufalme wa EL (kama utakuwepo) si bure mwanaume wewe uache kunywa mbege leo Xmas unamfagilia EL.
 
Mimi sijaona haja wala umuhimu wa sherehe hizi za KIKAFIRI kusherehekewa nchi ya Kiisilamu ya ZANZIBAR.
 
Sasa inadhihilika kwamba dini ni utapeli ambao ulitengenezwa enzi hizo na wazungu/waarabu ili waweze kumiliki lasilimali watu ona sasa kanisa linavyomthamini mtu mwenye pesa haramu,makanisa ya leo yanajitaid kukumbatia mtu et sababu ana hela nakumkabidhi dhabahu atambe atakavyo alafu ambae ni mchungaji kanywea kama kamwagiwa maji ya barid ni ujinga mnadharirisha makanisa yenu acheni ushamba na uvivu,iko cku mtakuwa mnasli na hawo wenye vijipesa haramu na ndio maana muamko wa watu kwenda kwenye nyumba za ibada zinashuka @cku
 
Alafu naye mhuni tu. Angalia shati hapo kifuani kaacha kifua wazi ka wahuni wa bongo fleva mh Tanganyika tuna safari ndefu ati huyu naye aje awe rais makubwaa

mpambanaji anasikia Joto
 
Sasa inadhihilika kwamba dini ni utapeli ambao ulitengenezwa enzi hizo na wazungu/waarabu ili waweze kumiliki lasilimali watu ona sasa kanisa linavyomthamini mtu mwenye pesa haramu,makanisa ya leo yanajitaid kukumbatia mtu et sababu ana hela nakumkabidhi dhabahu atambe atakavyo alafu ambae ni mchungaji kanywea kama kamwagiwa maji ya barid ni ujinga mnadharirisha makanisa yenu acheni ushamba na uvivu,iko cku mtakuwa mnasli na hawo wenye vijipesa haramu na ndio maana muamko wa watu kwenda kwenye nyumba za ibada zinashuka @cku

Mkuu, wenye afya hawamuhitaji daktari wagonjwa. Kanisa ni nyumba ya wote, wenye mioyo safi kwa ajili ya kumtukuza Mungu, na wenye dhambi kwa ajili ya kutubu.
Nyumba ya Mungu huwa haina ubaguzi. Haya ni kwa mujibu wa mafundisho sio matakwa ya mtu yeyote kwa sababu zozote.
Halafu, hivi hatuwezi kujadili masuala ya imani bila kubeza au kudharau imani za wengine? Hakuna dini iliyo duniani kwa bahati mbaya ndugu yangu, tujifunze kujadili bila kuparulana, tutalipa heshima kubwa jukwaa hili.
Mwisho, nakutakia kila la kheri katika mabadiliko yako.
Ova
 
Mpe Lowasa sifa zake kama inavyostahili kama ifuatavyo:
Mheshimiwa, Raisi mtarajiwa, Waziriri mkuu mtaafu, mbunge wa Monduli Edward Lowasa.
 
Halafu sijaonankaitekaje Zanzibar! Ushabiki mwngine bwana! ni ugonjwa kabisa
 
Mpe Lowasa sifa zake kama inavyostahili kama ifuatavyo:
Mheshimiwa, Raisi mtarajiwa, Waziriri mkuu mtaafu, mbunge wa Monduli Edward Lowasa.
Umesahau moja

Mheshimiwa, Raisi mtarajiwa anaetegemewa sana!,
Waziri Mkuu Mstaafu mchapakazi,
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama!,
(Berinado, Othmano, Edisono, Erenesto, wako chini yake!)
Mbunge wa Monduli aliyepita bila kupingwa!
Mhe. Edward Ngoyayi Ole Lowasa

Mkuu Pasco,
Nimesoma posts zako za leo, kuanzia kule kwenye uzi wako kuhusu 'Rais na GPA' na kwa vile Leo X mass, inaonyesha uko High Mkuu, posts zako za Leo Ziko chini ya kiwango, sio za Pasco nilliemzoea hapa jamvini, .. Bora ungepumzika tu kwa Leo Mkuu.

Merry X mass
 
Waziri mkuu aliyestaafishwa kwa lazima kwa ufisadi akapata na stroke. Anavotumia mijihela kuingia ikulu...tumuogope kama ukoma. Wote wanaompigia chepuo humu wamelipwa ..ni njaa tuu za watanzania. Call a spade a spade sio kijiko kikubwa. Lowasa ni fisadi hatufai ikulu ..fedha anazotumia kugawa mpaka sasa nimabilioni anazitoa wapi? Kinanani friends of lowasa? For what purpose is this friendship based? Wizi mtupu na Nyerere alishatuonya tusije watanzania tukafanya makosa tuliyofanya kwa JK. Wote hao ni jamii moja MaFISADi
 
Back
Top Bottom