Captain-Chui
Member
- Dec 11, 2014
- 80
- 49
Sisi tunapima tu upepo, na kuripoti mwelekeo wa upepo. Mpende usimpende, pamoja na madhambi yake, pamoja na uzuri wake, Watanzania wengi wanamtaka Lowassa kuwa raisi 2015. Sasa kama wewe unabisha sema ni nani anamkaribia Lowassa hata kwa mbali. Na tunavyoelekea 2015 ndio mwelekeo wa upepo utakavyokuwa dhahiri. Mimi binafsi ningependa Mwakyembe awe raisi 2015. Lakini ndio hivyo, upepo haupo kwa Mwakyembe, yaani Mwakyembe hayupo kabisa kwenye picha.