LNG Project: Njooni tujadili unadhani kwanini mradi wa gesi ya LNG unachelewa na nini chakufanya ili utekelezwe kwa wakati

Humu utaona watu wanafiki wanajifanya conscious ,bila hao jamaa hata huo mpango tusingekuwa nao.

Kama tumeshindwa kuja na idea ya kufanyia kazi ,bora kuwapa kupata chochote kuliko kukalia uchumi.

Hata hayo madini hapa bongo unamuuzia nan ? Wapeni tu wafanyie kazi ,sisi tuendelee kufanya siasa za wizi.
 
Twende polepole; LNG ni gesi asilia ambayo imekuwa-cooled hadi kubadilika kuwa kimiminika kwa kufanya hivyo nyingi inaweza kukaa kwenye container ndogo....; Kwahio kwa nchi kama Japan n.k. ambazo zina uhaba wa nishati na ni vigumu kuweka mabomba kutokea source mpaka destination ni rahisi ku-cool gesi asilia na kuisafirisha kwenye mameli tankers mpaka destination na ukifika huko kuitumia accordingly...

Kwahio kwa soko la ndani hakuna umuhimu wowote wa kuwa na LNG (Piped ni cheaper kwa kupikia) Tena umeme ni cheaper zaidi kama tukitumia akili kwa Tanzania; lakini kwa kuendesha magari n.k. Compressed ndio mpango mzima...; Soko la LNG ni Japan na China ambao wana tumia sana nishati hivyo wakiachana na Coal inabidi wahamie sehemu nyingine....

My two cents badala ya kuwaza tu kufanya ili tuuze tungewaza pia kutumia ili tupunguze gharama (CNG kwenye Magari) Piped mpaka kwenye Electric Generation ili umeme uzambazwe watu wapikie umeme
 
Tulitakiwa kuanza utekelezaji hata kabla ya Mozambique.
Nakiri kwamba sina kielelezo :
Kuna viashiria vya hujuma na harakati za kukwamisha miradi zinazoongozwa na taifa flani la Gulf ... tumbonomics za watu flani hapa kwetu weshavuta cha kwao ... nyingi mno ... nasikia, ili kufanikisha hilo.
 
Wachangiaji tunaomba mawazo yenu. Njooni huku huu ni mjadala huru.
Mkuu, according to Wikipedia inaonekana kuna sehemu bado makubaliano hayajafikiwa kati ya serikali na wawekezaji.
Pia isitoshe mazungumzo yalianza awamu ya tano chini ya waziri Kalemani. Samia nae akaja na mawaziri wake pengine wakaona kuna vipengele havipo sawa wakaamua warudi mezani kuplan upya kutokana na ukubwa wa project.
Nadhani ni vyema kutokukurupuka na kuingia kwenye mikataba mibovu eti kisa tu Msumbiji wameingia, we still have time.
Let's learn from our past mistakes.
 
Mkuu, according to Wikipedia inaonekana kuna sehemu bado makubaliano hayajafikiwa kati ya serikali na wawekezaji.
Pia isitoshe mazungumzo yalianza awamu ya tano chini ya waziri Kalemani. Samia nae akaja na mawaziri wake pengine wakaona kuna vipengele havipo sawa wakaamua warudi mezani kuplan upya kutokana na ukubwa wa project.
Nadhani ni vyema kutokukurupuka na kuingia kwenye mikataba mibovu eti kisa tu Msumbiji wameingia, we still have time.
Let's learn from our past mistakes.
Mkuu umeeleza vyema sana. Sasa nini kifanyike.
 
Nani kakuambia kuwa mradi unachelewa?
Kwa experience yangu, masuala yanayohitajia kufikiri kama hili, hayapati wachangiaji wengi. Na mtu akichangia huwa ni hivyo- 'nani kakuambia kuwa mradi unachelewa?' aina hiyo. Watanzania tuna tatizo kubwa ndugu yangu. Suala kama hili lingetolewa kwenye forum za Uganda au Kenya vile....lingejadiliwa hata kwa siku kumi. Hapa anzisha uzi wa nani kafanya nini, timu gani inakwenda wapi, Samia ni mzuri si mzuri?........nk!
 
Mkuu umeeleza vyema sana. Sasa nini kifanyike.
Time is not on our side. Mradi wa 41b hata ukiwa mbovuTanzania itafaidika sana. fikiria out of box: ajira, wageni, training, na vitu chungu nzima. Hawa negotiators wetu wataka fixed percentage tu ndicho wanachokijua. Hakuna mtu atakayekupa 41 b halafu asione kama anazirudisha. Na Tanzania ni 'a high risk country' kutokana na mabadiliko ya siasa, uvunjaji wa mikataba....etc, watu wanaangalia hayo.
Aidha wakubali au mradi usifanyike kabisaaa.
 
Nani kakuambia kuwa mradi unachelewa?


Kuna vitu viwili

1. Rushwa hizi kampuni hazitaki kutoa maana kwenye nchi zao wanapigwa mafaini makubwa kwa rushwa. Na kampuni za Marekani wana CIA kabisa
2. Kuna wanasiasa wanatafuta namna ya kulwa rushwa kinamna na familia ya mzee wa Msoga nayo ipo ndani.

Ndiyo maana Mama naye watu wake wanataka kutafuta njia ndiyo maana wamemtema Matarajio pale TPDC
 
Back
Top Bottom