Kwanini Marekani imetoka hadharani kuutaka Mradi wa gesi wa Kusini? Kwanini wanatishia kwamba tukizubaa hakuna mwekezaji atajitokeza tena?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Majasusi wa Marekani wameanza kutumia vyombo vya habari kuitisha Tanzania kuhusu Mradi mkubwa gesi huko Kusini.

Makampuni haya makubwa yanalazimisha tuanze utekelezaji wakati huo kama kawaida sisi inaonekana tulikwenda kuwaita ila tulikuwa hatuajajiandaa. Wao wamefika na baada ya kuona wanasiasa wetu na wataalamu wanataka kushtuka wameanza kutumia mashinikizo ya vyombo vya habari wakidai gesi imetapakaa duniani hivyo tukigoma wawekezaji wataondoka na hawatarudi tena.

Swali la kujiuliza, kuna ulazima wa CCM kubinafsisha kila rasilimali tuliyonayo? Kwanini wasiache baadhi kwa kizazi kijacho? Miaka sitini bila kuuza gesi tumewahi kufa kwa njaa? Niwaombe Serikali na CCM wawaachie wajukuu zetu japo rasilimali kidogo. Siyo vizuri kuwa na utawala wakuuza kila tulichopewa na Mungu.

Nchi zote za Ulaya na Asia zilizoendelea ziliwekeza kwenda kuvuna nje siyo kuuza rasilimali za ndani. Sisi kujenga barabara imetulazimu kuuza madini yote na gesi. Tujaribu kuwa wavumilivu. TUSIWEKEZE KUUZA KILA KITU NDUGU ZANGU.

Tusitishwe na maneno yao hawa majasusi, kama wanaamini gesi imetapakaa duniani kote tuwaache wakachimbe huko kwingine kwetu tutachimba wenyewe miaka 50 ijayo.
 
Kuna watanzania wa mwaka 3200 wanatakiwa kuzikuta hizi rasilimali wazitumie pia.
Una uhakika wakati huo kutakuwa na matumizi ya gas? Miradi hii inatakiwa itekelezwe ili vijana wapate ajira, kisha tuondokane na huu uchumi wa rasilimali, tuanze uchumi wa viwanda na biashara tupu
 
Back
Top Bottom