Jifunze kuhusu Liver Bird
Nikuwa nafikiri yule ndege wa Liverpool ni secretary bird kumbe siyo, bali ni ndege 'imaginary' aliyetungwa tu na wanaliverpool wa zamani kama huku bongo tulivyo na vibwengo.
Cha kwanza, utamkwaji wa neno 'Liver' hapa ni kama utamkavyo 'driver' na siyo kama utamkavyo 'river'.
Kuna masanamu mawili ya hawa ndege juu ya jengo la Liver (the Liver building), jijini liverpool. Wametengenezwa kwa Bronze (shaba). Yule ndege wa kike (anaitwa Bella) anatazama baharini, akihakikisha anaongoza mabaharia waende na wafike salama katika safari zao za baharini. Yule wa kiume (anaitwa Bertie) anaangalia jiji la Liverpool, akiangalia usalama wa wake za mabaharia na kuhakikisha vilabu vya pombe havifungwi.
Kwenye hayo masanamu utaona kama ndege hao wameshikiliwa na kamba ili wasiruke na kutoroka na pia hawaangaliani. Sababu ni kwamba inaaminika kwamba wakiweza kupandana na kuruka, jiji la Liverpool litatoweka nao, au pia kwamba ndege hao wakiruka, mto Mersey utafurika 'enzi za Nuhu-style' na kumeza jiji na kila kiumbe hai kilichomo.
Pia Liverpudians wanaamini kuwa plae mwanamke mtakatifu wa kweli, asiye na doa kabisa (a truly pure woman), akipita kati ya ndege hao, basi watageuka kutoka kuwa wa chuma na kuwa hai. Kitu ambacho kamwe hakiwezi kutokea. Huu ni utani wa Liverpudians kuwa wanawake watakatifu au 'wasafi' hawajawahi kuwepo, hawapo na hawatakuja kutokea.
Sijajua hilo jani midomoni mwao ni nini ila ni rahisi kufikiria kuwa ni mirungi, au bangi mbichi, maana tabia za mashabiki wa Liverpool wenyewe mnazijua.