Do you think trent will be converted to a RM?
I watched him vs Westham again yesterday, tracking back has been a problem for him now
Mkuu, its tempting, kutokana na traits alizonazo Trent, ana kila aina ya tactical trait ya kucheza as RM in a 442
- Chance(s) creating merchant
- World Class Passer
- Standard & effective Pace
- Strong ball carrier
- World Class Vision (Line breaker)
- etc
Traits zote hizi anazimiliki Trent, but my worry ni kuwa he's so short of confidence now, for the past few years Trent alikuwa ame-improve a lot katika suala la ku-defend, though he had prime Wijnaldum, Henderson & Fabinho in the MF, so it was so easy kwa yeye ku-build, kujifunza na kujiimarisha zaidi katika kuzuia, last season ambayo imeisha few months ago, alikuwa ni one of the top DEFENDERS in the world, na alikuwa ni one of our most consistent player throughout the season, hence amemaliza nafasi ya 22 kwenye BDO rankings, so hii bad patch anayopitia sasa ni ya muda tu, huwa inatokea kwa kila mchezaji, tumeshuhudia kwa kina Salah, Mane, Robertson, Firmino, Matip, VVD, Fabinho etc, tena Fabinho now is really struggling na hii siyo mara ya kwanza kwa Fabinho, so kama ni real football fan, huwezi kupata shida kuhusu hili, though huwa tunaombea tu hizi bad patches zisiwe zinatokea kwa wachezaji muhimu sana, na ukiangalia, ukiachana na Trent kuwa out of form, ni wazi kuwa shape tuliyoanza nayo msimu huu ilikuwa haimpi uhuru au kuwa comfortable (tumeelezea sana), it happens.
He was good in a 442 against rangers, na pia he was good in a 442 against Westham kwenye kipindi cha kwanza, though alitoka mchezoni tena baada ya sub ya Thiago & Nunez kwenye dakika ya 60, as Klopp reverted back to 433 na tukapoteza control yote ya game.
So its up to Klopp, kuangalia anaweza kumrudisha vipi kwenye form, ku-change set up na formation ni good start.
Mkuu, naona kwa Trent kucheza as RM, tutahitaji two good & strong defenders on our RHS, ili kutoa burden kwa Trent ya ku-defend na kucheza as a free creator from the right side, so utamuhitaji Gomez at RB na Konate at RCB, both ni strong & pacey defenders na good katika counter-pressing, so maybe, i mean MAYBE, akirudi Konate, Klopp anaweza kuwa tempted.
But for the meantime, OX amerudi, RM is his bread & butter, kama unavyojua a fit and firing OX is our best RCM, he knows how to play that right side, ana attribute zote za ku-shine at RM, and for the first time in a long period tunacheza mfumo ambao unam-favour to a tea, so i pray Klopp, alione hili, kumchezesha OX at RM, kutabadilisha msimu wetu wote, because that is his position, problem ni kuwa he got frozen out last season, so hatujui kama uhusiano wake na Klopp umerudi kuwa sawa, maana last season uliharibika. But its time kuweka personal feelings pembeni na kujaribu kurudisha msimu on the track, play Ox at RM and Carvalho at LM in a 442, and we will cruise games.
Trent should stay at RB, he has a legacy to proctect & build, we need to support him now, its the first time in his career anaingia kwenye bad patch, na pia bado hana uhakika wa kwenda WC, so hayupo good mentally, unajua dogo kakulia maisha marahisi sana, hajapata rabsha zozote, kakulia kwenye LFC academy, kakulia kwenye family inayojiweza, he's making a lot of money now but bado anakaa kwa wazazi, free time yake anatumia ku-DM kila mwanamke instagram, and funny thing is, you cant fault him, he's human afterall, na he's turning 24 soon, wote tumefanya stupid mistakes tukiwa around hiyo age, so its not suprising, na ule umayai wake unafanya iwe ngumu zaidi kukabiliana na bad patch yake because kila pundit, rival fans, jornos etc wapo on his ears, and on top of all, Southgate dissed him hadharani (kwenye media), so he's struggling mentally, tofauti na kina Fabinho ambao wamekulia favela, dangerous and rough places ni kama useme Manzese au Buguruni ya Bongo, so ni lazima atakuwa strong sana mentally, hawezi kuwa phased out na small bad patches, same kwa Firmino, same kwa Nunez, Diaz, Mane, Salah, Keita etc, ambao they had to rise, they had to dig deeper ili kutoka kwenye slums, kutoka kwenye kucheza peku, kutokuwa na hela ya gozi, hela ya nauli ya kwenda uwanjani, hela ya viatu, hela ya nguo, kushindia mlo mmoja, kulala chumba kimoja na dada & brothers, etc, mpaka kufika Anfield, Liverpool, so hawawezi kuwa phased na stupid jornos, stupid pundits, stupid LFC & rival fans, VVD alikuwa anaosha masufuria, sahani etc kwenye migahawa, Robertson was at one point jobless, na ana relegation on his football CV, huwezi kum-phase au kumtingisha akiwa na bad patch, so Trent kalelewa tofauti na hata kupokea negative reaction inakuwa ni ngumu sana kwake ku-process.
So acha tumlee kimayai, tumpe muda, ana watu kwenye dressing room ambao watamsaidia, kina Thiago, Alisson, VVD and Uncle Milner, so i think atarudi, na mimi siku zote huwa sikatii tamaa TALENTS, kwasababu ni moja tu, they will always PROVE you wrong.