Hivi bill shankly alipomkabidhi timu Bob paisley , alimkabidhi kama assistant wake au Bob paisley kuna timu alikuwa anafundisha ndio akapewa liverpool?
Na vip kuhusu Joe (Joseph) Fagan
Unajua Shankly alistukuza sana kustaafu kwake mwaka 1974 na klabu haikua na plan B ya hapo kwa hapo na kwa vile tangu Shakily anateuliwa kua kocha wa Liverpool mwaka 1959 alimteua Paisley kama msaidizi wake basi uongozi ukaona kumpa hio kazi mwaka 1974 itakua ni mwedelezo Wa yale mazuri aliyokua anafanya Shankly...
Shankly alimkuta Paisley Liverpool akiwemo na Fagan na hapo hapo wakaanza kazi maridadi kabisa kujenga kikosi..
Bob Paisley alikua pia ni daktari Wa viungo pale Liverpool kazi yake ya kwanza baada ya kustaafu soka, inasemekana Kwa kuangalia tu mchezaji bila hata kupima aliweza kujua nini kinamsubua. Kazi hii hakwenda chuo mbali alijifundisha mwenyewe.
Bob Paisley alijiunga Liverpool mwaka 1939 na alikuja kustaafu mwaka 1983. Aliitumikia Liverpool miaka 44. Alishinda mataji 20 ndani ya misimu 9 aliyodumu kama meneja.
Alikua ni real scouser mzaliwa Wa jiji la Liverpool, alifariki mwaka 1992.
Joseph Francis Fagan alijiunga na Liverpool mwaka 1958 kama kocha wa reserve team kazi aliyoifanya mpaka mwaka 1971, baada ya hapo alifanya kazi na kikosi cha kwanza mpaka 1974 alivyopandishwa rasmi kua kocha msaidizi Wa Bob Paisley.
Baada ya Bob Paisley kustaafu mwaka 1983 klabu iliona itumie mbinu ile ile ya kuedeleza aliyoifanya Paisley na wakampa kazi hio Joe Fagan.
Msimu wake Wa kwanza alishinda vikombe viatu League Championship, League Cup na European Cup.
Alistaafu mwaka 1985 japo alipanga kustaafu mwaka 1984 na hakushinda taji lolote msimu wake Wa mwisho ikiwa ni mara ya kwanza kwa Liverpool kutoshinda chochote ndani ya miaka 10. Baada ya Fagan klabu ikamteua kocha mchezaji King Kenny Dalglish mwaka 1985.
Tukio ambalo lilipelekea akumbwe na msongo Wa mawazo ni ile Fainali ya Ulaya kati ya Liverpool vs Juventus iliyochezwa uwanja Wa Heysel Ubelgiji na ikatokea ajali ukuta kuangukia mashabiki wengi wakiwa ni Wa Juventus. Baada ya ile ajali mechi ilichezwa na Juventus wakashinda moja bila goli akifunga Platini Kwa penati. Hili Tukio lilipelekea Liverpool kufungiwa kushiriki mashindano ya Uefa Kwa takribani miaka 6 na vilabu vingine Kwa Uingereza miaka 5.
Joe Fagan alikua ni scouser pia mzaliwa Wa Liverpool, aliitumikia Liverpool Kwa miaka 27. Alifariki mwaka 2001.