Siku zote Beki bora tunamjua uwezo wake kwa kumpokonya mpira adui inapotakikana kufanya hivyo, sikumbuki kama jamaa alishine siku hiyo
Shuleni tulifundiswa kuwa unapotoa
CHANGAMOTO basi uwe na
SULUHISHO la changamoto hiyo.
Mimi huwa ni ninamsemo wangu Titakapopata Kipa bora Zaidi basi hata Alisson tutataka aekwe benchi.
Tutakapopata Beki bora Zaidi basi hata VVD tutataka aekwe Benchi.
Tutakapopata Mshambuliaji bora Zaidi basi hata Salah tutataka aekwe benchi.
Lakini tutakapo kosa Mshambuliaji hata SOLANKE tutataka acheze pangapangua.
Sasa na Liverpool kwasasa haina suluhisho la mbadala wa TAA.
Najua utasema ni Milner na Clyne!
Lakini kwanza Clyne si mbadala wa TAA kwa sasa! Na Milner tunamuhitaji Zaidi kwenye Role ya Midfield kuliko RB kwa Baadhi ya Mechi ikiwemo game kama ya Leo Kumkosoa Milner kwenye Midfield ni Suicidal.
Na TAA si mbovu kiasi hicho munachomsema! Na kizuri Zaidi Msimu huu TAA kwenye EPL hajafanya error leading to goal hata moja. Sasa sijui ubovu huo wa kupindukia umetokea wapi.
Mimi sio kwamba nakupinga Mkuu! Ninajua wazi kuwa msimu huu TAA katika kulinda hayupo vizuri na anatupa wakati mgumu!
Lakini ana advantage Yake ya Kuwa ahead of Milner & Clyne! TAA kwenye offensive anadeliver vizuri tu kinyume na watu wanavyoongea! Anahitaji Credit kwa hili.
Kumbuka kuwa upande wa kushoto wa Robertson unatoa Mashambulizi mengi Zaidi kwasababu ya uwepo wa Mane, na vilevile Bobby anapenda sana kutokea upande huohuo wa kushoto hata kama atakuwa yupo kati.
Lakini upande wa kulia almost ni TAA na Salah tu jambo linalomfanya TAA anatumia pace kubwa kutoka chini mpaka kufika juu peke Yake ili amtafute Salah, tofauti na Robbo ambaye anapotoka na mpira chini basi Mane na Bobby wanamhelp mpaka kufika juu kueka Cross.
• Kwahiyo Mkuu ni kwamba TAA msimu huu hayupo vizuri kwenye Kukaba, Lakini si Ubovu wa kupindukia wa Kiasi hicho kama Munavyomuongelea.
• Halafu katika Magoli 7 tuliyoconcede kwenye EPL hakuna goli hata moja ambalo tumefungwa kwa direct mistake ya TAA.
• Na Mwisho ni kuwa kwasasa kwenye Kikosi chetu TAA ni lazima kucheza coz hatuna mbadala wake wa kusema tumreplace.