Live on Mlimani TV: Zitto Kabwe Vs Hamis Kigwangalla - Pushing forward the youth/Housing agenda!

Tehe tehe said bagaile a.k.a hamisi kigwangallah,ukiteuliwa tena na ccm kugombea nzega 2015 ntajiuzulu uanachama wangu chadema nnachokipenda
 
Mara nyingi huwa siwaamini viongozi wa CCM, lakini kuna wachache wanaoni-impress na wanaweza kuleta mabadiliko kwa taifa hili lakini siamini kama wanaleza kuleta mabadiliko ndani ya chama chao. hawa ni Deo Filikunjombe, January Makamba, Hamis Kigwangala na yule mbunge wa Mbarali.
 
Best wishes ila nakushauri usinywe maji huko au kujifuta kitambaa chochote huko uendako manake najua wajua wazi kuwa Prof.rwekaza ni usalama wa t.....
 
hapo kwenye current affairs ningeshukuru kusikia maoni yako juu ya suala la mteule wa ccm arumeru je kuna umuhimu wa kurudia kura?mbona nzega haikuwa hivyo?hata kipindi kikiisha naomba uje kujibu hapa jf
 
Nimetumiwa ujumbe kuwa Dr Kigwangala kumbe yuko live pamoja na Zitto Kabwe ndani ya Mlimani TV sasa hivi. Wale wenye access kwa sasa tuhabarisheni wanachozungumzia kwa sasa maana niko mbali na TV ningeweza kutoa updates
 
LIVE: Kingwalla anasema tatizo Watanzania wengi mind set zao ni ndogo wengi hawafikirii kujiajili bali wote wanawaza kuajiliwa, kwa hiyo ukosefu wa ajila utawafanya vijana waamke ili waanze kujiajili.
 
kama una nafasi fungulia tv yako halafu utoe updates jf. mwenzenu leo nmebanwa. hii ni special kwa wenye access na tv tu.
 
LIVE: Zitto Kabwe: Hakuna Mbunge anaezuiwa kufanya biashara zake kama anaona maslahi ya wabunge ni kiduchu, unaweza kuwa Mbunge na ukaendelea na Biashara zako. Wananchi wamechoka wasitonoshwe maumivu waliyonayo.
 
LIVE: Kigwalla: kama kuna mbunge anaona maslahi ni madogo na aende zake sio lazima kuwa mbunge na wapo Watanzania wengi tu wenye sifa za kuwa wabunge kuliko hawa wabunge waliopo sasa.
My take: Ukiwaangalia kwa Makini Zitto na Kigwangalla ni kwamba tu wameamuwa kumstahi Spika maana ananuka kila kona, Kigwalla bila kumungunya maneno anasema hakubaliani na spika ila inaoneka kuna ile kumstahi tu huenda anazeeka vibaya na hana mume bi mkora.
 
ashukuru mbeleko aliyobebewa chamani
Jamani msichakachuwe hii thread, kwa tunaofuatilia Live naona yuko poa tu anawakilisha vizuri yeye pamoja na Zitto Kabwe na ndio kipindi cha kwanza hiki naona mbunge wa Magamba hajaja kwenye kipindi kwa ajili ya kuwa tarumbeta la kusifu CCM na serikali yake. kwahiyo nashauri tuwe tunapingana kwa hoja.
 
Ajira kwa vijana, ufanyaji biashara, na ujenzi wa mtaji jamii – tuna matege

Na Perecy Paulo Ugula, IRINGA

Februari 19, 2012, Mheshimiwa Dr. Hamisi Kigwangalla (MB), Nzega, katika mtandao wa Facebook, na Jamii Forums, alinukuliwa akiandika: "Leo nimeamka nikimfikiria kijana wa Kitanzania. Haswa baada ya kupokea maombi ya vijana 6 kwa sms wakitaka niwasaidie kupata mahala pa kujishikiza, kwa 'marafiki zangu'. Mtihani huu mgumu sana. Nitautatuaje? ........ Nikasema, labda tuanzishe mjadala mahsusi wa kitaifa, utakaolitazama suala la ajira kwa vijana wa Kitanzania kwa mapana na marefu, na kulifanyia utekelezaji.......". Wazo zuri hili.Nimependa niandike. Ila tukijua kwamba: "........ Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Tena vijana wa siku hizi hawako tayari kutumiwa na wanasiasa kwa faida za kisiasa.....", (Dr. H. Kigwangalla).


Nimebahatika kusoma fomu za kuomba kujiunga na shahada za uzamili (master degree) katika usimamizi wa biashara, uongozi wa umma, na mambo ya utandawazi na maendeleo kwa baadhi ya vyuo vikuu vya Ulaya. Kwa pamoja wana utaratibu wa maswali yenye kumtaka mwombaji ajibu. Kigezo hiki hulenga kupima uelewa na maono ya mwombaji katika mambo ya umma, maendeleo, uongozi, utawala, utandawazi, na mambo mengine mtambuka. Hii ni tofauti na vyuo vyetu ambapo mtu anapojaza fomu za kujiunga na masomo hayo, haulizwi maswali magumu kujua maono na mchango wake katika jamii, zaidi ya kujaza taarifa nyepesi zikihusisha kuambatanisha vyeti vyake au barua za udhamini (reference letters) toka kwa wahadhiri waliopita au mwajiri wake.

Maswali magumu niliyopenda, miongoni mwao ni haya: "Ukipata nafasi ya kukutana na kiongozi mkuu wa nchi yako, kwa mfano Rais au Waziri Mkuu, utamuuliza swali gani na kwa nini? Umekuwa na mchango gani kwa jamii yako ndani ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita? Unapanga kuchangia nini katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi yako katika kipindi cha miaka kumi baada ya masomo yako?"

Nilifanyia kazi swali moja ambalo niliona lina mahusiano makubwa na mustakabali wa mambo mengi ya nchi yetu, yakiwepo yanayoguswa na kichwa cha makala haya. "Ukipata nafasi ya kukutana na kiongozi mkuu wa nchi yako, kwa mfano Rais au Waziri Mkuu, utamuuliza swali gani na kwa nini?"

Nilipenda kupata maoni ya swali hili kutoka kwa watu tofauti kama wahitimu wa vyuo vikuu, wahitimu wa vyuo vya ufundi, wafanyakazi kwa ngazi na nafasi tofauti za uongozi na wananchi wa kawaida. Majumuisho ya maswali yao kwa Rais au Waziri Mkuu yalihusu ukosefu wa ajira, kuporomoka kwa thamani ya fedha na uchumi wa nchi, kutoeleweka dhana ya uchumi kukua huku idadi ya maskini inaongezeka, kuwepo rasilimali nyingi na huku tumeendelea kubaki maskini na tukiomba misaada.

Kutokana na maoni ya watu mbalimbali kuhusu maswali ambayo wangeuliza, nilijenga msingi wa swali langu kwa viongozi hawa, kwa kuumba swali hili: Tanzania imesifika vizuri kwa kujenga uchumi wake katika uelekeo sahihi: (a) hii ina maanisha nini maana idadi ya watu wanaoishi katika umaskini mkubwa inaongezeka? (b) kwa nini ukuaji huu wa uchumi haondoi tatizo la ajira miongoni mwa makundi ya jamii kama vijana, wanawake na wahitimu wa vyuo mbalimbali? (c) Ni upi utakuwa mpango endelevu na mkubwa wa serikali kuleta matokeo chanya kwa kuondoa tatizo la ajira miongoni mwa makundi katika swali la (b) hapo juu?

Tatizo la ajira kwa vijana
Kupunguza tatizo la ajira kutoka asilimia 12.9 mwaka 2000/01 hadi asilimia 6.9 mwaka 2010 na kuongeza ajira maeneo ya vijijini ilikuwa ni malengo ya utekelezaji ya MKUKUTA I.

Wakati anaingia katika uongozi, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete aliahidi kutengeneza ajira milioni moja kati ya mwaka 2005 hadi 2010 kwa vijana wa Tanzania; ambapo alitoa shilingi 21 bilioni (Tanzania Bara), kwamba kila mkoa upate shilingi bilioni moja, ikiwa ni kuwawezesha wajasiriamali. Katika kipindi cha Bunge la Bajeti la 2008/2009, ilisemwa kwamba tayari zaidi ya ajira 400,000 zilishatengenezwa, na kwamba fedha zilizotolewa zilichangia katika upatikanaji wa ajira hizo. Wote tulisikia katika vyombo vya habari, mpango huu (ambao ulijulikana zaidi kama Mabilioni ya JK) ulinufaisha ambao tayari walikuwa wamesimama kibiashara vizuri, na wenye nafasi katika taasisi za fedha au serikalini.

Taarifa zinaonyesha kuwa ingawa tatizo la ajira linatofautiana kati ya maeneo ya mjini na vijijini; vijana wakiathirika zaidi kwa asilimia 13.4 ikilinganiswa na wastani wa kitaifa wa asilimia 11.7; sasa, kwa kuwa tatizo la ajira ni mtambuka na linahitaji ushiriki wa wadau wengi wa kiuchumi kulikabili; ni muhimu sana kuwepo ulinganisho mzuri wa kiwango cha ongezeko la nguvukazi (isiyo na kazi) inavyokuwa na kuingia katika jamii na kiwango cha ukuaji wa uchumi katika kuongeza fursa za ajira kwa makundi muhimu, tofauti na namna ambavyo serikali imekuwa ikitamka kwamba imeongeza ajira.

Mh. Dr. Kigwangalla ni mwanaCCM. Sitaki kumsema vibaya kwa chama chake. Jitihada za serikali kuhusu ajira (kupitia chama cha CCM) zilitamkwa kisiasa kuliko kiuchumi na kimaendeleo. Katika uchaguzi wa 2005, kutengeneza ajira milioni moja ifikapo 2010 ilikuwa ni ahadi ya chama. Aidha, Sera ya Taifa ya Ajira ya 2008 inataja changamoto ishirini na nne za ajira na mikakati ya kisera katika kukabiliana nayo; pia Sera ya Maendeleo ya Vijana ya 2007 kusimamia mambo ya vijana. Tunaposoma sera hizi, namuunga mkono Mh. Dr. Kigwangalla kwamba: "Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Tena vijana wa siku hizi hawako tayari kutumiwa na wanasiasa kwa faida za kisiasa".

Hivyo, kwa kuwa tumeona sera hizi ni nzuri kimaandishi, ni vema zikawa zenye tija (robust and impacting) na endelevu. Jamii zote vijijini na mijini zinavuja jasho vibaya mno, kwa tatizo la ajira na uzalishaji duni kiuchumi. Waathirika wakubwa wakiwa ni vijana wanaomaliza hatua mbalimbali za kielimu na akina mama. Kwa nini imekuwa hivi kwa muda mrefu? Ahadi zinazotamkwa zinatupeleka mbele au tunarudi nyuma kilomita nyingi?

Nafasi yetu katika ufanyaji biashara kati ya nchi 183 ikoje?
Tanzania imebarikiwa kuwa na sekta nyingi za kumpa fursa ya kiuchumi mwananchi. Kilimo, uvuvi, utalii, madini, huduma za chakula, hoteli, malazi, usafirishaji wa umma, huduma za jamii kama shule na afya. Sekta hizi zina fursa nyingi kibiashara. Tunapojenga hoja kuhusu ajira, ni vema tuangalie nafasi yetu kibiashara katika vigezo vya kuwezesha na kusaidia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa wazawa na wageni.

Ripoti za Ufanyaji Biashara (Doing Business Reports) ambazo hutolewa kila mwaka na Wataalamu wa Benki ya Dunia hueleza kwa uchambuzi taratibu zinazowezesha ufanyaji biashara na zile zinazoleta changamoto katika ufanyaji biashara kwa kila nchi, ambapo Tanzania tumeonekana kuporoka kwa nafasi tatu katika ripoti ya 2011 kwa kuwa nafasi ya 128 badala ya 125 mwaka 2010.

Vigezo kumi na moja (11) vya uchambuzi vya kuwezesha ufanyaji biashara huangaliwa ambavyo ni: kuanzisha biashara, kupata vibali vya ujenzi, kusajili rasilimali, kupata mikopo, kulinda wawekezaji, ulipaji kodi, kufanya biashara nje ya nchi, kutekeleza mikataba, kufunga/kufilisi biashara, kupata umeme na kuajiri wafanyakazi.

Kwa mwaka 2012, kutokana na taarifa za kwenye wavuti za Doing Business Report Tanzania iko nafasi ya 127 (ikiwa imepanda kwa nochi 1), toka nafasi ya 128 mwaka 2011; ambapo kwa kila kigezo tunasomeka kama ifuatavyo: kuanzisha biashara (123), kupata vibali vya ujenzi (176), kusajili rasilimali (158), kupata umeme (78), kupata mikopo (98), kulinda wawekezaji (97), ulipaji kodi (129), kufanya biashara nje ya nchi (92), kutekeleza mikataba (36), na kufilisi biashara (122).

Taarifa hii inatupa picha gani kuhusu uwepo wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)? Wakala wa serikali wenye jukumu la kusaidia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa wazawa na wageni; hasa tunapotafakari hoja ya ajira kwa vijana, umaskini unaoonekana, rasilimali nyingi tulizonazo, na ombaomba yetu inavyoongezeka?

Kuanzisha mfuko maalum wa kutoa mikopo ya uwekezaji kwa vijana wa Kitanzania, si maono mapya. Azimio la Arusha, Dira ya Tanzania 2015, Mpango wa Maendeleo wa Tanzania 2012/2016, MKUKUTA, MKURABITA, sera, mipango, mikakati, na mabilioni ya JK zinataja ‘kujielekeza' kwenye maendeleo. Kuwezesha walio pembezoni. Zinataja kwamba ‘dhamira' ya serikali ni kuwaletea wananchi hali bora ya maisha. Hali ikoje?

Kuna ushahidi. Uchambuzi makini unapofanyika kuhusu matokeo ya mikakati na mipango yetu mingi ya maendeleo, malengo hupapaswa.Wizi na kujilimbikizia mali huongoza. Ndiyo maana tumekuwa katika nafasi hizo hapo juu tunapopimwa vigezo-wezeshi vya ufanyaji biashara.

Nia yetu ya ujenzi wa mtaji jamii ni ipi?
Wakati wa nusu ya pili ya karne ya ishirini, kulijitokeza maendeleo makubwa katika sayansi na teknolojia na uimarishaji wa serikali, katika kujali kwamba dhana ya maendeleo inalenga kufanikisha ubora wa maisha ya watu. Karne hii imebeba tofauti kubwa sana ya hali ya maendeleo ya watu na kutengeneza matabaka kiuchumi, kijamii, huduma, na uimara wa serikali katika kutatua matatizo hasa majanga yanayokumba maskini. Hili linayumbisha ujenzi wa mtaji jamii (human capital).

Jamii ya nchi yeyote ile ni rasilimali amali kuitambulisha nchi husika: kimaendeleo – kiuchumi, utamaduni, kijamii, teknolojia, utawala bora na uongozi. Mtaji jamii ni ‘bohari' ya stadi, maarifa, na utu uliopandikizwa kwa jamii ili kuiwezesha jamii kuweza kufanya kazi yenye thamani kiuchumi na utu. Ni wajibu wa serikali kujenga mtaji jamii imara kwani ni muhimu kufanikisha uhai wa nchi. Mtaji jamii, hujengwa na kuboreshwa kwa kuwaongezea wananchi maarifa, elimu na uzoefu – kwa kuwapa fursa ya kufikia kwa urahisi huduma za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, stadi, fedha, afya, na elimu. Bahati mbaya matege ni makubwa katika elimu – hasa ubora wake katika kumsaidia mhusika kuyakabili mazingira ya maisha yake.

Nimesema, taarifa mbalimbali za maendeleo ya jamii na watu nchini zimesongwa na mkanganyiko wa mishtuko ya kufeli. Biashara ya madawa ya kulevya, usafirishaji binadamu na makosa ya jinai, vimeongezeka kwa kasi katika jamii – yakisifika kuzalisha ‘faida' kubwa, na kufanywa na watu wenye nafasi kubwa katika idara za serikali. Vijana wamekuwa wahanga wakubwa wa biashara hizi. Fedha za miradi yao ‘hupindishwa' na kuvujia mifukoni mwa viongozi hawa. Washtakiwa wakubwa wa makosa hayo ni vijana wenyewe; wa kiume na wa kike.

Hitimisho
Asilimia 80 ya nguvukazi nchini inaishi vijijini. Nia ya dhati ya kujenga mtaji jamii ili kuwezesha ajira kupatikana, kama Mh. Dr. Kigwangala anavyotafakari kuhusu kijana wa Tanzania tunahitaji uongozi wenye nia ya dhati na uwezo mkubwa wa kuthubutu kutenda na kusimamia nidhamu. Tumekuwa na matege katika nia ya dhati na uwezo wa uongozi unaothubu katika kusimamia na kutenda nidhamu. Uongozi unaothubutu utahangaika kupunguza au kuondoa asilimia 13.4 ya tatizo la ajira kwa kutumia kila fursa ya kiuchumi kwa ufanisi. Uongozi unaothubutu, utamfanya Mh. Dr. Kigwangala kutotofautiana baadhi ya misimamo yake katika maslahi mapana ya kijamii na chama chake. Uongozi unaothubutu, utahangaika kupunguza nafasi mbaya za vigezo vya uduni wa mazingira yetu kibiashara katika Taarifa ya Ufanyaji Biashara 2011 na 2012.

Saikolojia inatujulisha kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya hulka au tabia ya kiongozi (Rais, Waziri, Mbunge, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi, au Baba/Mama) na picha ya maendeleo katika utawala wake (nchi, wizara, jimbo, mkoa, au familia). Na hapa ndipo wasiwasi mkubwa ulipojionyesha katika wachangiaji kwenye ukurasa wa facebook kuhusu hoja hii. Wengi wameonyesha wasiwasi. Tuna shida ya uongozi wenye nidhamu. Hatusemi ili kujitafutia sifa bianfsi. Tunasemwa kutofanikiwa katika uongozi wenye nidhamu, hasa matumizi!

Rais Paulo Kagame wa Rwanda amejitambulisha katika uadilifu, nidhamu na tabia ya kujali umma kwanza, ndio maana miradi ya maendeleo ya umma wa Rwanda inasimamiwa kwa nidhamu. Tumekuwa tukibeza kwamba nchi ya Rwanda ni ndogo kama mkoa mmoja wa Tanzania ndio maana wamefanikiwa, sawa. Sisi tumekuwa tunashindwa kujikita katika jambo moja kikweli kweli kwa nidhamu si kwa bahati mbaya. Na huu ni msingi wa tatizo la uongozi wenye kushindwa kuthubutu ulipo, katika vyama vya siasa mpaka serikalini. Haya ni matege!

Ni upi utakuwa mpango endelevu na mkubwa wa serikali kuleta matokeo chanya kwa kuondoa tatizo la ajira miongoni mwa vijana, wanawake na wahitimu wa vyuo nchini? Serikali itashtuka na kuona hoja hii inahitaji msukumo mpya wa mipango yenye kulenga matokeo na usimamizi wenye tathimini ya nidhamu na uwajibikaji? Tafakari. Chukua Hatua!



Perecy Paulo Ugula,
Rafiki wa Elimu,
Simu: 0766 082388
 
Kipindi ndio kimemalizika sasa hivi, Kigwangalla yupo fresh na Zitto yupo fresh, nimeridhika na ushiriki wao makini huu ni mwanzo mzuri, ndio tunaanza sasa kuwapambanunuwa ni kina nani wanasimama na sisi na kina ni maadui wa Taifa letu. Hongera Kingwangalla kwa kujitenga na mawazo mufilisi ya kimagamba.
 
The show was excellent, very vibrant with excellent new ideas sema muda ulikuwa mdogo...simu zilikuwa nyingi sana sikutegemea kwa kweli

Nilikuwa niwapigie kuwauliza matokeo ya uchunguzi wa kamati ya bunge dhidi ya UDA. Kuna habari UDA inunuliwa mabasi 30 kupitia accounts za nje kwa vile accounts zao zimekuwa frozen.
 
The show was excellent, very vibrant with excellent new ideas sema muda ulikuwa mdogo...simu zilikuwa nyingi sana sikutegemea kwa kweli
Inabidi hivi vyombo vya habari kuwekea mkazo zaidi vipindi kama hivi na kutoa nafasi zaidi kwenu kuweza kuzungumza na kukusanya mawazo mbali mbali..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom