Tulia Ackson: Wanaojitolea kwenye Kada za Afya na Ualimu wapewe kipaumbele kwenye Ajira

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 6, 2023 kwenye Mkutano wa 11, Kikao cha 3.



RIPOTI YA CAG YALETWA BUNGENI
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imepelekwa Bungeni leo na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.
WANAOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE KWENYE AJIRA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amemshauri Waziri wa Afya na Waziri wa TAMISEMI kukaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ili kutengeneza mfumo mzuri wa kuajiri Watumishi wa Kada za Afya na Walimu wanaojitolea pindi nafasi za kazi zinapotangazwa.
Amesema, "Huwa haipendezi sana yaani kwamba wao ndio huwa hawana sifa za ajira, yaani kwa sababu ajira zikitangazwa, wale wote wanaojitolea wanajikuta kwamba kwenye eneo lako hakuna hata mmoja aliyepata. Sasa huwa tunajiuliza kama wale wanaojitolea hawana sifa, waliokaa nyumbani wanaomba kazi ndio wana sifa kuwazidi hawa wengine?"

Amewashauri kutengeneza mfumo mzuri wa kupata taarifa za watu wanaojitolea ili ajira zinapopatikana zitumiwe kuwapa kipaumbele cha kuajiriwa.

MAADILI YA TAIFA YALINDWE
Mbunge wa Iringa, Jesca Jonathani Msambatavangu amewataka Watanzania kulinda maadili ya nchi kwa kutokuiga mambo mabaya yanayosambaa kwa kasi duniani.

Amekemea ukatili unaoendele dhidi ya binadamu, watoto pamoja na kushika kazi kwa vitengo visivyofaa vya ulawiti, ubakaji na ushoga.

JESCA.jpg

Jesca Jonathani Msambatavangu, Mbunge wa Iringa Mjini
Amewaasa Watanzania kutoa fursa kwa mataifa Mengine ya nje kuja kujifunza nchini namna ya kutunza watu wake na kuishi kwa maadili yanayofaa.

Pamoja na uwepo wa usalama wakutosha kwenye mipaka ya nchi, Mbunge MSambatavangu amebainisha kuwa hali ya usalama wa watoto nchini upo hatarini.

Amewaomba watanzania kwa umoja wao kukemea na kulaani vvitendo vyote visivyo na maadili kwa taifa. Ameongeza, "Suala hili la ukatiki kwa watoto wetu, ulawiti kwa watoto wetu, ubakaji wa watoto wetu, masuala ya ndoa za jinsia moja yasifumbiwe macho. Tuyaongelee makanisani, tuyaongelee misikitini, tunaanza hapa bungeni, tuyaongelee Serikalini, tuyaongelee kwenye familia zetu, tutapotea"

CHANGAMOTO ZA VIJANA KWENYE AJIRA NA MASOMO
Mbunge wa Kilolo, Justin Lazaro Nyamoga amezungumzia utaratibu wa ajira kwa vijana wanaojitolea kwenye Sekta mbalimbali nchini, amesema Serikali iboreshe mfumo wa kujitolea, pamoja na kuweka mifumo thabiti itayakayowezesha wanaojitolea kuajiriwa.

Amesisitiza uwepo wa uwazi kwenye kuchagua vijana wanaoajiriwa, hali hii inazalisha malalamiko na kutoa mianya ya upendeleo.

IMG-20230223-WA0367.jpg

Mbunge wa Kilolo, Justin Lazaro Nyamoga
Suala la Mikopo kwa vijana wanaosoma vyuo vya kati, Nyamoga ameeleza kuwa haelewi kwanini hawapewi mikopo kwa kuwa wao pia ni watoto wa maskini wanaohitaji kusaidiwa.

"Mimi sijajua, Kigugumizi cha kuwakopesha vijana wanaosoma vyuo vya kati kinatoka wapi? vijana hao ni watoto wa maskini, vijana hao wakimaliza vyuo tunawaajiri.." Amehoji

Utengenezwa mfumo maalumu ambao hautoi upendeleo kwenye sehemu za kujitolea, na kuwe na mfumo mzuri wa ufatiliaji ikifika kipindi cha ajira inakuwa rahisi kuwa na data zao.

Ameongeza kuwa kwenye mradi wa BBT, ilikuwa ni rahisi kupata vijana ambao wapo kwenye mikopo ya 10% ambao wanajishughulisha na kilimo kuliko kuchukua vijana wapya ambao hawajui lolote. Mradi wa BBT ambao unafuata uzingatie hilo.

Pia, amekemea maadii yasiyofaa kwa kusema kuwa sisi wenyewe tuna mifumo yetu na hatuwezi kufundishwa na taifa lote kuhusu kukuza mila na desturi zetu, tutajenga taifa zuri kama tutaheshimu mil ana desturi zetu suala la ushoga. Kila mtanzania aone haja ya kuwajibika katika taifa letu kwa kutunza mil ana desturi zetu.
 
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 6, 2023 kwenye Mkutano wa 11, Kikao cha 3.



WANAOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE KWENYE AJIRA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amemshauri Waziri wa Afya na Waziri wa TAMISEMI kukaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora ili kutengeneza mfumo mzuri wa kuajiri Watumishi wa Kada za Afya na Walimu wanaojitolea pindi nafasi za kazi zinapotangazwa.

Hapo kuna Simbachawene, hii tayari tunaiita kuwa ni tick.
Nampongeza sana mama kwa hoja hii nzito mno
 
Sijaipenda hii italeta upendeleo kwa kisingizio cha kujitolea...

Dalili nyingine ya mwanya wa upigaji maafisa utumishi, wakurugenzi na wakuu wa vitengo mwanya huo hapo muwajaze ndugu zenu.
 
Mara waseme vijana wajiajiri ooh sijui wajitolee! Akili za kijinga sana hizi. Yaani mtu ajitolee bure kabisa wakati mfukoni hana hata mia. Huu ni uzwazwa!

Kwa kifupi anayejitolea mara nyingi sio mbunifu, mahiri na mwerevu kulinganisha na aliyejiari.
 
Mara waseme vijana wajiajiri ooh sijui wajitolee! Akili za kijinga sana hizi .
Yaani mtu ajitolee bure kabisa wakati mfukoni hana hata mia..
Huu ni uzwazwa!!
Kwa kifupi anayejitolea mara nyingi sio mbunifu, mahiri na mwerevu kulinganisha na aliyejiari.
Kiukweli nawashangaa wanaojitolea hivi wamekosa kabisa cha kufanyaa! Hawa ndio wanaowapa jeuri waajiri awawezi kuona uhitaji mapengo yanazibwa na wanaojitolea hawajui tu wao wenyewe ndio chanzo cha matatizo yao wenyewe ya kukosa ajira
 
Ni kweli na kwa nini watu wajitolee wapewe ajira mkiwa mnajitolea tolea ndio chanzo cha waajiri kutokuajiri wanaojitolea mimi huwa siwaelewi hvi wameshindwa kabisa kutafuta cha kufanya wanawalemaza waajiri awaajiri kwa sababu uhitaji auonekani
Wengi wa wasomi wa kitanzania ukikitoa cheti kile alichonacho(degree) kichwani ni empty set
 
Mheshimiwa Tulia amepotoka,ila Mimi bado najiuliza hawa viongozi wetu wanapotoa maagizo yao huwa wako fine kwa akili zao!??

Tulia anatakiwa ajue kuwa kwa upande wa elimu hakuna walimu wanaojitolea kuannzia January Hadi December bila malipo ,Bali kuna pesa wazazi wanachanga theni wanalipwa,


Lakini pia atambue kuwa kuzipata hizo nafasi za kujitolea ni mbinde,mashule yamejaa,sasa unaposema hawa wanaojitolea ndo wapewe kipaumbele ni kuleta upendeleo usio na maana,aache watu waajiliwe kwa sifa zao.

Lakini pia akisema ati waajiriwe wanaojitolea unaleta mianya ya rushwa pindi ajira zinapotolewa kwani wahitimu huwa wanaenda kwa wakuu wa shule,maafisa rasilimali watu na wakurugenzi ili wawatambue kuwa wanaojitolea hapo lengo lao wapate ajira
 
Back
Top Bottom