Jamani wana Jambo Forums wenzangu, wahenga walisema "if you can not beat them, join them". Uchaguzi wa CCM kwa kweli umetufunza mengi, tusisahau ya kwamaba ingawa JK twamchagua wote (hata kama hujamchagua bado no rais wa waTanzania wote. Yeye ana vita vilevile ndani ya chama (wanamtandao, asilia etc) kama alivyo nao nje..... Sasa kuangalia ju juu, inaonyesha kidogo kunaweza kuwa na mwanga mwisho wa njia...Tumpe muda mzee ajipange, tukumbuke ana zile nafasi za wabunge wa kuteuliwa na rais (nadhani amebakiza 6) pia ana nafasi za kuteua za NEC (amebakiza 8) kwa hiyo shime, hatuwawezi hivyo tujipange na kuwasaidia kulisukuma gurudumu letu jamani.
Naomba kuwakilisha............