Kama Malecela ameona vyombo vya habari ni muhimu katika kutuma ujumbe wake, kwa nini anawakataza wengine kuvitumia hivyo hivyo vyombo vya habari kujisafisha??.
Hapa nimeona alitumwa kufanikisha mambo matatu yafuatayo;
- Kuvionya vyombo vya habari kuwa sasa viko karibu vitafungiwa kwa kuandika wasiyoyapenda wakuu.
- Badala yake wanataka, vyombo vya habari vimsaidie raisi (yaani vimpambe), na moja kati ya mapambo ni kuwa viwahabarishe wananchi na wafadhili kuwa tayari mafisadi wameshachukuliwa hatua na JK.
- Lakini kubwa zaidi ni kuwa Mzee Malecela pia alitumwa kumpiga mkwara Dr. Mwakyembe na wenzake (Prof. Mwandosya n.k) ambao inaelekea wana nia ya kumpinga Kikwete in 2010. Hili ameliweka wazi kwamba Kikwete atakuwepo hadi 2015 na akina Mwandosya ni vema tu wakatumia vipesa vyao kwengine maana hawataweza kupambana na BOT ya Kikwete.
Asijekurithisha tu huo ubunge kuendeleza libeneke.
Sababu kubwa ya Press Conference ya Mzee Malecela sio Malumbano ya Viongozi wa CCM.CCM walikuwa na nafasi ya kujadili malumbano hayo katika vikao vya Ndani vya CCM.....Message aliyokuwa anataka kuitoa Dr.Malecela ni kwamba""Mwanachama yeyote wa CCM asithubutu kufikiria kugombea Urais 2010,nafasi hiyo bado ni ya Kikwete,ni utaratibu wa CCM kumuacha Rais amalizie vipindi vyote viwili""Message hiyo Dr Malecela ameipa msisitizo.

Kuna fununu kuwa kuna baadhi ya WanaCCM wanataka kumshinikiza JK asigombee tena katika kipindi kijacho...JK ni mdhaifu kukiwa na kelele nyingi za namna hiyo,kwa hiyari yake mwenyewe anaweza kusema "Mimi sasa basi!! Mwanachama mwingine mwenye uwezo aendeleze kazi hii"...Dr Malecela analijua hilo...ameamua kwa makusudi kuchukua nafasi ya kufanya campaign ya kuwatia Uoga wanaoshinikiza kumuondoa Kikwete,Kazi ndio imeanza.Maneno ya Dr Malecela yatakuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari Tanzania...
Ningependa na kufurahi kama kuna Mwanahabari ambaye angemuomba Mzee Malecela sasa apumzike Ubunge wa Mtera....kwa miaka 75+ kuweza kwenda kasi na maendeleo ya Jimbo si rahisi,lakini kwa maelezo yake inaonekana bado atagombea Ubunge huko Mtera!
Mzee Malecela anasema kuwa kwenye ukumbi wa NEC kuna maneno ya Baba wa Taifa yanasema "mimi ninang'atuka lakini naendelea kuamini bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba...."
Halafu anaendelea kusema mwaka 1992 wakati wakipitisha ripoti ya Nyalali kuruhusu vyama vyingi wakati yeye ni Waziri Mkuu "ndipo Baba wa Taifa alisema maneno haya."
Nyerere aling'atuka lini na vyama vingi viliruhusiwa lini? Malecela, of all the people, asiwe loose na hizi facts.
Hahahaha point...!

Sasa kama yeye anasema wanaolumbana wamalizane kwenye vyombo husika i.e. Chama n.k. na siyo kwenye vyombo vya habari kwa nini yeye asingesema hayo kwenye kikao cha chama chake hadi kuitisha mkutano na wanahabari wa kutoka kwenye vyombo vya habari na kusema wanaolumbana wasilumbane kwenye vyombo vya habari? What the hell?