Kweli mkuuila kila mara anaongea maneno yanayoonyesha kujutia urais, kuna kipindi aliongea na Pengo na kusema anatamani saa nyingine asingechukua form, juzi alipokuwa anakabidhiwa ripoti ya uchaguzi na Lubuva alisema anatamani urais ungekuwa ni awamu ya miaka 5 tu kwa sababu ya maneno ya watu.
Mimi naona kweli anafanya kazi, anatamani sana nchi isonge mbele haraka ila ilikuwa wrong kwake kuchukua urais,
angekuwa chini ya rais, mtu ambaye anaweza kuchora ramani za maendeleo, diplomatic na anayejua ku deal na criticism za kisiasa kitaifa na kimataifa, kisha yeye akawa kwenye nafasi ya kiutendaji iliyopo chini ya huyo mtu
urais ni nafasi ya kisiasa, unahitaji mtu mwenye temperament iliyo stable, diplomacy nzuri, mwenye calculation za mbali, na mvumilivu,
kwenye dunia ya leo mtu huwezi ukawa una sema eti hutaki wanaokukosoa eti tufanye kazi,
dunia ya leo media zimejaa, hata ukifungia mikutano bado wapinzani wanapewa coverage na vyombo vya habari, social media kama forums, facebook, YouTube Twitter n.k pia zinatumika sana na wananchi na wanasiasa wa upinzani wanazitumia, je utazuia pia media zote hizo kwa sababu hutaki kelele?
siku hizi kama huwezi deal na criticism bora usiwe mwanasiasa kwa kuwa huwezi kuzima, ni miezi 8 tu ila mtu keshaanza kutweta...tuone
huyu anataka viwanda viote kama uyoga, kwa kupiga marufuku bidhaa za nje kama sukari, kuongezea kodi bidhaa za nje kama nguo na mafuta ili tununue vya ndani wakati viwanda vya ndani vipo usingizini
Ahadi ipi aliyoitekeleza? Mojawapo ya yaliyomshinda ameapa kuwakamata mafisadi, kwa akili yako kuna mafisadi gani wakubwa kuliko wale waliokuwa madarakani? Na ndiyo mbele za watu ameamua kusema na kila mtu amesikia kuwa atawalinda. Makontena yalitopitishwa bandarini bila kulipiwa kodi, bomba la mafuta la wizi, ESCROW account, IPTL, RICHMOND, nyumba za serikali, meremeta, UDA, EPA, Lugumi, mikataba ya madini ya ovyo, yote ni kazi ya waliokuwa wadarakani , yeye ameapa kuwalinda mahakama ya nani sasa? Punguza kujipendekeza kuwa mzalendoMagufuli yuko sawa katika uongozi. Yeye anafanya kwa vitendo zaidi. Ndani ya kipindi kifupi tu tangu kuingia madarakani ametekeleza ahadi nyingi. KUMHUKUMU RAIS KWA SASA KUWA AMESHINDWA NI UPUUZI MTUPU KWANI KIPINDI CHAKE CHA KUONGOZA MUHULA MMOJA NI MIAKA MITANO.
wewe tulia utupe hojaUngetulia ulikuwa na hoja mzuri sana, hata hivyo hongera!!
ww kweli chai,kwani hiii mitandao yote ya jamii siimeanzia ulaya na ulaya ndipo wananchi wake wengi wanatumia mitandao mbona bado wanaandamana???Dunia ya Leo yenye social media like Facebook, WhatsApp, Jamii forum, magazeti kibao, redio kibao siyo lzm uandamane au kufanya mkutano ndio ufikishe ujumbe kwa jamii.
Unaweza kuongea kwenye redio tu kila MTU akasikia ujumbe wako.
UKAWA kuweni wabunifu
anatumbua kimya kimya ile insu ya kutangaza ameona haina dili mfano wiki iliyopita mkuu wa utumishi , manunuzi mamlaka ya bandari wametumbuliwa pamoja na wakurugenzi wengineNimemiss sana kusikia PM na Mkuu wa Kaya wakitumbua majipu...
Maana utumbuaji umekua wa kusua sua now days...
Magufuli yupo vizuri sana katika uongozi. Yeye anafanya kwa vitendo zaidi. Ndani ya kipindi kifupi tu tangu kuingia madarakani ametekeleza ahadi nyingi. KUMHUKUMU RAIS KWA SASA KUWA AMESHINDWA NI UPUUZI MTUPU KWANI KIPINDI CHAKE CHA KUONGOZA MUHULA MMOJA NI MIAKA MITANO.
hiyo kitu kwa wa Africa ni ndoto sana labda miaka bilion 1 ijayo.si ajiuzulu mbn pm camerun amejiuzulu, only in Africa that never happen
Yan kwa kweli hivi ndo huyu mkuu wa kaya wa Majipu kweli? Mbona kachuja sana alafu kwa haraka mno
Yupo sahihi kbs media coverage online ni kubwa sana mukubwa, bunge gizani lakini watu wanajua fulani kasema nini hata hao bunge hawajahariri.unatumia kichwa au kiungo kingine kufikiri? I doubt!
2500Sukari unanunua shilingi ngapo huko kwenu
Alifungie kwa uchochezi upi na sheria ipi? au unataka aitie serikali hasara tena kwa kulipa fidia kwenye kesi inazoshindwa?Nadhani umefika wakati TANZANIA DAIMA lifungiwe kabisa...lifungiwe kama lilivyofungiwa MAWIO...Baadhi yetu tumechoka na kauli za 'kihuni' na uchochezi...
Alifungie kwa uchochezi upi na sheria ipi? au unataka aitie serikali hasara tena kwa kulipa fidia kwenye kesi inazoshindwa?
Nawashangaa watu mnaomtetemekea na kumuabudu rais ambaye ni mwanadamu mwenzenu tena mwenye madhaifu kibao, mnatokwa na mapovu na kutukana akikosolewa kwa jambo dogo, eti kauli za kihuni?
Magufuli hana kauli za kihuni? kusema meya anatetea ujambazi, watu watoe tairi za magari wauze, kuwaita wanafunzi wa UDOM, kusema sukari inayotoka nje ni nafuu kwa kuwa haifai kwa matumizi ya binadamu etc. sio kauli za kihuni hizo? au una utiifu wa kikondoo sana hadi unashindwa kuona? nakuhurumia mtu mwoga kama wewe