Lissu: Urais umemshinda Magufuli

Lissu: Urais umemshinda Magufuli

Magufuli yupo vizuri sana katika uongozi. Yeye anafanya kwa vitendo zaidi. Ndani ya kipindi kifupi tu tangu kuingia madarakani ametekeleza ahadi nyingi. KUMHUKUMU RAIS KWA SASA KUWA AMESHINDWA NI UPUUZI MTUPU KWANI KIPINDI CHAKE CHA KUONGOZA MUHULA MMOJA NI MIAKA MITANO.
Kwa kweli! Mbona mambo meengi yamerekebishika. Go Magufuli Go! Wachache wenye maslahi yao binafsi wasikubabaishe!
 
Nashangaa wanao ona Lissu kasema uongo jambo ambalo jpm kesha litamka.
Kukiri hadharani kuwa angejua kazi yenyewe iko hivyo asingegombe sio kukiri kuwa imemshinda? Kutamka kuwa JK kamwachia kazi ngumu sana sio kuona kuwa kazi hiyo ni mzigo asio weza kuubeba? Bado hayo yakukataa kuhojiwa au kukosolewa, kutaka mambo yasiwe ya uwazi na hata shughuli za kisiasa zilizo kikatiba kutumia dola kuzuia yote hayo ni kushindwa kazi.
Mwenye kazi kakiri (kiutu uzima) kuwa nimeshindwa sasa Lissu akirudia kauli yake watu mnapinga tuwaeleweje? Mnataka kumlazimisha kuwa hajashindwa?
 
Ha ha ha, unamshindaje, wakati JPM sio mtu wa Ahadi ni utekelezaji tu.. Na amewabana kila kona
Unamaanisha nini kusema hivi? Ni kona zipi unazofikiri wewe zimebanwa? Au Una maana kuadimika kwa sukari na maisha kuwa magumu? Au biashara na mapato kushuka ndio kona unazomaanisha? Bado Una safari ndefu ya uelewa na uchambuzi wa hoja.
 
Yeye jimbo lake amefanya lipi la maana tuanzie hapo ndipo tumjadili Rais.
Jimbo litafanya nini Kama ruzuku na mafungu ya fedha za miradi hazipelekwi kwa sababu limeporwa na upinzani? Thibitisha maendeleo ya jumbo atokako waziri mkuu na like LA nape lenye shida ilipita sifa za kimataifa LA ukosefu wa maji ulinganishe na jumbo LA Lissu. Siku nyingine siyo unaropoka tu hapa bila kufanya vivid comparison utaumbuka. Nenda bagamoyo alikotoka mstaafu na sasa lipo chini ya Prince utuambie maendeleo take yanafanana na jumbo LA Lissu? Njoo hapa kisarawe tu ilikotawala ccm utueleze maendeleo yake kama yanafanania na
muda mliotwala hapo. Fanya tafiti kwanza sio unawahi buku mbili.
 
kuongoza watanzania ni shida sana mimtu haina shukrani cjui mpaka wabebwe khaa
kuongea ni rahic sana.
Ungekuwa mhanga wa wanafunz wa udom au kusubiri ajira mpya wala usingeongea hivyo.
Kiukweli, sasa hiv maisha magumu mtaani.
Gharama za manunuzi kila siku zinaongezeka kila kukicha.
Ndio sikatai anaongoza vizuri ila kuna wakati anawaumiza wanyonge.
Unapongeza kodi ndivyo na bidhaa zinaongezeka.
Aongeze na mishahara pia,
ila mm la ajira mpaka miez 2 sijakubaliana naye kbs.
Km mtu unakula na kunya huwez kumkumbuka aliyeshinda njaa
 
Kwa kweli! Mbona mambo meengi yamerekebishika. Go Magufuli Go! Wachache wenye maslahi yao binafsi wasikubabaishe!
Kiukweli maisha yamekuwa magumu japo anaongoza vizuri lkn kajisahau sana.
Sasa biashara haziend hasa weny hotel na mabar. Wanafunga tu. Najua utabisha sana lkn kwa uhalisia maisha yamekuwa magumu.
Sasa hata haliposema ajira baada ya miez 2 nahic urifurahi sana
 
Yeye Lissu ndiye ubunge ummemshinda maana kapigwa BAN bungeni baada ya kukosa adabu (kwenda kinyume na taratibu za kibunge walizojiwekewa wabunge wenyewe, yaani sheria na kanuni halali za kibunge), na kibaya zaidi hata kama BAN ikiisha atarudi bungeni ila atashindwa kuwa mbunge kamili maama BOSI wao kawapiga mkwara wamuongope Dr. Tulia na kuwahimiza wakiiona tu sura yake waogope na kukimbia haraka sana kutoka bungeni.
 
Kati ya lissu na magufuli nani mshindwa....?ama kweli nyani haoni kundule.
 
Kiukweli maisha yamekuwa magumu japo anaongoza vizuri lkn kajisahau sana.
Sasa biashara haziend hasa weny hotel na mabar. Wanafunga tu. Najua utabisha sana lkn kwa uhalisia maisha yamekuwa magumu.
Sasa hata haliposema ajira baada ya miez 2 nahic urifurahi sana
Okay it is very true nami nimesikia hivyo ila kihistoria hamna mabadiliko mazuri yasiyokuwa na maumivu. Huu ni mwanzo tu na nia ni kurekebisha utendaji nk. Kuhusu kutoajiri kwa miezi miwili mimi kinifurahishe nini? Labda ungesema sababu za kusimaisha ndizo zinaweza kunifurahisha kwani naamini ni za kujenga. Kuna mambo mengi ambayo yamekaa vizuri na mengine yatafuata! Ni muda tu ndio tuvute subira!
 
Back
Top Bottom