Lissu: Urais umemshinda Magufuli

Lissu: Urais umemshinda Magufuli

Sasa habari kama hii ina mchango gani hapa JF!
Ulipaswa ulete arguments za Lissu ili watu waelewe na kujadili, huku nako udaku ushaanza kuwa mwingi!
Usisubiri kutafuniwa kila kitu .
 
ila kila mara anaongea maneno yanayoonyesha kujutia urais, kuna kipindi aliongea na Pengo na kusema anatamani saa nyingine asingechukua form, juzi alipokuwa anakabidhiwa ripoti ya uchaguzi na Lubuva alisema anatamani urais ungekuwa ni awamu ya miaka 5 tu kwa sababu ya maneno ya watu.
Mimi naona kweli anafanya kazi, anatamani sana nchi isonge mbele haraka ila ilikuwa wrong kwake kuchukua urais,

angekuwa chini ya rais, mtu ambaye anaweza kuchora ramani za maendeleo, diplomatic na anayejua ku deal na criticism za kisiasa kitaifa na kimataifa, kisha yeye akawa kwenye nafasi ya kiutendaji iliyopo chini ya huyo mtu

urais ni nafasi ya kisiasa, unahitaji mtu mwenye temperament iliyo stable, diplomacy nzuri, mwenye calculation za mbali, na mvumilivu,

kwenye dunia ya leo mtu huwezi ukawa una sema eti hutaki wanaokukosoa eti tufanye kazi,
dunia ya leo media zimejaa, hata ukifungia mikutano bado wapinzani wanapewa coverage na vyombo vya habari, social media kama forums, facebook, YouTube Twitter n.k pia zinatumika sana na wananchi na wanasiasa wa upinzani wanazitumia, je utazuia pia media zote hizo kwa sababu hutaki kelele?

siku hizi kama huwezi deal na criticism bora usiwe mwanasiasa kwa kuwa huwezi kuzima, ni miezi 8 tu ila mtu keshaanza kutweta...tuone

huyu anataka viwanda viote kama uyoga, kwa kupiga marufuku bidhaa za nje kama sukari, kuongezea kodi bidhaa za nje kama nguo na mafuta ili tununue vya ndani wakati viwanda vya ndani vipo usingizini

Salute to one among few great thinkers! You got nothing but bull's eye.
 
MAGUFULI kipindi cha kampeni alisema akiingia madarakani tatizo la umeme litakuwa historia. Akatoa sababu kuwa Tanesco wanakata umeme ili kumhujumu, tena akasema umeme ukikatika hovyo Waziri mwenye dhamana anamtimua. Leo miezi 7+ tatizo liko pale pale.
 
Hapo si kweli,nadhan umemhukumu bila rejea,rais anafanya kazi nzuri sana,tabu ya watanzania ni kuishi kwa mazoea
 
bado mapema kwa sasa anaunda muundo wa serikali yake kabla ya kuanza ku take off
 
Nadhani umefika wakati TANZANIA DAIMA lifungiwe kabisa...lifungiwe kama lilivyofungiwa MAWIO...Baadhi yetu tumechoka na kauli za 'kihuni' na uchochezi...
Sampuli yenu mpo wengi sana!ila kwa dunia hii mtakwama.
 
Dunia ya Leo yenye social media like Facebook, WhatsApp, Jamii forum, magazeti kibao, redio kibao siyo lzm uandamane au kufanya mkutano ndio ufikishe ujumbe kwa jamii.

Unaweza kuongea kwenye redio tu kila MTU akasikia ujumbe wako.

UKAWA kuweni wabunifu
Nashauri na mkutano wa ccm unaokuja tufanye kwa kutumia Facebook au WhatsApp mbona social media zipo nyingi.CCM tuwe wabunifu
 
Sampuli yenu mpo wengi sana!ila kwa dunia hii mtakwama.

Unajidanganya...kamwe hatuwezi kukwama...ila nakuthibitishia jambo moja, and you should mark my words...WACHOCHEZI WOTE MTAKWAMA...Dunia ya sasa haitaki uchochezi, ukiwa mchochezi ni lazima ukwame...Ndiyo maana nchi zote au niseme karibu zote zimeachana na masuala ya upinzani wa Tanzania...Kwanini nasema hivyo, kwa kuwa wameona nyie wapinzani hamna sera, hamtaki maendeleo, mnachochea vurugu...Nchi za ulaya hazitaki mahali kwenye vurugu...ofcourse wamewaacha kwa sababu za kiuchumi...Wapinzani you have nowhere to go...nyie ni Watanzania kama ilivyo kwa watanzania wengine ambao hawako upinzani...kutamka maneno ya uchochezi kama eti JPM ameushindwa Urais huo ni uchochezi....kusema hivyo ni 'kuvimbiwa' uhuru wa kutoa maoni...Upinzani wa Tanzania utafanya jambo la maana ikiwa utakaa chini na kujitafakari...kususia bunge hizo siyo mbinu muafaka za kuiondoa CCM...wabunge wa upinzani kufunga midomo yao na makaratasi siyo mbinu nzuri za kuiondoa CCM madarakani...wapinzani kuwa na lengo la kuandaa maandamano nchi nzima eti kumshitaki JPM kwa wananchi ni mbinu zilizopitwa na wakati ambazo ni kutaka kuleta civil disorder...Upinzani uchukue hatua kwa kuwashawishi Watanzania kwanini CCM imeshindwa kuleta maendeleo baada ya miaka 50 au zaidi ya uhuru...lakini mbinu za ushawishi haziwezi kuwa zile za kususia bunge na kufunga midomo na makaratasi au kuandaa maandamano ya 'kumshtaki' JPM kwa wananchi...
 
wanaosema rais ameshindwa wao wameweza lipi??huyo lissu inamaana yote aliyoahidi katekeleza??
Hivi unadhani mbunge wa upinzani anatekeleza ahadi zake kwa pesa yake ya mfukoni auu. Kushindwa kutekelezwa kwa ahadi za wabunge wa vyama vyote ni kufeli kwa Raisi. Ndio maana tunapinga NS Tulia kuitetea serikali badala ya kuliongoza bunge li simamie serikali kwa manufaa ya wananchi. Nashangaa sana watu kushabikia vyama bila kujali maslahi ya Taifa. Binafsi nili mkubali sana JPM ila hili la kijfanya malaika kila analo amua ni sawa sikubaliani nalo hata kidogo.
 
Magufuli is the right president that Tanzanians wanted in this particular time. The Lisu's auguments are baseless and are polically motivated. The guy and his fellow kind of politicians should leave the president to execute his presidential duties accordingly. What our president is doing is actually what a clean, focused and a determined president expected to be doing and not otherwise.
So I advice Hon. Lissu to seriously start working hard in his Singida East constuency or else come 2020 Njau is our new MP. You will tell me.
 
Miongoni mwa kitu kibaya tulichorisishwa Watanzania ni kushabikia vitu visivyo na tija...

Rais Uhuru Kenyetta aliwaahidi wakenya ajira wakati wa kampeni zake na baada miezi 6 tangu kuapishwa kwake akawa amepunguza tatizo la ajira kwa asilimia 28.

Ebu angalia Kwa Mkuu wa Kaya wetu sasa...

Serikali haina vision yoyote ya kiuchumi kitutoa hapa tulipo,bajeti imepitishwa je kuna mkakati wowote wa kutukomboa kiuchumi????

Hakuna nchi hapa duniani iliyowahi kupata maendeleo kwa kuwa na viongozi wanaoigiza kama hapa kwetu.

Tuendelee tu kumshabikia lakini nawahakikishieni mwisho wake mtauona jinsi utakavyokua.

Natamani hata Comrade Kenyetta aje aongoze Tz walau kwa siku 60 tu.
 
Habar Jf mm naona tusihukum mapemaa kwan ndio kwanza kazi imeanza kwa jpm..chamsing ni ashauriwe aachiee demokrasia na ashirkiane na stakeholdrs wengiine ktk kuleta maendeleo ya taifa...Mungu ibarki Tanzania
 
Back
Top Bottom