Lissu: 'Time limit' kwenye uongozi ni anasa

Lissu: 'Time limit' kwenye uongozi ni anasa

Makosa mawili hayahalarishi makosa... ukomo wa muda huondoa tabaka fulani kushika wadhifa fulani mpaka kifo... hayo ni maisha ya nchi za kifalme kitu tulicho kiacha kuanzia kwenye katiba mama. CCM pamoja na utaratibu wao wa Rais kuwa Mwenyekiti wa chama bado wana time limit.. ila ACT na ninyi time limit kwenu ni "anasa" tena anaezungumza hivyo ni nguli wa ukosoaji.
Kauli hiyo inadhihirisha hata umakamu wake ni timeless mpaka kifo au aamue kwa kivuli cha uchaguzi.
Inajaribu kupunguza msigano kati yake na mwenyekiti kuwa amerejea kugombea uenyekiti..
Watetezi wa ujinga kisa ni Tundu kaongea endeleeni na ushabiki.
Unapoandika ukomo wa muda huondoa tabaka fulani kushika madaraka mpaka kifo, unazidi kuonesha usivyojua unachotetea, wala hujui maana ya maneno unayotumia kutetea kile unachokiamini.

Uchaguzi unapofanyika, wanakuwepo wagombea tofauti toka sehemu tofauti, hawa wanapigiwa kura na wanachama wao, mshindi anapatikana kwa wingi wa kura toka kwa wanachama wote, bila kuwepo matabaka kama unavyoandika wewe..

Kwanza nikufundishe; Chadema hakuna matabaka, wanachama wote ni sawa, kile chama ni public property, mtanzania yeyote mwenye sifa za kujiunga anaruhusiwa kufanya hivyo, wakati wowote atakapoamua akifuata taratibu.

Wewe kwa ujinga wako [japo unajiona mjuaji] ndio unaona pale kuna matabaka, kisa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti, hukumbuki kura anazopigiwa huzipata toka kwa wajumbe tofauti nchi nzima, sasa hayo matabaka unayoandika yanatoka wapi?

Mwisho, Mbowe ameshasema hataendelea kuwa kiongozi Chadema, mwaka huu ndio mwisho wake, sasa unapoandika kauli aliyoitoa Lissu amelenga kupunguza msigano kati yake na Mbowe ili asionekane amerudi kugombea uenyekiti, haya yako ni mawazo ya mjinga tu, asiye na taarifa yoyote muhimu.
 
Mbona kila wakati wanajitokeza watu kutaka kugombea mnaishia kuwabatiza majina ya wasaliti na kuishia kuwatimua. Hao mnaowaeleza kuwa sumu haionjwi sio watu ama. Hata huyo Tundu Lissu ukweli anaogopa kutamka na hizo kauli ni za kiuoga. Juzi alisema yeye hana mpango wa kugombea uonyekiti, Jana anasema time limit ni anasa. Hizi kauli zote ukizipima zimejaa uoga, ukweli anaogopa kugusa palipo na mkono wa mwenyekiti, na uzuri anajua what happens unapojaribu hilo.
Chacha Knows, Zitto knows, yule dogo( In Halima' Voice) wa Mtwara knows na Mzee Sumaye knows!
Mbowe ameshasema hatogombea tena uenyekiti, sasa Lissu aogope kitu gani kusema anautaka uenyekiti?

Lakini, kama yeye akisema leo, halafu mwingine aseme kesho, na mwingine afuatie kusema kesho kutwa, huoni hiyo itaanza kuleta vurugu chamani, na kuharibu mipango ya chama chao, hasa wakati huu wakipigania mambo ya msingi kama Katiba Mpya?

Tatizo lenu mna upeo mdogo, na bahati mbaya, mnalazimisha mawazo yenu mafupi ndio yawe mawazo ya wale wanaojitambua, hili mnalotaka halitawezekana, labda mkajaribu kwa vyama vingine.

Mwisho, Sumaye na Mwambe kuondoka Chadema, wale waliondoka kwa aibu zao, na Zitto nae aliondoka kwa aibu zake baada ya vikao vyake vya usiku na "baba yake JK" kushtukiwa, punguzeni mawazo potofu mkijadili mambo ya msingi, kama una ushahidi Wangwe alifanywa nini na Mbowe, weka hapa, au nenda mahakamani, sio kelele zenu zisizoeleweka kila siku.
 
Nashngaa watu wanaomuona huyu jamaa ana akili. Kwahiyo kama tu kwenye ka chama hawana watu wa kuongoza, watu wa kuongoza Nchi watawatoa wapi!
Tofautisha kuongoza chama cha upinzani na serikali, vyama vya upinzani kiongozi anafungwa,jela,ananunuliwa,anauawa,anapigwa risasi.. hivyo kupata kiongozi atakae pitia yote hayo na bado akawa imara,sio rahisi. Ondoa ujinga kichwani mwako acha uchawa. Think for yourself
 
Hiyo akili ya kujua hayo ataitoa wapi
 
Tofautisha kuongoza chama cha upinzani na serikali, vyama vya upinzani kiongozi anafungwa,jela,ananunuliwa,anauawa,anapigwa risasi.. hivyo kupata kiongozi atakae pitia yote hayo na bado akawa imara,sio rahisi. Ondoa ujinga kichwani mwako acha uchawa. Think for yourself
Alooo kama hizi ndo akili basi naomba mimi nibaki na hizi hizi zangu. Kama kuongoza ka chama kasikozidi wanachama laki ndiyo changamoto, ila kuongoza taifa la watu milioni sitini ni kazi nyepesi basi naanza kuelewa kwanini hii nchi haopigi hatua. Watanzania hatuna akili, hasa wewe uliyotoa hiyo hoja hapo juu
 
DnooJ
Mbowe ameshasema hatogombea tena uenyekiti, sasa Lissu aogope kitu gani kusema anautaka uenyekiti?

Lakini, kama yeye akisema leo, halafu mwingine aseme kesho, na mwingine afuatie kusema kesho kutwa, huoni hiyo itaanza kuleta vurugu chamani, na kuharibu mipango ya chama chao, hasa wakati huu wakipigania mambo ya msingi kama Katiba Mpya?

Tatizo lenu mna upeo mdogo, na bahati mbaya, mnalazimisha mawazo yenu mafupi ndio yawe mawazo ya wale wanaojitambua, hili mnalotaka halitawezekana, labda mkajaribu kwa vyama vingine.

Mwisho, Sumaye na Mwambe kuondoka Chadema, wale waliondoka kwa aibu zao, na Zitto nae aliondoka kwa aibu zake baada ya vikao vyake vya usiku na "baba yake JK" kushtukiwa, punguzeni mawazo potofu mkijadili mambo ya msingi, kama una ushahidi Wangwe alifanywa nini na Mbowe, weka hapa, au nenda mahakamani, sio kelele zenu zisizoeleweka kila siku.
denooJ wewe ni muandishi na mjenga hoja mzuri ila kwa alichosema Lisu hakiteteeki yeye ni mwanasiasa mzoefu lazima ajue namna ya kujibu maswali ya mitego kama haya huwezi kusema anasa hata siku moja, kwenye hili kateleza. Kulikuwa na njia bora zaidi ya kujibu kuliko kutumia neno anasa. Halafu huwezi kutenganisha katiba ya chama na ya nchi maana kama ya nchi mbovu tunatarajia chama kinachotaka kufanya mabadiliko kiwe na katiba bora zaidi waswahili wanasema ihsani inaanzia nyumbani.Unaweza kutetea kwa ugumu wa kuendesha siasa za kifraki ila sio kwa kutumia anasa
 
Kwanza unatakiwa uifahamu chadema, mgombea urais au rais sio lazima awe m/kiti wa chama.

Time limit sio kigezo kinachomfanya Mbowe kuendelea kuwa m/kiti kwani kila term inapomalizika uchaguzi ktk nafasi zote za uongozi unafanyika na Muheshimiwa Mbowe siku zote anaibuka kidedea

Tunataka kuona na ccm kuwa na wagombea ktk nafasi ya uwenyekiti wa chama

Hujajibu maswali nlokuuliza unakimbilia ya ccm
Katiba ya chadema haikuwahi kua na time limit?
Ikitokea wanapewa nchi hawawezi kukiondoa kipengele cha time limit kwa kisingizio cha kujenga nchi na kukosa mtu makini na waaminifu kwa taifa?
Halafu mimi sio mwana ccm ila najua hua kuna mabadiliko ya M.Kiti
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 ITV leo usiku (tarehe 06-02-2023 09:00PM) kwanini watu wanahisi hakuna Demokrasia ndani ya chama chake hasa katika nafasi za Uongozi wa juu amesema kwamba demokrasia ipo lakini hakuna "time limit" kwa kuwa ni jambo hili ni anasa kwa mtizamo wa kichadema.

Anasema chama chake kutokana na changamoto ya kuwapata viongozi wanaofaa imeona ni bora kutokuwa na "time limit".

Wadau mnaonaje, kweli "time limit" kwenye uongozi ni anasa?

Nawasilisha,

Article.
"Term Limit" sio time limit; uongozi sio mdahalo! Nyau we!

Sent from my Nokia G21 using JamiiForums mobile app
 
Inaelekea Chadema wakishika dola, mazuri ya chama chao, watayahamishia katika nchi, yaani wataondoa anasa ya time-limit ktk katiba ya nchi ili kiongozi anayetokana na chama chao atawale bila ukomo wa vipindi.

Hawa ndo Chadema, Zilongwa mbali, zitendwa mbali
 
Hapo sasa mapovu yatawatoka
Wewe mwenzetu siyo mwananchi wa Tanzania? Unadhani wanao umizwa na uongozi mbovu ni viongozi wa CHADEMA ambao unasema watatokwa na mapovu ama sisi wananchi wa kawaida ukiwemo wewe? Jaribu kukua mzee,ID yako ni kongwe mnoo hapa JF
 
Ikitokea ccm wakabadili katiba ya chama na ya nchi kumruhusu mama Samia kua rais na mwenyekiti wa kudumu nayo itakua ni demokrasia?
Kwa hiyo itakuwa ni nini. Unajua maana ya kemokrasia? Suala la kuondoa ukoma lipo kwenye katiba ya Chadema, waliamua wanachadema bila kushurutishwa na mtu. Suala la katiba ya nchi ni watz na mambo ya CCM ni CCM.

Jifunze kwanza maana ya demokrasia ndio urudi tujadili
 
DnooJ

denooJ wewe ni muandishi na mjenga hoja mzuri ila kwa alichosema Lisu hakiteteeki yeye ni mwanasiasa mzoefu lazima ajue namna ya kujibu maswali ya mitego kama haya huwezi kusema anasa hata siku moja, kwenye hili kateleza. Kulikuwa na njia bora zaidi ya kujibu kuliko kutumia neno anasa. Halafu huwezi kutenganisha katiba ya chama na ya nchi maana kama ya nchi mbovu tunatarajia chama kinachotaka kufanya mabadiliko kiwe na katiba bora zaidi waswahili wanasema ihsani inaanzia nyumbani.Unaweza kutetea kwa ugumu wa kuendesha siasa za kifraki ila sio kwa kutumia anasa
Unaposema kile alichosema Lissu hakiteteeki, umepima kwa standard zako zilizothibitishwa na mamlaka gani yenye jukumu hilo inayotambulika uwepo wake kisheria?

Kama jibu huna, basi kwangu hoja za Lissu zinateteeka, na hata kwa hiki ulichoandika hapa, nitamtetea pia.
 
Back
Top Bottom