Lissu: 'Time limit' kwenye uongozi ni anasa

article

Senior Member
Joined
Sep 10, 2016
Posts
192
Reaction score
349
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 ITV leo usiku (tarehe 06-02-2023 09:00PM) kwanini watu wanahisi hakuna Demokrasia ndani ya chama chake hasa katika nafasi za Uongozi wa juu amesema kwamba demokrasia ipo lakini hakuna "time limit" kwa kuwa ni jambo hili ni anasa kwa mtizamo wa kichadema.

Anasema chama chake kutokana na changamoto ya kuwapata viongozi wanaofaa imeona ni bora kutokuwa na "time limit".

Wadau mnaonaje, kweli "time limit" kwenye uongozi ni anasa?

Nawasilisha,

Article.
 
Time limit kwa upande wangu kuna muda ina faida na kuna muda naona hasara nyingi sana kwake.

Hivyo kwangu mimi time limit haina maana, akipatikana kiongozi bora ni vyema kuendeleza ubora wake kwa muda kadhaa mbele na sio kupata kizingiti cha time limit.
 
Nashngaa watu wanaomuona huyu jamaa ana akili. Kwahiyo kama tu kwenye ka chama hawana watu wa kuongoza, watu wa kuongoza Nchi watawatoa wapi!

..Nchi ni kubwa kuliko chama, hivyo watatafuta watu wa kushika nafasi mbalimbali toka nje ya chama.

..Mfano mzuri ni Mama Samia ambaye baada ya kukosa watu ndani ya Ccm ameamua kuteua wasanii kujaza nafasi mbalimbali.
 
Lisu kadai kwamba Chadema wameona time limit ni lazima kwa kuwa wana changamoto ya viongozi.Eti kwao ni anasa.Yaani viongozi waliopo ni irreplaceable?

Hoja hii inadhihirisha kwamba Chadema hawana viongozi wa kuaminika wa kutosha kuwabadili waliopo au ni kivuli cha kutetea udikteta?

Be the judge!
 
1. Ndani ya miaka kumi kiongozi anakuwa na experience ya kutosha na hivyo kumuondoa inakuwa si sawa ilhali ndio kwanza anaanza kutumia experience yake

2. Kutokana na upungufu wa watu wenye vigezo ikawa ni sahihi kuondoa ile time limit

Nilikuwa nadokeza tu Ila nawaacha wafu mzikane
 
Siasa sio lain hivo
 
Nashngaa watu wanaomuona huyu jamaa ana akili. Kwahiyo kama tu kwenye ka chama hawana watu wa kuongoza, watu wa kuongoza Nchi watawatoa wapi!
Kama huna hizo akili utazionaje kwa mwingine?
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 ITV leo usiku (tarehe 06-02-2023 09:00PM) kwanini watu wanahisi hakuna Demokrasia ndani ya chama chake hasa katika nafasi za Uongozi wa juu amesema kwamba demokrasia ipo lakini hakuna "time limit" kwa kuwa ni jambo hili ni anasa kwa mtizamo wa kichadema.

Anasema chama chake kutokana na changamoto ya kuwapata viongozi wanaofaa imeona ni bora kutokuwa na "time limit".

Wadau mnaonaje, kweli "time limit" kwenye uongozi ni anasa?

Nawasilisha,

Article.
Kaamua kua wazi kabisa hata yeye hana sifa ya kua kiongozi wa chama wala kuongoza nchi
 
Back
Top Bottom