Tundu Lissu akiwa Alabama nchini USA wakati anazungumza na watanzania waishio huko ,ameulizwa swali kama Freeman Mbowe alihusika kwa namna moja au nyingine kutokana na kupigwa risasi kwake, akawajibu hata yeye hajui huenda alihusika kweli!.
Lissu ametaka uchunguzi huru wa kuwachunguza Mbowe, Makonda ,Magufuli kama wamehusika kwenye tukio lake la kupigwa risasi.
My take:
Kitendo cha Lissu kutaka hata Mbowe achunguzwe kitakuwa mwiba mchungu kwa BAVICHA wanaopenda kumkingia kifua Mbowe ,huku wakimtaka Lisu agombee urais wa Tanzania.
Kama kweli Mbowe atachunguzwa kama Lisu anavyotaka ,basi huenda yakaibuka mengi na hata hatima ya mauaji ya Chacha Wangwe ambayo Mbowe amekuwa akihusishwa bila uchunguzi kwa miaka mingi sasa.
Sent using
Jamii Forums mobile app