Lissu awaalika Wananchi wa Dar na mikoa ya jirani kufika Mahakamani Kisutu kwa wingi tarehe 26 kusikiliza shauri lake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,958
141,951
Mgombea urais wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu amesema atahudhuria mahakama ya Kisutu kujibu kesi inayomkabili siku ya tarehe 26/08/2020 baada ya kuwa amekamilisha matakwa yote ya kisheria kule Tume ya Uchaguzi.

Tundu Lisu amesema kesi yake ni ya wazi (open case) hivyo amewaomba Wanachama wa CHADEMA na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza mahakamani siku hiyo.

Chanzo: Star TV Habari!
 
Akiongea na waandishi wa habari, leo ndugu Tundu Lissu ameelezea kirefu taarifa za njama za kumuengua kugombea kupitia kumfungulia mashitaka mapya ya papo kwa papo pindi akienda kusikiliza mashauri yake ya zamani.
Lissu amesema taarifa za uhakika walizo nazo kutoka katika vyanzo vya taarifa ndani ya serikali ni kuwa, mpango uliosukwa ni kuwa tarehe 26 imechaguliwa makusudi kwa sababu tarehe hiyo ndiyo tarehe pia ambayo kama kuna mapingamizi huko NEC ya kugombea, basi mgombeaji anapaswa awepo kuyajibu. Hata hivyo kwa upande wa Lissu tarehe hiyohiyo amepangiwa awepo mahakamani kuendelea na mashauri yake. Lissu amesema taarifa walizonazo ni kuwa akifika mahakamani atasomewa mashitaka mengine mapya ya papo kwa papo, kunyimwa dhamana kisha kesi kuahirishwa tarehe ya kutajwa na kisha kunyimwa dhamana ili asiweze kwenda NEC kujibu mapingamizi yoyote yatakayoibuliwa na hivyo kuwa kuondolewa katika kugombea!

Lissu amesema, kuwa kesi za jinai ni kesi za hadhara ambapo umma unaruhusiwa kwenda kuzisikiliza, hivyo anawataka wananchi wa Dar na mikoa ya jirani wahudurie mahakamani siku hiyo!

Pamoja na shauri lake kutajwa tarehe hiyo, Lissu hajawwka wazi msimamo wake kuwa Je atakwenda yeye binafsi au hatakwenda, lakini kwa jibu alilolitoa kwa mwandishi wa habari ameonyesha kuwa Jambo la kugombea ambayo ni haki yake ya kikatiba analipa kipaumbele zaidi.

Kwa habari zaidi tazama video hii:

 
Akili kubwa hii!!

Anyway,ili waanguke,ni lazima wakose busara,maarifa na zaidi wawe na viburi, na pia waendelee kuyatenda haya kabla ya wao kuanguka.

Hata Yesu,kutokana na kiburi cha Wanadamu, ilimpasa kupita katika kipindi kigumu kabla ya kukamilisha kazi aliyokuwa ametumwa.

Tukumbnuke tu Mungu ni yule yule na bado anatenda yale yale hata kwa wanadamu wa leo.

Muda utathibitisha.
 
Back
Top Bottom