Lissu alivyomhoji shahidi leo- kesi Singida

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
MAHOJIANO NI MENGI, ILA JAJI AMEINGILIA KAATI KUWEKA MAMBO SAWA. Wakili wa walalamikaji wa CCM anaomba akaongee na Mashahidi Nje, jaji amekataa na mahojiano yakaendelea.

Jaji: Akasirishwa na wingi wa mashahidi ambao hawaongei vitu vya msingi (irrelevances)

Tundu Lissu: Je unamfahamu Cleti kidamwina?

SHAHIDI: NamfahamuTundu

Lissu: Je unamfahamu kwa kuwa anaishi kijiji cha Unyaghumpi karibu na making? NDIO

TUNDU Lissu: Ulikuwa wakala wa kituo cha shule ya msingi makiungu namba 1.NDIO.T. L. Mwambie jaji ulifika katika Kituo saa ngapi na uliondoka saa ngapi

Sh. Nilifika saa 12, na zoezi la kupiga kura lilianza saa 2, asb, na nilitoka saa 2 usiku.

T.L. Ni sahihi nikisema kwamba ulitoka saa mbili usk baada ya matokeo ya kituo chako kutangazwa? Ndio.

Ni sahihi pia nikisema kwamba kati ya saa 12 asb na saa 2 ulipotoka ulibaki muda wote ili kulinda maslahi ya mgombea wa ccm. NDIO. SIKUTOKA, MAWAKALA WOTE WALINIZUIA NA HIVYO NILIBAKI NDANI MUDA WOTE, KILA NILIPOTAKA KUTOKA WALINIZUIA.

T.L. Je ni sahihi nikisema kuwa uliona kila kitu 12:00 hadi 2;00 usiku kwa kuwa ulikuwepo ndani muda wote? NDIO.

Je ni Sahihi nikisema kuwa kura zilianza kupigwa saa 1:00 asb? HAPANA.

Zoezi lilianza saa mbili. Kwa vile hukutoka, hivyo ni sahihi kusema kuwa wewe ulipiga kura katika kituo ulichojiandikisha? NDIO Mweleze jaji: Kama ulimwona Cleti kidamwina kituoni mwako.

SHAHIDI: SIKUMWONA

SHAHIDI; ANAPANDISHA MAJINI, ANAPANDISHA MAPEPO, KWIKWI KIBAO

LISSU nauliza: Upo Salama Ulipewa mafunzo ya uwakala wa CCM? NDIO: MAFUNZO TULIPEWA. Mweleze jaji hayo mafundisho mlipewa na nani? Tulipewa na makamanda wa CCM.

Mweleze jaji, kama katika maelezo hayo mlipewa maelekezo kwa mawakala ambao wamepangwa kituo tofauti na kituo alichojiandikisha? Ndio.

Unapoondoka kituo chako unapewa kikaratasi ili ukifika huko ili uweze kupiga kura.

T. L. Lissu anamwonyesha Shahidi picha yake, na kituo alichopigia kura, shahidi anakataa kituo alichopigia kura.

SHAHIDI: Picha ni ya kwangu, majina ni yangu. Ila waliopanga haya ni kazi yao, haya hayanihusu.

T. L. Mbona ulisema wewe hujui kusoma na kuandika? Una Cheo gani katika Chama? SHAHIDI: Katibu wa CCM: kata ya MungaaKwa hiyo ni sahihi mimi nikisema kuwa wewe ni mwana CCM damu damu, SAHIDI: NDIYO DAMU DAMU.

Mwambie Jaji mlilipwa posho na Chama chenu kwa kuwa mawakala? SHAHIDI: HATUKULIPWA. Ni kweli au si kweli kwamba kila wakala wa CCM alilipwa Sh 5000? SHAHIDI: SIJUI.

Mweleze Jaji kama uliletewa Chakula siku ya uchaguzi, SHAHIDI: NILILETEWA CHAKULA TOKA NYUMBANI KWETU, Je ni makosa wakala kuletewa Chakula na wakala wa Chama chake?

SHAHIDI: SIO KOSA.Je ni kosa wakala kuletewa chakula na Mgombea wa Chama chake? Sio kosa.Tunakubaliana kwamba, wakala anatakiwa awe muda wote kituoni? Je ni kosa kwa Chakula kuletwa kwa gari piki piki au baiskeli? SHAHIDI: sio kosa.

T. Lissu Je ni kosa au sio kosa, kununua chakula hicho mahakamani na kasha kupelekwa kwa mawakala?

Shahidi anasema: Tundu Lissu aliingia na jezi za Chadema kwenye chumba cha kupigia kura. Hili halikuwepo katika mashtaka.

LISU: Kama hayo unayosema ni ya kweli, Kwanini hao walionishtaki ambao wanasema waliniona, mbona hawajaandika hapa katika mashtaka haya?

SHAHIDI: kwenye kituo changu ulikuja umevaa.Waleta mashataka, wanasema wameniona kituo Namba Moja sikuvaa, wewe unasema nilivaa nilipokuja kituo cha pili, je nilivalia kituo gani? SIJUI:

T. Lissu Unajua Chakula hicho unachodai kilinunliwa kililipiwa na nani? SIJUI.Je ni kweli au si kweli kwamba ukiwa wakala, ukiona kosa linatendeka, na ujaze fomu ya malalamiko namba 14, je nisawa? NDIO

Mwambie jaji, kama uliniona nimeingia nimevaa jezi ya Chadema kama ulijaza fomu ya malalamiko.SHAHIDI: nilijaza, ila walipokuja watu wa halmashauri walichukua zote.

Fomu uliyojaza ulilalamikia nini?

SHAHIDI: KWANZA; Mheshimiwa Mbunge na Diwani kuleta Chakula kwa mawakala, nililalamikia kuzuiliwa kutoka kituoni na mawakala wa CHADEMA hata kwenda kujisaidia., nililalamikia na zoezi la kuhesabu kura.

Jibu Maswali haya:Ulisema wewe hujui kusoma, je uliwezaje kuandika? SHAHIDI: SIWEZI KUSOMA BILA MIWANI? Macho yangu madogo halafu hayaoni vizuri.

Je ni kweli au si kweli kila wakala anayejaza fomu ya malalamiko anajaza nakala mbili? Shahidi: Sijui

Unamfahamu Mathew Cosmas Mnyambii? NAMFAHAMU Huyu ni Mwenyekiti wa CCM, na alikuwa Wakala. Kama wewe unadai fomu yako ya malalamiko ilichukuliwa na wakusanya matokeo, Mbona ya huyu ambaye ni kiongozi wako iliachwa?

SHAHIDI: SIJUI.Je ni sawa au si sawa, nikisema ukiwa wakala unasimamia kura za mbunge, rais, na diwani wote wa ccm? NDIO.

Vile vile mawakala wengine walisimamia wagombea wa Vyama vyao? NDIO.Mweleze jaji? Nani alishinda Udiwani kata ya Mungaa? Anaitwa nani? Wa Chama gani? JAJI: Nani? Mbona hujibu?

SHAHDI:MATEO Kilongo wa chadema.

Mweleze jaji, wewe au wengine wa CCM kwanini hawakupinga matokeo ya udiwani wa kata ya Mungaa? au mpiga kura yeyote aliyepnga ushindi wa Diwani wa kata ya Mungaa – CHADEMA?

SHAHIDI: hakuna.Matokeo ya Udiwani yalikuwa halali au hayakuwa halali ndo maana hajalalamikiwa?

SHAHIDI: SIJUI.

Lissu: Diwani ameshinda, kwa mawakala wale wale,waliosimamia je imekuwaje mlipinga matokeo ya Mbunge mkaacha ya Diwani? Nani alishinda kwenye kituo chako kati yangu na Jonathani Njau.

SHAHIDI: SIJUI

Wewe unajua sheria za uchaguzi? SIJUI?

Umejuaje kama matokeo hayakuwa halali?

Unajua Njau CCM alipata kura gani katika kituo chako? SIJUI.

Walioshitaki wanasema walipoona walishindwa walikaa na vikao vya CCM kujadili ili wafungue ulishiriki? HAPANA.

Mengine sijui.

Mweleze jaji, nani amekutuma kuja kutoa ushahidi hapa! Chama change kimenileta. Mweleze jaji wamekupa shilingi ngapi?

Hawajanipa pesa.TUNDU LISSU AMEMALIZA MASWALI KWA SHAHIDI SOPHIA. Wakili wa walalamikaji, akamwomba tundu Lissu amsaidie kujua baadhi ya kanuni za uchaguzi,Tundu Lissu akasema sio wajibu wangu, alipaswa kuja mahakamani akiwa amejiandaa.

JAJI Anawasuluhisha,anamwomba Lissu awe anawasaidia wakikwamba. Lisu akasema SAWA!

Kumetokea mgongano kati ya wakili wa walalamikaji; CCM, na jaji Mzuna Moses baada ya kuombwa kuwa wanaleta mashahidi wanaozungumza mambo yasiyo ya msingi irrelevant. jaji amewapa walalamikaji CCM muda watoke nje wakajipange upya.
 
nilisema kesi za chadema tutayaona ya firauni mwaka huu
walitakiwa wajipange kuangalia nani wa kumpeleka mahakamini loh
 
Hivi kesi ya LISU nayo kuna wakili wa upande wa utetezi au ameuvaa mwenyewe? maana naona alivyompeleke huyu shahidi ni putaputa!
 
Lisu kiboko sizani kama ana haja ya kuweka wakili wa kumtetea. Chadema wana jembe pale kwenye mambo yote ya sheria. Namkubali sana Lissu naamini hukumu ya kesi yake itakuwa kama ya jimbo la ilemela Mwanza. Peoples!!!!!!!!!!!!
 
ccm HAWAJAWAHI KUWA NA WATU MAKINI KUANZIA NGAZI YA KAYA HADI HALIMASHAURI KUU...ANGALIENI MAKATBU WAO TU WANAOWACHAGUA KUWA NDIO WENEZI ANZIA MAKAMBA, NA TENA NNAUYE...NI VIMEO ILE MBAYA. NDIO SHAHIDI! HUYO SI ATAKUWA MAVI KABISA
 
Ahsante kwa update za Singida Mnyampaa Isango, umejitahidi sana sijui ulikuwa na kinasa sauti , ama spidi ya kuandika ni kali, professionalism (journalism) big up. Ila sina uhakika kama njau alihudhuria. huyo shahidi kama hajui matokeo ya kituo chake basi amebambikwa mzigo usio wake. mpe pole.
 
Asante sana senior issango kwa kutupatia updates! Watajuta kwa ku file hiyo petition mwaka huu!
 
hizi kesi very interesting! nadhani hawa jamaa makamba aliwapoteza kuwaambia wafungue mi-kesi bila kujipanga! wakili wao Masumbuko Lamwai yupo? kila zama na sheteni wake!
 
Wangefuta tu hiyo kesi kuliko kuendelea kuunguza raslimali zza taifa. Judge analipwa mamilioni, wananchi wanapoteza muda wao muhimu wa kufanya kazi wakati kesi yenyewe haina maana! Ccm bana!
 
Back
Top Bottom