MAHOJIANO= SHAHIDI WA SITA (SHAHDI WA PILI LEO)
SHAHIDI; Matheo Cosmas Mnyambii.
Wakili wa CCM anataka kujitoa katika kesi kwa kudai kuwa mashahidi wake wanatishiwa hapa hapa mahakamani. Hivyo anatoa taarifa kwa Jaji.
Shahidi ameombwa aeleze jinsi alivyotishiwa. (Lakini ukweli ni kwamba wakati shahidi huyu na wakili wake wamejifungia ndani kupika majibu, Tundu Lissu na wafuasi wake walikuwa nje.
JAJI: je unamfahamu aliyekutishia?
SHAHIDI: Simfahamu;
WAKILI WA CCM: mbona uliniambia unamfahamu.
LISSU: Naomba niseme: wakili wa walalamikaji alisistiza kuwa mashahidi wake wasijulikane. Na hajawahi kuwataja hapa mahakamani? Sasa wamejulikanaje hadi watishwe wakati hawakutajwa ni akina nani? Je waliomtisha ni watumishi wa mahakama? Maana ndio wenye majina
JAJI:aliyekutisha ni nani?
SHAHIDI. NI Yule Mwenye Shati Jekundu.
MWENYE SHATI JEKUNDU:
WAKILI WA UTETEZI: hapa hatuna nafasi ya kusikiliza malalamiko au vitisho vya shahidi, apeleke taarifa polisi, ila hapa awe huru kueleza ushahidi wake kwa kesi iliyomleta hapa.
JAJI: Ni kweli kwamba kila vitisho hupelekwa polisi, lakini malalamiko yanapoletwa hatuna budi kuyashughulikia. Ila nawaonya wasikilizaji wa kesi kama kuna mtu ana tabia hiyo aache
.
WAKILI WA WALALAMIKAJI: Muda wa uchaguzi ulianza saa ngapi?
SHAHIDI; Saa mbili.
WAKILI WA WALALAMIKAJI; Uliona kaitu gani cha kawaida?
SHAHIDI: Zoezi zima la Uchaguzi.
WAKILI; katika zoezi hilo uliona nini ambacho sio cha kawaida?
SHAHIDI; Niliona mawakala wa chadema wakigawiwa, maji, juice na biskuti.
WAKILI :Nani aligawa?
SHAHIDI: Mgombea Udiwani kupitia CHADEMA.
JAJI: DIWANI WA WAPI?
Shahidi: WA KATA YA Mungaaa.
PINGAMIZI: TUNDU LISSU anarejea aya ya 9 ya hati ya maombi, inataja waliohusika na hicho kinachoitwa kuwa ni rushwa ya Chakula, mdai anasema kuwa alilipia Chakula na usafiri, na anajulikana kama Cleti KIDAMWINA, HIVYO KUTAJA DIWANI WA MUNGAA SIO PLEADED KATIKA PETITION, na hivyo wajibu maombi na wakili wao wanafanya kazi ya uvuvi wa ushahidi kwa mambo ambayo hawakuyalalamikia. Hiyo inakiuka kanuni 23 ya kuendesha kesi za uchaguzi, inakiuka 147, kifungu kidogo cha 3 kinachowataka kuleta relevant facts kwa mambo wanayolalamikia, Tundu Lissu amewomba jaji, wakili wa walalamikaji na mashahidi wao waache uhuni wa kufanya uvuvi wa maelezo ya ndani ya mahakama, wajikite katika malalamiko waliyoyaleta tangu mwanzo, ambayo ndiyo yapo katika hati yamashtaka.
WAKILI WA MLALAMIKAJI Amekubali pingamizi, na hivyo kuomba shahidi wake aendee.
JAJI ANAKUJA JUU: Tulipoenda kupumzika tulienda kufanya nini?
WAKILI WA CCM, anasema mashahidi wametoka vijijini, hivyo anajieleza ovyo. Tunaiomba mahakama ituangalie.
JAJI: hatupo tayari kusikia kuwa hata vyama ambavyo havikushiriki uchaguzi eti nao walitoa rushwa. Muwe makini.
WAKILI WA CCM anaendelea.
Umesema kwamba, Chakula kiligawiwa, hebu rudia.
SHAIDI:Maji, biskuti na juice,
Nani alipewa?
Paskali hema, Onesmo Mohamed, na Lukasi Lusian
KWANINI UNASEMA HAWA WALIPEWA?
Walipewa Chakula kama mawakala wa CHADEMA.
Walikuwa wapi siku hiyo?
Ndani ya kituo cha shule ya msingi makiungu Namba 3.
Una kiingine unachotaka kueleza mahakama zaidi ya hicho?
Naweza kuongeza nje ya hicho
HAPANA: Sema yanayohusiana na hapa.
SHAHIDI. Chakula walichopewa kilionekana kuwa ni rushwa kwa kuwa mimi sikupewa.
WAKILI WA CCM TAYARI AMEMALIZA KUMHOJI SHAHDI WAO.
SASA TUNDU LISSU;
Ulijiandikisha kupiga kura?
NDIO.
T/L UNAWEZA KUNIONYESHA KADI YAKO YA KUPIGA KURA?
NDIO..... hii hapa
T/L Ulikuwa wakala wa CCM Kituo cha 3 makiungu?
NDIO.
T/LNANI likupangia kuwa wakala wa CCM katika kituo cha Makiungu 3?
Ni viongozi wangu wa CHAMA
T/L. Naomba kumwonyesha shahidi barua ya Mwenyekiti wa ccm 8/10/2010 yenye orodha ya majina ya mawakala..... Tundu Lissu anamwonyesha.
T/L. Shahidi unajua kusoma,
SHAHIDI; Ndio lakini mimi hapa sina miwani.
T/L. Nakusomea. Aliyepangwa na CCM katika kituo chako ni Ally Kiemi.
T/L shahidi: Je ni kweli au si kweli, kwamba wewe ulipangwa shule ya Unyaghumpi?
SHAHIDI: nilipangwa kule lakini viongozi wangu walipogundua kuwa ni mbali walibadilisha.
T/L. Kwa hiyo ulipangiwa Unyaghumpi ka katibu wako wa wilaya, ninyi mkaamua kubadilisha ukaenda Makingu.
SHAHIDI; NDIYO.
T/L. Ili uwe wakala, unatakiwa ule kiapo, kweli au si kweli?
SHAHIDI: Kweli.
T/L. Unapokula kiapo unakuwa na nakala mbili, moja anachukua msimamizi nyingine unabaki nayo, kweli au si kweli.
SHIHIDI; Kweli.
T/L Na ile unayobaki nayo ndio ushahidi wako kuwa wewe ni wako, kama unayo mpe jaji.
Shahidi: Nimeiacha Nyumbani.
T/L. Unataka tufanye maamuzi kwa kutegemea makaratasi yaliyoko nyumbani kwako?
SHAHIDI: ............... KIMYA....................
T/L. Ulipigia wapi kura?
SHAHIDI. Nilipigia Makiungu.
T/L. Unaweza kupiga kura hata hukupangiwa katika kituo hicho?
HAPANA.
T/L. Kuna kitu kinaitwa shahada ya Utumishi, ninachofahamu mimi, kama umepangiwa kituo ambacho hukuandikishwa, inabidi upewe shahada ili uweze kupiga kura.
SHAHIDI: Mimi nilikuwa MSIMAMIZI Kituo namba 3, na kura nilipiga kituo namba 2.
T/L, ulipiga kura saa ngapi?
SHAHIDI: kati ya saa 8 hadi 9
T/L kwa hiyo uliacha kituo ukaenda kupiga kura?
SHahidi: NDIYO NILIIACHA
T/L. Ulizaliwa lini?
SHAHIDI 1954.
T/L. Naomba shahada yako ya kupigia kura............. Shahidi anampa kadi ya kupigia kura
T/L. Mwambie jaji kama kadi yako kuna mwaka wa kuzaliwa, na kama mwaka uliotaja.
SHAHIDI: Sioni, kwa kuwa macho hayaoni
T/L. Mbona kadi yako haionyeshi mwaka wa kuzaliwa?
SHAHIDI: Sasa we unajua mwaka niliozaliwa mimi?, labda aliyeandikisha hakujaza. Mimi sijui, yeye ndiye alikosea.
T/L Wakati unaandikishwa 2004, ulisahamu mwaka wako wa kuzaliwa, leo baada ya miaka 8 tangu uandikishwe ndo unakumbuka mwaka wa kuzaliwa?
SHAHIDI HAJUI KAMA ALIZALIWA SINGIDA, SHAHIDI HAKUMBUKI KAMA ALIJIANDIKISHA, HAKUMBUKI KATA ALIYOTOKA, HAKUMBUKI HATA ALIYEMWAMBIA MWANDISHI KUWA YEYE ANATOKA MKOA WA SINGIDA.
T/L: Ulisema wewe ni Mkulima: Kweli au si kweli
Mweleze jaji kama wewe sio Mwenyekiti wa CCM tawi la Makiungu.
SHAHIDI: Hiyo sio kazi inayonipatia riziki.
SHAHIDI: Mheshimiwa jaji naomba Ninywe maji, Koo limekauka.
JAJI: SAWA.
T/L. Mweleze jaji. Je ulimwona Cleti Kidamwina kuwa aligawa juisi, maji na biskuti?
SHAHIDI; Mimi naomba niwe mkweli, mimi sikumwona kabisa.
SHAHIDI: SIKU YA UCHAGUZI. Mimi sikumwona kabisa,
T/L. Je ulimwona Kidamwina akiwa na pikipiki yenye shehena ya chakula
SHAHIDI: HAPANA, SIKUMWONA KABISA.
T/L. Je chakula walichotumia mawakala ulijua kilinunuliwa na nani? Kilifikaje makiungu? Nani alikilipia?
SHAHIDI: Sijui katika hayo yote.
T/L. Nimeshitakiwa kuwa nilinunua Chakula, nikagawa, na nilisaidiana na Cleti Kidamwina siku ya uchaguzi je unasema vipi juu ya tuhuma hizi?
SHAHIDI: Mimi nimesema niliyoona yaliyofanyika. Sisemi uongo. Mimi sikuona hayo
T/L. Mwambie jaji kama kweli mawakala wa CCM kila mtu alipewa posho.
SHAHIDI: jaji baada ya Uchaguzi tulipewa 5000/=
T/L. Mwambie jaji, kama kulikuwa na ahadi, kuwa kama mkifanya uwakala kuwa mngekuja kulipwa baadaye.
SHAHIDI: Ahadi haikuwepo ila tulilipwa pesa mawakala wote tuliosimamia uchaguzi.
T/L. Mweleze jaji kama pesa mliyopewa baada ya uchaguzi ilikuwa rushwa?
SHAHIDI. Ilikuwa ni pesa ya Chakula na sio rushwa hata kidogo.
T/L. Umeeleza mahakama kuwa wenzako wa CHADEMA walipewa Juisi, Maji na Biskuti, sasa mweleze jaji, Kwenye Kituo chako ulikuwa unasimamia mgombea urais, Ubunge, na Udiwani ni kweli au si kweli
SHAHIDI: KWELI.
MAJIBU MENGI YA SHAHIDI ANAJIBU SIJUI AU SIKUMBUKI.
T/L. Umesema kuwa katika Chumba ulichokuwepo kulikuwa na mashahidi zaidi ya 5 je ni kweli?
NDIO.
T/L uliangalia hati zao vya viapo?
SHAHIDI. Haikuwa kazi yangu.
T/L. Je uliniona namwelekeza aliyegawa maji?
SHAHIDI: SIKUMWONA
T/L. Vyama vingine vilivyokuwa na wagombea wa Urais, vikawa havina wagombea Udiwani na ubunge, je una uhakika hakutuma mtu kuleta chakula katika kituo?
SHAHIDI: Sijui.
T/L. Uliziona barua za mawakala wa CHADEMA za kuwatambulisha?
SHAHIDI; Sikuziona, na haikuwa kazi yangu.
T/L. Nikisema kwamba kila mmoja alipelekewa barua kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Singida mashariki, wewe unafahamu hilo?
SHAHIDI: Sijui.
T/L. Ulipoona kuwa kuna vitu ambavyo haviendi sawa je uliandika barua ya malalamiko?
SHAHIDI: Ndiyo.
T/L. Anasoma fomu 14. Sikuridhika na zoezi la upigaji kura kwa kuwa karatasi za kupigia kura ni chache, yaani ni 400 wapiga kura 403/, lakini mwisho wakati wa kumaliza uchaguzi karatasi za kura zilibaki.
T/L. Nilikosea au sikukosea mimi kuvaa magwanda ya CHADEMA siku ya uchaguzi?
SHAHIDI; Jibu wewe.
T/L. Mweleze jaji, mliambiwa nini kuhusu kuvaa nguo zenye nembo ya Chama.
SHAHID: SIKUMBUKI.
T/L. Nimeshitakiwa, na jaji ameombwa afute matokeo ya uchaguzi. Kwa ukweli wa Mungu, unadhani ni sahihi mahakama kufuta uchaguzi huu kwa kuwa unahisi aligawa chakula?
SHAHIDI: Ushahidi ndio utakaofanya matokeo yafuwe au yasifutwe:
TUNDU LISSU. Sina swali zaidi mheshimiwa jaji.
Wakili wa Serikali: Sina swali;
Wakili wa CCM: naomba niende MSALANI kidogo nimebanwa
JAJI; Sawa tu ila urudi haraka.
JAJI AMEAHIRISHA KESI TUNARUDI BAADA YA SAA MOJA NA NUSU