Lissu alivyomhoji shahidi leo- kesi Singida

CCM wanakufa kifo cha aibu sana.. huyo shaidi naye wanamlipa? kweli chama kimeshika hatamu
 
Ukiijua sheria mpaka raha! Lissu kanikumbusha kile kitabu 'THE VENICE MERCHANT' mabepari wa venice. Eti shahidi anasema hajui kusoma wala kuandika, hapohapo anasema akivaa miwani anasoma! Teh teh teh!
 
Tundu Lisu unapoamuwa kusimama nae mahakamani tafsiri yake ni kwamba umeamuwa kujidharirisha na watu wakudharau zaidi maana utaumbuka vibaya, ninavyomjuwa mimi Tundu Lisu akikuuliza swali la kwanza ujuwe ameshakuandalia mpaka swali la nne!!...
 
Haya sasa, nahisi huyo wakili wa ccm alihara mpaka akaishiwa nguvu!
 
Ni kweli kesi ni gharama na mashahidi wengine huongea maneno ambayo hayatuingii akilini na kutuachia maswali mengi kama kweli shahidi yuko serious!!!! lakini NDIVYO HAKI na UKWELI UNAVYOTAFUTWA... kumsikiliza kila mtu ambaye anadhani ana hoja ya ushahidi ili hakimu aweze kuamua !!! Nhii ndo gharama ya HAKI na PIA NDO GHARAMA YA DEMOKRASIA.. Mwanafalsa mmoja alishawahi kusema:" If you think democrasy is expensive... Try Dictatorship"
 
sikio la kufa halisikii dawa,rubber stamp ndivyo zilivyo,ukasuku wa kukaririshwa ukaulizwa swali yote hupotea.Inakuwa kama story ya mtu mmoja aliyekaririshwa kiingereza,aliambiwa akiulizwaswali lolote aseme yes,akiendelea kuulizwa tena aseme because of money.Basi ikatokea bahati mbaya kubwa yakatokea mauajio maeneo yale katika kamata kamata aliyekaririshwa naye akakamatwa na kuulizwa maswali kamaifuatavyo:

Hakimu:Do you kill that people?
aliyekariri:Yes
Hakimu:why
aliyekariri:because of money
Hii yote haina tofauti na mashahidi wa kesihiikukaririshwa wakati hawajui nini na ni wapi matukio hayo yalifanyika
 
Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali, halafu kila siku malalamiko kuwa kesi ni nyingi kumbe kesi nyingine za kujitakia tu.
 
isango saa moja nusu likiisha uje tena na kipande cha mwisho..yaani leo nimeshikilia mbavu
 
Kama Jaji F. Welema anamwogopa Lisu. Spika akimwona Lisu kasimama bungeni anaomba muda uishe haraka ama mic zigome jamaa asisikike. Na hawa wote ni wasomi sasa shahidi ambaye hajui A wala Z ya sheria ataweza kusimama na Lisu au ndo kujidhalilisha. Shame on magamba
 
Kijana wangu TL noma, ila Mungu amulinde sana, huyu ni mwanaharakati wa ukombozi wa taifa letu
 
Wakubwa nimecheka sina mbavu! Asante sana bwana Isango. kimsingi hapo mahali na watu wote ni home kabisa...kila mtu namfahamu fika.
Shahidi, MATHEW COSMAS alikuwa mwalimu angu enzi hizo, baadaye akaacha akawa anauza nyanya pale sokoni Makiungu.

Asante sana bwana Isango, hii ni burudani tosha. Kwa kweli Makiungu tulifanya kazi kubwa sana ya kumnadi Tundu Lisu hata kabla ya uchaguzi...niliwaambia jamaa...Tundu Lissu akigombea tena ubunge (aligombea mwanzo 1995) msifanye mzaha...namjua ni jembe hasa. Nashukuru Mungu wengi walituunga mkono na mamo yakawa hivyo. Hao mashahidi wa CCM ukiwaona ndugu yangu utasikitika... wamechoka...teacher yy ni hoi...kuuza nyanya tu. Sophia ni ndugu yangu kabisa kiukoo...yy ni muuza tu gongo na pombe za kienyeji. Tliwaeleza hawakusikia, wakaendekeza njaa...ona sasa teacher anatoka mbio chumba cha mahakama kwenda kuharisha...kisa 5000/!
 
sheria waliitunga wao, ngoja iwakandamize mwanawane, hata hivvyooo si tulisikia wakili wao amekimbia kesi, tena ni bora warudi shule,
 
Wakuu nimecheka sana jinsi huyu shahidi wa ccm anavyojichanganya! kazi wanayo ccm kwa T.L
 
Back
Top Bottom